Kwanini usalama unapuuzwa kiasi hiki na Serikali ipo?

Kwanini usalama unapuuzwa kiasi hiki na Serikali ipo?

PHALTEND

Member
Joined
Nov 4, 2016
Posts
14
Reaction score
27
Ipo hivi, Mwenzenu katika swala hili nimeangalia clip nyingi zilizorekodiwa na watu mbalimbali na nimeshuhudia kwa macho yangu kuhusiana na mwendokasi wa bus za abiria hasa za mikoani.

Tena baadhi ya miendo, matendo na maamuzi ya madereva wa mabasi hayo yamekuwa yakijirudia.

Sasa unajiuliza;

1. kwann yanajirudia?

2. Kwann Kuna ushabiki kwa jambo hatari la hivyo?

3. Je, Wasimamizi wa haya mambo kweli wako duty?

Nduguzangu, Mimi naona kwa mapendekezo yangu kila awezaye kuiombea dua nchi yetu asiache kufanya hivyo. Maana ukifikiri vizuri vyanzo vya haya yote viko mbali sana.

Mnasemaje wanajamvi, kuna maoni? Au nini kifanyike? Labda kupitia kitakachosemwa na wadau tutakua tumeisaidia jamii kwa namna moja au nyingine.

Karibuni.
 

Attachments

  • ed1ff841da5f9fc4085ab9e8cfc1fdb9.mp4
    556.6 KB
  • ed1ff841da5f9fc4085ab9e8cfc1fdb9.mp4
    556.6 KB
Back
Top Bottom