Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Hili la wabunge kutaka kujadili masuala ya mahakamani bungeni ni kuingilia mamlaka ya mhimili mwingine. Suala la kesi za jinai dhidi ya Tundu na Jonathan yapo mahakamani, kwanini yanaingiliwa na wabunge? kwani mbunge anakinga kutoshitakiwa kwa kwa jinai? kwanini waache kujadili masuala ya wananchi wajadili masuala ya mbunge binafsi ambaye yupo kwenye mikono ya sheria?
Lazima wabunge wajue hakuna mwananchi anayeweza kugoma au kuumizwa na mbunge kufikishwa kortini kwa makosa binafsi. Zile hoja za kamati ya miundombinu nk na Tundu nani muhimu?
Zitto alifanikiwa kuleta habari ya 'kutorokea ughaibuni' ili kujenga taswira ya kuwa wapinzani kunyanyaswa wakati kasafiri kwa mambo binafsi, sasa anawateka wajinga kwa kutoa 'unabii' ya kuwa maafisa wa bunge wamemtonya kuwa aatakamatwa na polisi. Kwa kawaida polisi hukamata wabunge nje ya eneo/uzio wa bunge na hawahitaji kuwataarifu askari wa bunge, HUU ni UONGO.