mdesi
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 1,373
- 2,251
Habarini wanajamii..
Mimi ni mkristo wa moja ya madhebu ya kikristo, huwa napenda kuheshimu kila imani ya mtu, hata kama haamini vile namini. Kilichonifanya kuja hapa; ni mashambulizi ya kihasira ya mda mrefu ambayo madhehebu mengine yanafanya dhidi ya hili dhehebu la kakatoliki au RC kama wanavyoita wengine.
Vitendo hivyo vilinifanya nianze kulifuatilia kwanini linashambuliwa tena wakati mwingine kwa matusi, na kwanini watu wanazingatia na kuudhiwa na imani ya mtu mwingine?
Katika kudadisi nikagundua SDA ndo wako mstari wa mbele wakifuatiwa na madhehebu mengine, ugomvi mkubwa ni kusali siku ya jumapili badala ya juma mosi, yaani wanaosali jumamosi ni kama hawajiamini hivyo kutumia nguvu kubwa kuwainesha wengine kuwa wako sahihi.
Zaidi ni wanalituhumu kuwa wana abudu sanamu, zaidi wanawapinga kuwa na sikukuu zao mbali mbali km vile Ijumaa kuu, Pasaka, Noel, etc. Cha ajabu hao wa RC ktk kuchangamana nao sijawahi ona wakidharau au kutukana madhebu mengine, hilo lilinifikirisha sana.
Nikafuatilia ibada zao including zile za juma pili na hizi za Alhamis na Ijumaa kuu, nimeona ni ibada ziko very calm, deep and very well organized, tofauti na nitokako (sina dhamira ya kuhama dhehebu langu).
Jambo lingine ambalo nime gundua madhebu mengi (including mine) kwa namna fulani yamefuata wakatoliki wanavyofanya nitatoa mifano michache:
I. Sikukuu za kidini:
Hapo kale dhehebu langu lilikuwa kama halijali hizo sikukuu, ila sikuhizi lime adopt ingawa hakuna miongozo ya nini hasa siku hiyo kinatakiwa kufanyika. Mfano kuna jumatano ya majivu ila hatupaki, kuna alhamisi na ijumaa kuu, usiku wa pasaka na pasaka. Niliwahi kusali RC pasaka mojawapo ya usiku, niliona wana mambo ambayo yako organised mahususi kwa siku hiyo and is like everywhere they do the same.
II. Kusali siku ya jumapili:
Na sisi tunasali siku ya jumapili kama RC ila hatushambuliwi hata kidogo na SDA kama wanavyoaashambulia RC, hapo sijauja ni kwa nini...
III. Kuwa na jumuiya mitaani:
Hapo awali hatukuwa na utaratibu huo, ila baadae ukaanzishwa km wafanyavyo RC.
IV. Mavazi ya wachungaji na maaskofu.
Wa kwetu wanavaa ya mfanano na RC hata askofu anavaa kofia ina pembe mbili na miraba miwili nyuma ila ile inavaliwa na maaskofu wa RC inasemwa kuwa ni alama ya 666 ila ya kwetu haisemwi hivyo kabisa.
V. Mazishi ya wafu:
Utafauti ni kuwa wa RC mtu akifariki huwa wawazi kabisa kuwa kwa imani yao wanaamini kuwa mtu akifariki hawezi fanya lolote tena, ila wana amini wanaobaki kwa maombi yao yanasikilizwa na Mungu hivyo kumuombea marehem, Mungu wa rehema anaweza msamehe makosa wakati wa hukumu kwa aliyetangulia.
Huku kwangu haiko wazi mtu akifariki tunasema habari yake imeishia hapo na hatuna utaratibu wa kuombea ila huwa tunafanya ibada kanaisani ingawa haiko specific.
Haya machache na mengine mengi dizain km tuna follow what RC has been doing.
My take ni kuwa ifike pahala tuache kushambulia imani ya mtu mwingine, ambaye haamni km unavyo amini wewe. Kunahaja gani ya kutoa lugha chafu za hasira kwa kitu ambacho hakikuhusu na haki athiri unacho kiamini wewe?
Matokeo yake madhebu ya kikristo yamekuwa ni mengi mno na makanisa binafsi yanazidi kujitokeza kila leo. Ila hawa wenzetu wakuwa watulivu hawabishani wala kuwatukana wenye mtazamo tofauti. Hakuna mwenye hati miliki ya Mungu. Mungu ni wetu sote ila namna ya kuwasiliana nae kila madhebu yana namna yao ila tusitake namna yako iwe yangu. Nawapenda sana!!