Mung Chris
JF-Expert Member
- Sep 12, 2017
- 3,474
- 4,007
Wana jamnvi, ebu tukae tutafakari, Kwanini mtu awe maskini. Kinachoweza kumsaidia mtu kuwa na maisha yake ya kawaida ni uwezo wake wa kufanya kazi, Elimu hata ikiwa ndogo bado anakuwa na uwezo wa kutafuta. Je kuna kitu kingine kinacho muandama mwanadamu na kumkandamiza ili asiwe hata na maisha ya kawaida. Je kitu hicho kinacho muandama kinaweza kuondolewa ili kisiendelee kumdidimiza mwanadamu. Kwa sasa tunao matajiri ambao hata darasa la 7 hawakufika na tunao wasomi walio jitahidi kupata pesa kwa njia zao nao matajiri. Kunani?
Mfumo wa maisha uliopo una kitako, kwenye kitako kuna watu wengi sana ambao ni casual au regular people ambao ni working class.. juu mfumo huo ni mwembamba sana ndo mana una watu wachache kina bahresa na Dewji etcetera.
Sasa inahusiana vipi na mada yetu ya umaskini mkuu?Elimu ya darasani inaua vipawa.
Maisha yanataka ujuzi na sio vyeti
Uko sahihi ,umaskini ni mfumo tu basi .Ubeparini mbaya watu wanapambana wawe juu na Wengine wawe chini.Pengine mifumo ya kibepari inatudidimiza au kutupa wakati mgumu kuwafikia walioajiriwa juu.... Labda mifumo ya kijamaa iliyoboreshwa inaweza kuwaweka watu wote kwenye mizani sawa..
Moja kati ya nguzo moja ya ujamaa kama unakumbuka aliousimamia Nyerere ni KuPUNGUZA UKUBWA WA GEPU LILILOPO KATI YA TAJIRI NA MASKINI. Gepu hili kwemye ubepari huwaga linatanuka kila kukicha mana vitu vinatoka kwa maskini kwemda kwa matajiri.Pengine mifumo ya kibepari inatudidimiza au kutupa wakati mgumu kuwafikia walioajiriwa juu.... Labda mifumo ya kijamaa iliyoboreshwa inaweza kuwaweka watu wote kwenye mizani sawa..
Nonsense,Utajiri ni siri ya mtungi aijuae kata.
Mtaka cha uvunguni sharti ainame, mtu anataka utajiri ila hafanyi mambo ya kumfanya awe tajiri.
Haba na haba hujaza kibaba, watu wanataka utajiri wa haraka wa kafara,upako, na kubet wasijue polepole ndio mwendo na haraka haraka haina baraka.
Usione vyaelea vimeundwa. Pambana, kuwa na subira, work hard work smart, acha tamaa.
Wanataka Utajiri kama wa Chief Godlove.Utajiri ni siri ya mtungi aijuae kata.
Mtaka cha uvunguni sharti ainame, mtu anataka utajiri ila hafanyi mambo ya kumfanya awe tajiri.
Haba na haba hujaza kibaba, watu wanataka utajiri wa haraka wa kafara,upako, na kubet wasijue polepole ndio mwendo na haraka haraka haina baraka.
Usione vyaelea vimeundwa. Pambana, kuwa na subira, work hard work smart, acha tamaa.
Kwa nn kushindwa kuwapa ajira au kuwapeleka ajira za tamisemi?Naamin mfumo wa elimu wetu umeongeza masikini
Huu mfumo wetu kijana anapokosa ajira anakuwa ni kama mlemavu hawez chochote tena hakuna ubunifu wa kutengeneza hela ni wachache sana wanaokuwa na uwezo huoKwa nn kushindwa kuwapa ajira au kuwapeleka ajira za tamisemi?