Kwanini utembelee Nanenane?

Kwanini utembelee Nanenane?

Ahead

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2013
Posts
2,410
Reaction score
2,735
Ikiwa leo ndio siku ya mwisho ya maonyesho haya ukifika utapata faida zifuatazo:
1.Kuziona mashine mbalimbali za kilimo
2.Kupata elimu ya kilimo na teknolojia mpya
3.Kuona wanyama mbalimbali wa mwituni na wakufugwa
4.Utashuhudia michezo ya watoto kama vile treni ya watoto hivyo nenda nae akafurahi
5.Mbali na ishu za kilimo utapata kuona na kununua bidhaa za makapuni mbalimbali ya biashara
6.Huduma karibu zote zinapatikana ndani ya viwanja vya nanenane kama vile benki,hotel/migahawa,vyoo.
Ikiwa upo Dodoma,Mwanza, Tabora,Mbeya na Lindi fanya ufike nanenane hutojutia muda wako karibu sana,hapa nimeeleza kwa kifupi.
 
Nilibahatika kutembelea jana,,,na kugundua wizi mkubwa sana pale kwenye lango la kuingilia.....risiti zimekatwa mapema,na hazina muda sahihi...pia ukilipia haupewi risiti mpaka pale utakapoidai...whoever is concerned na makusanyo,kapigwa hela nyingi sana na wale vijana.
Wizi mtupu!!!!Its a shame hata waandaaji hawalioni hili
 
Back
Top Bottom