Kwanini wabunge hawapendekezi punguzo la kodi kwa bidhaa za watoto?

ruukada

Member
Feb 24, 2014
67
117
Hivi kwanini sijawahi kusikia wabunge (si wa upinzani si CCM) wakipigania punguzo la kodi kwa bidhaa za watoto kama vile maziwa, vyakula, elimu ya awali na hata mavazi.!!

Hivi wananchi wa kijijini na hata wa mjini "na ni wengi" wanaweza kununua maziwa ya mtoto kwa tshs 20,000/ au 40,000/ au 60,000/ kwa kopo linalokaa wiki moja?

Je, wanaweza kununua vyakula vya virutubisho vya mtoto wa miezi mitatu mpaka mwaka.

Je, wanaweza kupeleka watoto wao kuanza elimu ya awali?

Au ni kwa ajili ya matajiri tu? Au ni kutokujali kizazi cha watanzania waliowengi.?

Nchi nyingi zilizoendelea hata nyingine ambazo hazijaendelea wana punguzo kubwa la kodi kwa bidhaa za watoto au wametoa kabisa. Hii inasaidia watoto wengi waweze kupata lishe bora na kuondoa ama kupunguza utapiamlo na kupata malezi yasiyotofautiana kwa kiasa kikubwa cha kutisha kama ilivyo sasa.

Wamama wengi waliojifungua,, siku hizi hawatoi maziwa ya kutosha mtoto kushiba na wengine wengi maziwa yanakata mapema , yote hii ni kutokana na ugumu wa maisha unaosababisha kutokula vizuri na msongo wa mawazo.

Ndio maana maziwa na vyakula mbadala vya kumuezesha mtoto kushiba na kupata virutubisho kama lactogen na cerelac vikatengenezwa.

Ni nchi pekee ambayo gharama ya kulea mtoto kwa standadi ya kawaida inayokubalika ni kubwa mno kuliko nchi nyingi duniani.

Na hii ni kuanzia ;-
1. Vyakula vya watoto, (mfano cerelac, lactogen ni kuanzia 15,000,20,000 na kuendelea)
2. Matibabu pamoja na dawa (
3. Elimu ya awali (baby care- zinaanzia laki nane mpaka millioni 3 na zaidi)
4. Mavazi ( bei kama nguo za watu wazima na nyingine kuzidi)

Wazo langu:
Wabunge mnabidi mjifunze kutetea vitu vinavyogusa maisha ya watanzania waliowengi mjini na vijijini kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha baadae na sio kutetea kundi dogo la watanzania kwa ajili ya faida binafsi.
 
Wazo langu:
Wabunge mnabidi mjifunze kutetea vitu vinavyogusa maisha ya watanzania waliowengi mjini na vijijini kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha baadae na sio kutetea kundi dogo la watanzania kwa ajili ya faida binafsi.[/QUOTE]
Hao wabunge unataka watetee unachosema dhidi ya nani?Mbona usiseme hiyo serikali yenyewe ilione kama ambavyo wanavyopandisha au kufuta kodi zingine?Au jitahidi kupeleka hayo mapendekezo kwa serikalini kama short cut.Maana makusanyo ya serikali hii ni madogo adi wamefikia kuhalalisha kula Rambirambi.
 
Hivi kwanini sijawahi kusikia wabunge (si wa upinzani si CCM) wakipigania punguzo la kodi kwa bidhaa za watoto kama vile maziwa, vyakula, elimu ya awali na hata mavazi.!!

Hivi wananchi wa kijijini na hata wa mjini "na ni wengi" wanaweza kununua maziwa ya mtoto kwa tshs 20,000/ au 40,000/ au 60,000/ kwa kopo linalokaa wiki moja?

Je, wanaweza kununua vyakula vya virutubisho vya mtoto wa miezi mitatu mpaka mwaka.

Je, wanaweza kupeleka watoto wao kuanza elimu ya awali?

Au ni kwa ajili ya matajiri tu? Au ni kutokujali kizazi cha watanzania waliowengi.?

Nchi nyingi zilizoendelea hata nyingine ambazo hazijaendelea wana punguzo kubwa la kodi kwa bidhaa za watoto au wametoa kabisa. Hii inasaidia watoto wengi waweze kupata lishe bora na kuondoa ama kupunguza utapiamlo na kupata malezi yasiyotofautiana kwa kiasa kikubwa cha kutisha kama ilivyo sasa.

Wamama wengi waliojifungua,, siku hizi hawatoi maziwa ya kutosha mtoto kushiba na wengine wengi maziwa yanakata mapema , yote hii ni kutokana na ugumu wa maisha unaosababisha kutokula vizuri na msongo wa mawazo.

Ndio maana maziwa na vyakula mbadala vya kumuezesha mtoto kushiba na kupata virutubisho kama lactogen na cerelac vikatengenezwa.

Ni nchi pekee ambayo gharama ya kulea mtoto kwa standadi ya kawaida inayokubalika ni kubwa mno kuliko nchi nyingi duniani.

Na hii ni kuanzia ;-
1. Vyakula vya watoto, (mfano cerelac, lactogen ni kuanzia 15,000,20,000 na kuendelea)
2. Matibabu pamoja na dawa (
3. Elimu ya awali (baby care- zinaanzia laki nane mpaka millioni 3 na zaidi)
4. Mavazi ( bei kama nguo za watu wazima na nyingine kuzidi)

Wazo langu:
Wabunge mnabidi mjifunze kutetea vitu vinavyogusa maisha ya watanzania waliowengi mjini na vijijini kwa ajili ya kizazi cha sasa na cha baadae na sio kutetea kundi dogo la watanzania kwa ajili ya faida binafsi. Na Serikali mnabidi mjifunze kujali watoto wenu kama mali ya nchi jifunzeni kwa wezenu.
 
MIMI WANGESAIDIA TU KUPUNGUZA BEI KATIKA VYAKULA INGESAIDIA SANA.WAKITAKA KUPIGA BAO 2020 WAPUNGUZE MFUMKO WA BEI KATIKA VYAKULA.
 
Back
Top Bottom