Habari wana JF na Watanzania.
Poleni kwa namna mnavyopambana kuipata kesho yenu yenye uhakika.
Sote tumekuwa tukiwasikia viongozi wa serikali hii ya CCM wakijitapa kwa majigambo na vijambo kuwa serikali yao imefanikiwa na sasa mambo ni muswano kabisa mtaani. Wanajitapa kwamba wanaleta maendeleo kwa kasi ya mwanga. Yule mwenyekiti wa chama chao kila mara ahutubiapo hutaja takwimu wa waliyoyatekeleza kuwa sasa watanzania tunaneemeka na serikali hii.
Husema mengi na kutaka kuwaaminisha walimwengu kwamba sasa aliyekuwa anakula nusu mlo ana uhakika wa angalau mlo mmoja kwa siku, naye wa mlo mmoja sasa anaweza kula miwili kwa siku, na hata wa milo miwili sasa amekuwa wa milo mitatu na mboga saba.
Sisi wengine kila tukijaribu kuangalia wale wananchi ktk nchi hii naona sura zimekunjamana, wamejaa huzuni, wako hoi na hawana uhakika wa kesho yao.
Wadau mbalimbali vikiwemo vyama vya upinzani wamekuwa angalau wakikosoa kwamba hali ya uchumi ni mbaya na hata hayo "matakwimu" yao hayaakisi ukweli kwani mtaani "vyuma vimekaza". Hao wote waliishia kujibiwa kwamba wanaolalamika walikuwa ni "wapiga dili", na sasa "makufuli" yamefungwa; no dili. Nikajiuliza sana hivi kweli mtaani kumejaa wapiga dili, tena hawa wa hali ya chini hivi. Je, ni dili gani hizo ambazo kina mama ntilie walikuwa wanazipiga, machinga na wengine?!.
Angalau juzi mwenyekiti wao mkuu akiwa ktk mkutano wa walimu Dodoma CWT, alionesha kukiri ingawa kwa shingo upande pale aliposema 'kama vyuma vimekaza, basi wekeni grisi', (nukuu sio rasmi). Ingawa akaongezea kwamba bado wanaolalamika ni wale waliokuwa wapiga dili hasa za "hewa...., hewa...,".
Sasa juzi kuna "thread/Uzi" uliletwa humu JF ukiwa ni wa mdau mmoja wa UVCCM, akijitambulisha ni Komredi kutoka Tanga. Mimi sijui maana ya Komredi kwamba huyu nae ni komredi..
Anyway, hoja yake kubwa ni "waraka wa wazi kwa mhamiaji Albert Msando kuhusu UVCCM".
Alisema mengi akimkosoa mhamiaji wao na akitaka "makomredi" waombwe msamaha.
Mimi kama mmoja wa watu ambao mioyoni mwetu tunaumia sana na Tanzania ijayo, nikadaka point moja ktk andiko lile..
Sehemu ya waraka ule anasema..
"... ..."
Kwamba UVCCM ina vijana jumla milioni 6, na waliohai kiuwanachama ni milioni 1.4
Akasema kwamba hao wengine milioni 4.6 miongoni mwao ni wale ambao wameshindwa kulipa ada za uanachama, wale walioondolewa, labda na kufa. Ukiipitia idadi utakuta wengi katika hiyo milioni 4.6 wameshindwa kulipa ada zao za kila mwezi ktk matawi yao ya chama.
Hii unatupatia picha gani? Je, vyuma vimekaza kwa hao vijana milioni 4. Na je, ndio hao wapiga dili anaozungumzia mwenyekiti wao?
Je, kwa nini huko nyuma waliweza kulipa ada zao na leo hii washindwe ilihali tunaambiwa maendeleo sasa ni dhahiri ni maziwa na asali?
Je, kama kweli hao milioni 4 ni wapiga dili, ni sahihi kwamba idadi kubwa ya vijana wa CCM waliishi kiujanja ujanja na bado ndio sehemu kubwa ya mtaji wa UVCCM na CCM kwa ujumla?!
Nina uhakika ada ya mwezi ya uanachama hata ukitajiwa hapa ni ndogo na utashangaa ni vipi idadi kubwa hiyo washindwe kulipa?
Hivi unaweza vipi kuwaambia watu kwamba hali ni nzuri mtaani wkt wanachama wako hata uwezo wa kulipa ada ya mwezi hawana. Lazima ujitoe ufahamu ili kutamka hilo ama uwe mwehu flani.
Wapo wataotetea hapa na kusema wananyoosha nchi, mara wanasafisha nchi sasa kwa nini msiwanyooshe kwa kuwafuta kabisa hao milioni nne uanachama maana hawana kitu na hawawezi kulipa ada na obvious kama alivyosema mkuu wa chama chao hao ni "wapiga dili".
Yapo mengi lakini gumu zaidi ni hili ..
Je, inawezekana kabisa hao milioni 4 wana hela na uwezo wao vizuri tu lakini wameamua kutokulipa ada kwa maamuzi yao.
Je, bado CCM inapendwa kama amnavyo nyinyi wana CCM na hao wahama vyama wanaosema sasa wanahama kuunga mkono juhudi na mafanikio ya Bwana mkubwa?! Mmmhhh..
Hapa UVCCM mmeamua kuivua nguo CCM yenu. Poleni..!!