Lengo la huu uzi si kuhamasisha watu kuachana na masomo bali ni kujadili kwa pamoja njia walizotumia baadhi ya wanafunzi walioacha shule hadi kufikia mafanikio. Kumbuka kuna wengine waliacha shule na hawakufikia mafanikio yoyote pia kuna wengine waliendelea na shule hadi kuhitimu tena kwa madaraja/ufaulu mzuri lakini pia hawakufanikiwa kutimiza malengo yao. Wana JF hebu tujadili kwa pamoja mambo mbalimbali yanayoweza kutuletea mafanikio kwa kutumia mifano michache ya hawa waliofanikiwa tena bila kusoma vyuo vikuu. Ili kusiwe na kisingizio cha elimu hebu tujadili mambo ya msingi yanayoweza kutufanikisha katika malengo yetu. Bila kubagua waliosoma na wasiosoma maana wote wanahitaji mafanikio.
Kwa miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia ongezeko kubwa la wasomi na wahitihu wa elimu ya juu katika vyuo tofautitofauti, na kupelekea ongezeko kubwa la ukosefu wa ajira katika maeneo mengi duniani. Hapa nchini pia tatizo la ajira ni kubwa sana kuliko watu wanavyolichukulia. Sasa tunawezaje kujiendeleza na kutimiza malengo yetu na kuwa na maisha mazuri kwa kutumia njia mbadala ya kupata ajira kupitia ujasiriamali?
HOWEVER, there list of people who dropped out and didn't succeed / lost opportunities because of that is much much larger. Your Degree is like a little savings account for a rainy day: when you really need it - you'll be able to fall back on it. What if your 1st or 2nd idea doesn't pan out and you need something in between while you are getting ready for your 3rd idea? So stay in school
- Bill Gates - moja kati ya waanzilishi wa Microsoft - utajiri wake ni $78.8 Billion. Aliacha chuo cha kikuu cha Harvard akiwa na miaka 19.
- Steve Jobs - muanzilishi mwandamizi wa kampuni ya Apple Inc - Jumla ya utajiri wake $8.3 Billion - Aliacha chuo baada ya kusoma muhula mmoja (semester)
- Mark Zuckerberg - CEO na moja kati ya waazilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook - Jumla ya utajiri wake $33.7 Billion - Aliacha chuo (Harvard) akiwa na miaka
- Michael Dell - Mwanzilishi wa komputa za Dell (Dell Computers) - Jumla ya utajiri wake $20.1 Billion - Aliacha chuo cha Texas akiwa na miaka 19.
- Larry Ellison - moja kati ya mwanzilishi na CEO wa zamani wa kampuni ya Oracle - Jumla ya utajiri wake ni $47.6 Billion - Aliacha chuo kikuu cha Chicago akiwa na miaka 20.
- Jan Koum- CEO na mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Whatsapp - Jumla ya utajiri wake ni $8.6 Billion - Aliacha chuo kikuu cha San Jose akiwa na umri wa miaka 20.
- Travis Kalanick - CEO and moja kaji ya waanzilishi wa kampuni ya kimtandao ya Uber - Jumla ya utajiri wake ni $6.2 Billion - aliacha chuo cha UCLA akiwa na miaka 21.
- Evan Williams - moja kati ya waanzilishi na CEO wa zamani wa mtandao wa kijamii wa oftwitter - Jumla ya utajiri wake ni $1.71 Billion - Aliacha chuo kikuu cha Nebraska–Lincoln akiwa na miaka 20.
- John Mackey -mwanzilishi wa kampuni ya Whole Foods - utajiri wake ni $ 100 million - Aliacha chuo kikuu chaTexas - Austin akiwa na miaka 22.
- Paul Allen - moja kati ya waaanzilishi wa kampuni ya Microsoft - Utajiri wake $17.7 billion - Aliacha chuo kikuu cha Washington State University akiwa na miaka 20.
- Dustin Moskovitz - Moja kati ya waanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook - Utajiri wake $9.2 Billion - Aliacha chuo Harvard
- Leslie Wexner - CEO wa L Brands - Utajiri wake ni $7.2 Billion - Aliacha chuo kikuu cha Ohio State
- Elizabeth Holmes - CEO na mwanzilishi wa Theranos - Net Worth $3.6 Billion - Aliacha chuo kikuu cha Stanford
- Jack Dorsey - CEO na moja kati ya wanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Twitter- Utajiri wake ni $2.3 Billion - Aliacha chuo kikuu cha New York.
- Gabe Newell - moja kati ya waazilishi na managing director wa kampuni ya gemu za video ya Valve - Utajiri wake ni $1.3 Billion – Aliacha chuo kikuu cha Harvard.
- Stacey Ferreira - mwanzilishi wa Forrge and moja kati ya waanzilishi wa Mysocialcloud - Aliacha chuo kikuu cha New York - Anamiaka 23 !
- Ralph Lauren - Mwanzilishi wa shirika la Ralph Lauren - Utajiri wake ni $5.6 billion - Aliacha chuo cha Baruch.
- Evan Spiegel - CEO na moja kati ya waanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Snapchat - Utajiri wake ni $2.1 billion - Aliacha chuo kikuu cha Stanford.
- Sheldon Adelson - Mwanzilishi wa shirika Las Vegas Sands - Utajiri wa $25.8 billion - Aliacha chuo cha City College of New York
Images source: Wikipedia and google images
Kwahisani ya Quora