Sema Tanzania
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 251
- 466
Hivi karibuni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) kilitoa ripoti ya nusu mwaka (kuanzia mwezi 1-6) kuhusu mwenendo wa haki za binadamu nchini. Taarifa ambayo haikuwa njema zaidi katika ripoti hiyo, ni ile iliyoarifu juu ya ongezeko la vitendo vya ubakaji na ulawiti dhidi ya watoto. Ripoti hiyo ilibainisha kuwa kwa kipindi cha mwezi Januari hadi mwezi Juni mwaka 2018 kati ya matukio 6,376 ya ukiukwaji wa haki za watoto, 2,365 yalitokana na ubakaji (takwimu ambazo ni sawa na watoto 394 kwa siku) huku matukio 533 yakihusisha watoto kulawitiwa.
Kimsingi, uchambuzi wa ripoti hiyo ulibainisha kwamba idadi ya vitendo vya ubakaji na ulawiti dhidi ya watoto nchini umeongezeka maradufu ikilinganishwa na ripoti ya nusu ya kwanza ya mwaka 2017 ambapo matukio ya ukiukwaji wa haki za watoto yalikuwa 4,728 huku watoto 759 pekee walibakwa na watoto 12 wakilawitiwa.
Kwanini mtu mzima abake ama alawiti mtoto? Vitendo vya kubaka watoto vipo kote duniani kwa muda mrefu. Kinachoshangaza hasa ni katika miaka ya hivi karibuni hali imekua kwa kasi ya kutisha zaidi siku hadi siku. Ukuaji huu pamoja na taarifa za vitendo hivi vimesababisha hofu kubwa kwa jamii jambo ambalo hutufanya baadhi ya wazazi ama walezi tusijue nini cha kufanya. Wakati haya yakiendelea kufanyika pengine wazazi hatutambui nini hasa kinachomfanya mtu kufikia uamuzi wa kumbaka mtoto ama kumlawiti ilhali mtu huyo pengine anatambua kwamba kufanya hivyo ni kosa ambalo adhabu yake ni kali.
Ieleweke kwamba zipo sababu kadhaa ambazo huwafanya watu kujihusisha na ubakaji. Moja ya sababu hizo ni ile ya kisaikolojia ambayo kitaalamu hujulikana kama “Paedophilia”. Tunaweza sema haya ni matatizo ya kiakili ambayo mtu mzima huyapata ambapo muda wote hutawaliwa na tamaa ya kujamiiana na mtoto wa umri mdogo hata kama mtu huyo anao mbadala wa kujamiina na mtu mzima mwenzake. Wanaougua maradhi haya mara nyingi ni wanaume na hutumia pesa, zawadi na lugha zenye mvuto ili kuwarubuni watoto na mara kadhaa hutumia hata nguvu ili kufanikisha azma yao.
Sababu nyingine ni uigaji wa mambo na msukumo unaotokana na makundi rika. Vijana wadogo na hata watu wazima husukumwa na hulka za makundi rika kutafuta na hata kufanya mapenzi na watoto wa umri mdogo ama kwa kupalilia sifa na hata kuwaharibia watoto husika safari za maisha. Fikra hizi potofu ni pamoja na ‘umwamba’ wa kujigamba kumtoa ‘bikra’ mtoto wa hapo mtaani / kijijini bila kujali madhara yatokanayo na vitendo hivi.
Aidha, baadhi ya watu wazima huamini kuwa ni rahisi sana kumrubuni kimapenzi mtoto mdogo kuliko mtu mzima na hivyo mtu huyo anapofanikiwa mara moja huendeleza na kueneza tabia hiyo kwa wengine. Pia ubakaji huchochewa zaidi na imani za kishirikina kwa waumini wa ushirikina waliojenga imani kwamba kupata utajiri kunafanikishwa kwa njia ya kujamiina na watoto wadogo wakiwemo watoto wao (wa kuwazaa) jambo ambalo si la kweli.
Wazazi tunapaswa kufanya nini ili kutokomeza vitendo hivi? Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 sehemu ya pili (2) inatoa wajibu na majukumu ya mzazi katika kumlea na kumlinda mtoto. Sheria inaeleza kuwa “Kila mzazi atakua na wajibu na majukumu yaliyowekwa ama na sheria au vinginevyo kwa mtoto wake ambayo yatajumuisha wajibu wa kumlinda mtoto dhidi ya utelekezwaji, ubaguzi, vurugu, unyanyasaji, madhara ya kimwili na kiakili na ukandamizaji”.
Ulinzi wa mtoto hauwezi kufanikiwa kama hautomuhusisha mtoto katika kujilinda. Tunapendekeza mzazi amshirikishe mwanae katika kuzitambua athari anazoweza kuzipata hasa pale anapofikia balehe. Mweleze aina zote za vishawishi kadiri unavyozielewa na mpe uhuru wa kukueleza mahusiano yake na mapito yake ya siku hata siku.
Pamoja na hayo ili kumaliza matukio haya jamii kwa ujumla tunapaswa kuacha utamaduni wa kuwalinda wabakaji, sharti tushikamane kwa kuwafikisha kwenye vyombo vya dola ili wachukuliwe hatua za kisheria bila kujali undugu. Tupaze sauti zetu katika kupinga ubakaji na ulawiti dhidi ya watoto ili madhara ya vitendo hivi yamguse kila mmoja katika ngazi tofauti. Tuongeze juhudi za kusimamia mabadiliko ya sera na sheria kandamizi bila kusahau mikakati ya Kitaifa ya kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vyote vya kikatili.
Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania, Twitter: @SemaTanzania na www.sematanzania.org