Hivi uongozi km wa mkwere utaandika nn kwa mfano?!Kwanin viongozi wetu hawaandiki juu ya uongozi wao na CHANGAMOTO ili wananchi wafaham ukweli na pia wajifunze?
Hii ni ndoto yangu pia. Lowassa naye angeandika. Tuwahamasishe waandike ili maswali mengi watueleze kwa niniNApenda Dr. Salim aandike Kitabu.
Jk pia,aeleze kiundani kipi kilitokea ile tar.1Julai..
Mwingine Balozi Lusinde.
nashangazwa na hii tabia ya viongozi wetu kustaafu na kupotelea gizani bika kuacha kumbukumbu yoyote.Kwanin viongozi wetu hawaandiki juu ya uongozi wao na CHANGAMOTO ili wananchi wafaham ukweli na pia wajifunze?
Kikwete anaweza kutwambia kuhusu safari yake ya kwanza na Lowassa kwenda Dodoma mwaka 1995 na ya mwisho mwaka 2015. Maamuzi ya kumpenyeza Magufuli badala ya Lowassa. Kuna escrow na EPA pia.Hivi uongozi km wa mkwere utaandika nn kwa mfano?!
thubutuuu..!!!Sawa sita ataandika lakini je ataandika ukweli au ni kupotosha tu, je anaweza kuandika jinsi alivyosimamia marehemu na wagonjwa wapige kura kwenye bunge la katiba, je anaweza kuandika jinsi alivyokuta macontainer yanapita bandarini bila kulipiwa na yeye akahamua kukaa kimya.Nafikri kwa sasa anayeweza kuandika ni Dr salm amed Salm na Jaji warioba
Kwanin viongozi wetu hawaandiki juu ya uongozi wao na CHANGAMOTO ili wananchi wafaham ukweli na pia wajifunze?
Kwanin visisomwe?Wakiandika Utavisoma? Kila jambo lina sababu hapa Duniani!
Kwa ujumla Watanzania hatuna utamaduni wa kusoma vitabu. Ukitaka visomwe may be viingizwe katika mtaala mashuleni. Ndiyo maana kwa sasa Wakenya wanachapisha vitabu vingi sana hasa kwa upande wa Kiswahili kwa sababu soko lao la vitabu ni zuri kuliko sisi. Sisi kama kitabu chako kisipopitishwa kutumika mashuleni basi hakuna mtu atakayekisoma. Hata lile vuguvugu la miaka ya sabini na themanini la kusoma vitabu vya kipelelezi vya akina Musiba, Katarambula, Mtobwa na wengineo sasa halipo tena. Inasikitisha!Kwanin visisomwe?