barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,874
Toka nimefikia umri wa kuwa na akili za kutambua mambo,mpira ni jambo mojawapo nililokuwa nalifuatilia kwa ukaribu sana.Toka enzi hizo mpaka leo mpira ni moja ya mchezo ninaoupenda na kuufutahia.
Linapokuja suala la utani wa jadi wa Simba na Yanga,mimi ni mshabiki wa timu mojawapo.Nadra sana kukosa ktk mechi wanazocheza hawa watani wawili.
Moja ya kitu nilichojifunza toka nianze kuwa nafuatilia mpira,iwe wa ndani ya nchi au nje ya nchi(kwa kutumia mifano ya mashabiki wa hapa Tz).Ushindi wa timu moja dhidi ya nyingine unahusishwa sana na mwanamke.
Yaani unaweza sikia mashabiki wakibishana kabla ya mechi,utasikia "Nyie ni wachumba tu,lazima tuwabambie"...au "Leo lazima muolewe na mtalala bila pichu,hayo ndio masharti ya ndoa"..."Tushawaposa nyie na mahali kala kocha,bado sherehe ya kubeba mwali".Utasikia matusi au maneno mengi na mengine hatuwezi andika hapa,lakini yote yanahusianishwa na timu iliyoshinda kama "Mwanaume" na ile iliyoshindwa kama "mwanamke".Hii nifafanulieni.
Watu huenda mbali na kutengeneza vibonzo vikionyesha taswira ya mwanamke mrembo kuashiria timu iliyofungwa na taswiara ya mwanaume ili timu yenye ushindi.Kifupi,mara nyingi timu iliyofungwa huonekana kama "imeolewa" na timu yenye ushindi kama "iliyooa".
Mbaya zaidi hata wanawake pia wapo ktk mkumbo huu.Unaweza kukuta mke wa mtu yupo timu tofauti na mumewe, timu ya mume ikifungwa utaona anasema "haooo wameolewaa...Hao wamechomekwa".
Sasa hii dhana ya kufananisha timu na wanawake ilianzia wapi?Nini mahusiano ya kufananisha timu iliyofungwa na mwanamke anayegegedwa au aliyeolewa?Hivi hata huko nchi za nje mashabiki hufananisha timu pinzani na wanawake?
Note:Kama mada haina mahusiano na jukwaa hili, Moderator watasaidia kuipeleka jukwaa husika.