Wakiwemo wahenga waliotumia vyoo vya shimo. Hivi ni kwanini hivi vyoo vilikua au hua vinatitia au kuharibika au kutumbukia usiku na mara chache sana kwenda na mtu yani kutitia na mtu.
Nilikua najiuliza sana utotoni kwa nini hiki choo chetu kinatumbukia usiku tena bila ya mtu kuwepo chooni? Mara nyingi sana nilikua naona bora nikajisaidie porini nifunge safari kabisa kuliko kuingia choo chenye mashaka. Nilikua naona wazazi hawaogopi kutumbukia ila mimi mtoto naogopa, nikawa nahisi kunatechnique wanatumia.
Bado swali langu KWANINI HIVI VYOO HUTUMBUKIA AU HUTITIA USIKU NA SIO MCHANA? Wale wataalamu wa phisics nikwamba usiku density au mgandamizo ardhini unakua wa juu sana? Au ni nini hasa.
Tafadhali sana naomba kujuzwa kama na wahenga au wanasayansi katika hili kuna uhusiano wowote.
Mkuu kweli kabisa.Wakati nikiwa mdogo kuna siku tumelala mara usiku saa tisa hivi tukaskia kishindo nje.Kutoka nje tukakuta kile choo chetu cha shimo kimezama asee.Sijui kwanini mkuu
Hesabu zinaweza kutusaidia kutatua hicho kitendawili.
Tuseme kwa siku nzima ukijumlisha muda wote ambao kuna mtu chooni ni kama dakika 30 hivi.
Kwahiyo probability ya kuwepo mtu chooni kwa siku ni (30/(24×60)) = 0.020833 = 2.0833%
Tuseme kwa mwaka kuna uwezekano wa choo kubomoka mara moja (msimu wa mvua kubwa labda).
Kwahiyo probability ya choo kubomoka kwenye siku yoyote ya mwaka ni (1/365)= 0.0027397 = 0.27397%
Kwahiyo uwezekano wa choo kubomoka katika mwaka wakiti kukiwa na mtu ndani ya choo ni
(0.0027397 ×0.020833) = 0.0000570767 = 0.00570767%.
Kwahiyo unaweza ukaona kua ni vigumu sana kwa choo kubomoka kukiwa na mtu ndani japo inaweza kutokea.
Kuhusu choo kubomoka usiku sina uhakika, mimi nakumbuka wakati wa mvua kubwa ilikua usithubutu kwenda chooni la sivyo watakuja kukutoa na kamba na utakua story kijijini kwa mwezi mzima.
"vyo vya shimo"? hivi kwani vyoo ambavyo sio vya shimo?
Labda ungesema "vyoo vya kienyeji" ambavyo sio vya kuflash na Maji au mashimo ya vyoo vya kuflash yaliyojengwa kienyeji pasipo kutumia cement.
Ila uchunguzi wako una ukweli, nadhani usiku kuna kuwa na unyevu zaidi kwenye shimo "udongo" kuliko mchana. Hii ni kwasababu ya lile joto la usiku ndani ya shimo.
"vyo vya shimo"? hivi kwani vyoo ambavyo sio vya shimo?
Labda ungesema "vyoo vya kienyeji" ambavyo sio vya kuflash na Maji au mashimo ya vyoo vya kuflash yaliyojengwa kienyeji pasipo kutumia cement.
Ila uchunguzi wako una ukweli, nadhani usiku kuna kuwa na unyevu zaidi kwenye shimo "udongo" kuliko mchana. Hii ni kwasababu ya lile joto la usiku ndani ya shimo.