Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Kwenye nchi nyingi zinazotekeleza demokrasia ya kweli pindi kiongozi yeyote wa chama kinachoshindwa uchaguzi huwa anajiuzulu kwenye mambo ya siasa ndani ya chama na kuachia wanasiasa wengi washiriki uongozi wa chama. Mfano wakati wa uchaguzi wa Uingereza mwaka 2015 kiongozi wa chama Labour Edward Samuel Millband akiwa na umri wa miaka 46 alijiuzulu kukiongoza chama chake baada ya kushindwa uchaguzi mkuu huo.
Hapa Tanzania tumeona viongozi kama Seif Hamad akiwa mgombea pekee wa chama katika kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar kwa chaguzi tano, na chama cha Chadema tumeona Mwenyekit ni yuleyule katika kusimamia chaguzi za chama hicho toka chama hicho kianzishwe. Ni vyema vyama hivi katika uchaguzi ujao wajipange kuleta demokrasia ndani ya vyama vyao kwa kuleta wagombea Urais wengine badala ya kuendelea kuwatumia wagombea/viongozi wameshiriki chaguzi za nyuma.