Pointi ni kuwa kutokana na uchache wao, hao wahindi hupendelea kuishi karibu na wahindi wenzao, kwa familia ya kihindi kumpeleka mtoto wao shule ya bweni ambayo mtoto ni minority kila kona hakuna wahindi wezie wao wanaona ni sawa na kumtelekeza mtoto.
Hivi hata wewe mtu mweusi utajiskiaje umpelekee mwanao shule ambayo wapo wahindi watupu yeye ahesabike jinsi alivyotofauti??
Lazima utahisi kuna kitu hakiko sawa, lazima at some point uhisi kuwa ni rahisi sana kwake kuonewa
Ndio maana hata mitaa wanayoishi, wahindi hupenda kuishi na wenzao, ndio maana wanaishi posta ama kariakoo, na Msione wana raha sana, kodi za huko posta ni kubwa sana kulipa, ila wanajitutumua kuishi huko, mradi tu wasiende kuishi maeneo ya mbali sana kama tunaoishi sisi waafrika ambako wao wakija kuishi watakuwa ni minority