Kwanini uliamua kurudi nyumbani?

Kwanini uliamua kurudi nyumbani?

Dagaa Tonge

New Member
Joined
Nov 11, 2021
Posts
3
Reaction score
15
S.Aleykum , Bwana asifiwe.

Tafadhali mada hapo juu yahusika.

Niko America mwaka wa pili huu nimejifunza mengi kwa kweli-

a)Bila kazi hakuna maisha, kazi ndo itakuwezesha kumudu gharama za food, cloth, shelter.

B)Bila Saving hutoboi hata wao wenyewe wanakwambia saving ni kitu cha muhimu sana.

C)Starehe, bila pesa hupati hata demu ile habari ya kupewa utelezi bure haipo so ili angalau upate bao moja itacucost kuanzia 100CAD, mwanamke yoyote unapata ni pesa yako tu. Mexico, Muhindi, Mzungu, Mwafrika yani any pesa yako tu.

D)Gharama za maisha ziko juu hasa rent, yani ni maumivu, pesa yote inaishia huko utasave hela ndogo sana ingawa ukiipeleka kwa Sh ni nyingi ila hapa ni kiduchu sana yani.

E)okay hasa kilichofanya niandike huu ujumbe ni kwamba, kazi nyingi hapa ni za viwanda ni kazi ngumu , kusimama masaa nane mpk kumi na mbili si kazi ndogo sometimes ni night shift si kazi rahisi, naona wafilipino, wachina, wahindi, Ghana, Nigeria, Kenyan wanavopambana ila cha ajabu wengine mpk 60 yrs bado mtu yuko factory nikagundua ukizubaa hapa unazeeka kwenye haya mateso, so mimi nimeamua niwekeze nyumbani nirud after sometimes pesa ya hapa kwa nyumbani unaishi kibosi kabisa lakin hapa hata ukirent eneo hta la kufuga njiwa hupati na maisha yako yote itakupasa kufanya kazi , kumbuka now days hakuna kaz hata hizo za viwanda tena na haya matariff ya trump ndo kabisa unemployment inakuja juu kwa kasi.

F)In conlusion tuambie wewe kwanini uliamua kurud nyumbani? au kwanini utaamua kubaki hapa mpaka uzee wako? Iwe Canada, Uk, US, Australia, au hta EU tiririka hapa watu wapate maarifa.

Nawasilisha.
 
Mm nadhan kila sehemu kuna Ugumu na urahisi wake,
Iwe kijijini, uwe Dar uwe mkoa.
Uwe Marekani au Uingereza.

Huu utofauti wa Ugumu na urahisi unaletwa na hasa ww unafanya nini ili kuingiza Kipato.
Na jinsi gani mazingira uliyopo unavyoweza kujikimu nayo.

Maisha haya, nyoko sana.

Kuna wanao hapo hapo ulipo wanakuja na wanatoboa na kuna wengine hapa hapa bongo wanatoboa na walikukuta mjini.
Dah! Salute
 
Back
Top Bottom