Kwanini Ulichelewa kufanya Maamuzi?

Mapico

JF-Expert Member
Apr 17, 2019
556
1,270
Habari za weekend Wakuu &wanajamii

Nimeleta kwenu swali hilo tujifikiririshe kidogo

Nakumbuka mambo mengi ambayo mpaka leo najiulizaga
kwa nini nilichelewa kufanya maamuzi mpaka zile fursa zikanipita nakubaki kuwa kumbukukumbu na story tu.

"2009 nilihitimu kidato cha nne wakati huo nafasi za kazi kama JESHI J.W.T.Z POLISI NA UALIMU zilikuwa mtu unaenda kwa kujivuta vuta nataka sitaki.
Mzee wangu alikuwa na kauli Nzuri na watu wa kwenye hizo fani hivyo kuingia huko mambo yalikuwa kama unamsukuma mlevi vile fursa ilipatikana ya mimi kuingia moja kwa moja mpaka JESHINI kwa tiketi ya Baba kanituma . nakumbuka nilizingua aga kutokana na kutaka harakati za kutoka Nje ya nchi kwenda kupiga biashara Mozambique kwa kaka yangu mkubwa ili nije nitoboe mapema.
nililazimishwa nikaambiwa ila moyo ulikuwa mzito kuchukua maamuzi Mpaka ile nafasi akaja kupewa mtu mwingine ambaye ni rafiki wa Familia .
Mwezi uliopita wakati nipo katika kambi moja hapa Dar nikiwa nakaguliwa ikaja Gari flani hivi ya Kijani full tinted ikapita askari wote wakasimama waliokuwa pale getini wakaisalute ile gari sikushangaa sana nikachukulia ni kawaida.
wakanikagaua wakaniruhusu nipite na gari mpaka ndani nakuonyeshwa sehemu ya parking.
nikashuka kwenye gari kuelekea kwenye ofisi zao chakushangaza nafika karibu na eneo flani pameandikwa ........#Assembly point akapita yule jamaa ambaye miaka mingi ilipita bila kuonana naye akiwa na walinzi wawili nyuma wanamu escot.
amechafuka nyota na vyeo kadhaa kwenye suti yake ya kijani
nikavunga kama simjui nimpimie. #uzuri ni mtu asiye na makuu akaja Mpaka nilipokuwa nimesimama akanisalimu kwa Bashasha sana na kunikaribisha Ofisini tukapiga story na kubadilishana Contact nikafanya kilichonipeleka tukaagana nikamaliza harakati zangu mule ndani nikageuka na kuelekea pale Tanzanite Hall Kimara Terminal wakati narudi nilikuwa katika kujilaumu sana kwa kukataa ile fursa ya kuingia jeshini nikajisemea "ningekuwa na nyota zangu za kutosha."
Ila na Mshukuru Mungu maisha yanasonga nasomesha nategemewa na ndugu na familia pia...
niishie hapo kwa leo.
.Maamuzi yako ni Mtaji
 
Umenikumbusha Kaka yangu aliyechezea bahati kama hiyo 2012 kwa madai hapendezwi hata kidogo na kazi ya ualimu.

Kilichomkuta na adha anazoendelea kukutana nazo hadi sasa hivi ni wa kumwonea huruma tele, maana amechakaa sana na kubaki kijiti kwa mawazo ya ugumu wa maisha na kuendelea kuwa tegemezi hadi sasa.

Hakika wahenga walisema "bahati haiji mara mbili".. .
 
Bahati inakujaga mala mbili wakati mwingine..mfano
Mimi nilikataaga nafasi fulani hivi baada ya miaka 5 hivi kupita nilikuja kuipata tena.

Nashukuru mungu.

Watu wengi tunaishi kwa majuto Na Ndio maana atutoki tulipo....Kama kweli una nia ya kutoka ulipo jikubali ulipo....furahia wakati ulio nao then apo ndipo fursa zitaanza kufunguka....ila ukibaki mtu wa kulaumu uwezi fika popote.

Life is like a magnet when you invest your time in negativity...negativity will attract your life.
 
Dah mtu anapotea na elimu yake kichwani vyeti kabatini
 
Bahati inakujaga mala mbili wakati mwingine..mfano
Mimi nilikataaga nafasi fulani hivi baada ya miaka 5 hivi kupita nilikuja kuipata tena.

Nashukuru mungu.
Hongera kwa hilo
 
Watu wengi tunaishi kwa majuto Na Ndio maana atutoki tulipo....Kama kweli una nia ya kutoka ulipo jikubali ulipo....furahia wakati ulio nao then apo ndipo fursa zitaanza kufunguka....ila ukibaki mtu wa kulaumu uwezi fika popote.

Life is like a magnet when you invest your time in negativity...negativity will attract your life.
Fact Mkuu
 
Life is now leave your man. Everybody has his own time zones
54247235_274863333414083_2080486736077369366_n.jpeg
 
Unajuaje kama ungerudi ndani ya maboksi kama wale jamaa 13 waliofariki? Kwani issue ni nyota au kuendeshwa?
 
Back
Top Bottom