Kwanini upinzani wetu haukui kama wa nchi nyingine?

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
18,716
28,624
Swali ndio hilo sitaki kulijaza maelezo mengi sana

Kwanini upinzan wetu haupigi hatua kama nchi nyingine mfano Kenya? Mbona uko palepale hausongi, shida ni nini wadau?

Naomba tujadili
 
unataka ukuweje kutoka kupata kura laki sita mpaka kufika kura milion sita.
 
swali ndo hilo sitaki kulijaza maelezo mengi sana

kwanini upinzan wetu haupigi hatua kama nchi nyingine mfano kenya mbona uko pale pale hausongi shida ni nini wadau
Mbele ya kuuawa, kupotezwa, virungu, kufungwa, kuzuiwa mikutano, kusingiziwa dawa za kulevya, risasi, vifo........
 
Hebu kaangalie toka mfumo wa vyama vingi unaanza,weka idadi ya wabunge na kura za urais kila uchaguzi mkuu!
Naamini ukitoka huko utajiona nanga kuanzisha thread bila kujua unachokiongea!
 
Wadhani kuwa upinzani umesimama au umedumaa?? Kaa chini kwanza, Tafuta data sahihi. 1995 hadi leo wapo wabunge wangapi wa upinzani?? Je upinzani umepoteza majimbo mangapi na umenyakua mangapi kutoka ccm??
Weka akilini kwamba, hakuja zaliwa wanachama wapya Tz ila wanachotwa huko huko ccm. Unataka waongezeke shingo ka twiga au??
 
swali ndo hilo sitaki kulijaza maelezo mengi sana

kwanini upinzan wetu haupigi hatua kama nchi nyingine mfano kenya mbona uko pale pale hausongi shida ni nini wadau
Mkuu hatua zipi ambazo huo upinzani haujazipiga??
 
Mwambie jamaa yako asihangaike na upinzani !! Wamemperekea kuzima bunge live, wamemsababishia kupiga marufuku siasa na mikutano ya hadhara, wamemsababishia kutumia dola kupoteza wapinzani wake etc.

WaTz wana akili sana na wanaona kinachoendelea
 
Kwa sababu ya aina ya wananchi kiakili. Hata hivyo upinzani unakua, labda kasi ya ukuaji ndiyo unayoiona hairidhishi.
Ili kupata maendeleo endelevu ni muhimu kuwa na vyama vingi vyenye uwezo wa kupata uongozi wa nchi.
 
Swali ndio hilo sitaki kulijaza maelezo mengi sana
Kwanini upinzan wetu haupigi hatua kama nchi nyingine mfano Kenya? Mbona uko palepale hausongi, shida ni nini wadau?
Naomba tujadili

Kwanza jiulize kwa nini umeitaja Kenya na usizitaje nchi rafiki kama Uganda na Rwanda nchi zinazoongozwa na madikteta uchwara kama hapa kwetu. Nadhani sababu kubwa ni kwamba hapa kwetu kwa ukosefu wa ustaarabu, Katiba kama sheria kuu haiheshimiwi, Rais wetu anaweza kuisigina jinsi anavyojisikia akiamka na ndoto aliyoota. Kasi ya mabashite kuongezeka ni indiketa mojawapo ya wapi tunakoelekea...chini ya Katiba ya porini.
 
Swali ndio hilo sitaki kulijaza maelezo mengi sana

Kwanini upinzan wetu haupigi hatua kama nchi nyingine mfano Kenya? Mbona uko palepale hausongi, shida ni nini wadau?

Naomba tujadili[/QUO
mtu mzima unauliza swali ambalo majibu yake unayo mfukoni...unatakiwa kuijtambua sana
 
Upinzani unakuwa ila kasi ya kukua inahujumiwa kwa matumizi ya risasi na mabomu kudhiti upinzani ambao hawana majeshi.
 
Demokrasia ni tunda la haki na usawa.Je tuna usawa? Je tuna haki? Katika mazingira ya sasa ukuaji hauwezi kuwepo kwa kasi kwani watawala wanaogopa kukuwa kwa upinzani.Mawazo yao ni kutawala milele.Watu wenye mawazo ya kutawala milele wana kasoro ambazo wakiondoka wanaogopa watakaokuja kuzihoji.Matokeo yake wanakuwa wakandamizaji,madikteta uchwara,na ukandamizaji.
 
Tatizo liko kwa wapinzani wenyewe,wabishi,mamangi meza demokrasia wanayoililia hawaitekelezi kwenye vyama vyao utumiaji wa makomandoo na kutembeza kelb kwenye vikao.
LIPUMBA3232.jpg
 
Swali ndio hilo sitaki kulijaza maelezo mengi sana

Kwanini upinzan wetu haupigi hatua kama nchi nyingine mfano Kenya? Mbona uko palepale hausongi, shida ni nini wadau?

Naomba tujadili
Mwambie mwenyekiti wenu basi aachie uhuru wa kisiasa uone kama ccm haitakuwa kama KANU ya kenya.
 
Swali ndio hilo sitaki kulijaza maelezo mengi sana

Kwanini upinzan wetu haupigi hatua kama nchi nyingine mfano Kenya? Mbona uko palepale hausongi, shida ni nini wadau?

Naomba tujadili
according to CHADEMA and UKAWA kwa uraisi walipata over ten million votes! Lubuva and CCM wanasema walishinda for the figure waliyotangaza! according to NGOs tallying results kama si sahihi!

Je jimbo la Ilala, Mbagara, and the like kiuhalali CCM walishinda au walipoka ushindi! kwa kigezo hicho it is most likely CHADEMA and UKAWA inawezekana ndio walishinda ila LUBUVA NA TEAM YAKE WANAJUA WALIFANYA NINI NA MUNGU ANAWAONA ila sidhani kama wanaamini kuwa Mungu yupo! Kwa wakati wake mavuno yataonekana!
 
Back
Top Bottom