Kwanini Ukonga hawaungi mkono juhudi ?

Kwa hali jinsi ilivyo ni dhahiri CCM imechokwa haswa Dar kiujumla sema tu wazembe kadhaa ndo wanapinga juhudo za maendeleo i.e. Dodoma, Singida,Tabora, Shinyanga, na Mwanza
Bado wanakuimbia chagua kijani mletewe maendeleo, wakati wameshindwa kuziletea maendeleo kambi zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na bado ule ukoo wa shetani watajitahidi pia kuiba kura!
Ee Mola wakifanya hivyo kawaunguze mikono yao
mikono yao na akili zao zikapate ukoma.
Ukawapofue macho yao kamwe wasione tena!
 
Tatizo ni moja tu ambalo upinzani hawajanote wanafanya kampeni vizuri watu wanapiga kura at the end "mwenye nguvu mpishe ndo inatumika"

I swear to god upinzani mnajisumbua" hamtoshinda kupata ubunge wala udiwani

Hapa namaanisha sio kwamba hamshindi ila hakuna tume huru kwa sasa

Yaani mnajisumbua tu!


Bila tume huru mnajisumbua

Sent using Jamii Forums mobile app

Okay, sawa!

Kwa kuwa umetambua tatizo,jitokeze basi uwe sehemu ya utatuzi wake.
 
Hapo ukiuliza wangapi wamejiandikisha kupiga kura unakuta watu 11 tu kati ya hao wanaosapoti CDM, mkishindwa mnaanza tumeibiwaaa..!!! Kila siku mnaibiwa na nyie si muibeeeee..!!:mad::mad:
 
Angalia uzinduzi, utaona mambo ni hayo hayo na umati utakuwa mkubwa hivyo hivyo. Watanzania qanafanya mikutano entertainment, wanahudhuriya kwa wingi sana, siku ya kura robo yao haipatikani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haki ya nani,, uchaguzi ungekuwaga huru siku zote CCM angekuwa kaburini sasa hivi! Tungekuwa tulishamsahau siku nyingi!!
Uchaguzi usingelikuwa huru na haki, mbona hata siku moja hamjaomba mahakama hayo mabox ya kura yaletwe mbele ya jaji myahesabu upya?? Acha tu ushamba
 
Kama picha hizo za Erythro ni za kweli; na watu hao wakajitokeza kupiga kura, CCM wataanzia wapi kupindua ushindi?

Tatizo la CHADEMA na wenzao linaanzia hapa, na siku zote tunawaambia waweke juhudi zao zote katika kuwekeza kwa watu.
Ni jambo moja kuwa na umati mkubwa kwenye mikutano, na likawa jambo jingine watu hao wakajitokeza kupiga kura. Je, mnaouhakika watu hao hujitokeza kupiga kura? Ushahidi upo wapi. Tuonyesheni! Kama hamna ushahidi tutawaamini vipi!

Anzieni kukaza hapo. Tafuteni kila njia ya kuwafanya hao watu wajitokeze kupiga kura. Jiulizeni, kama hawaji kuwapigia kura ni nini kinawazuia, na ziondoeni sababu hizo.

Jambo la pili. Kama kweli watu hao wanajitokeza, na wanawapigia kura nyinyi halafu kura zao hazihesabiwi au zinaibiwa kuna umuhimu wa kulieleza vizuri hili kwa wananchi hao. Kura zao zinapoibiwa au zinakataliwa kwa maksudi tu, sio CHADEMA tu wanaofanyiwa dharau. Kimsingi ni wao, wapiga kura ndio wanaonyimwa haki yao. Sasa jiulize, ni kichaa gani anayeweza kuwafanyia uhuni umati kama ule, hata kama anao polisi wenye washawasha!

Tafuteni njia nzuri za kuwaelewesha wananchi, na wawaamini mnachokisema. Kazi ya kulinda kura zao na kuhakikisha hawadhurumiwi watalisimamia wenyewe. Hakuna NEC wala polisi anayeweza kupora haki ya wananchi waliodhamiria kukataa kuonewa.

Mnaposhindwa nyinyi (CHADEMA) ni hapo pa kuwaongoza wakatae kudhurumiwa. Hili limewashinda kabisa, na mtaendelea kuwa mnalialia tu na kutuonyesha ni jinsi gani mikutano yenu inavyovuta umati wa watu, lakini matokeo ya ushindi hakuna, na wala ushahidi usiopingika hakuna; na hata mahakamani hamtaki kwenda. Inapokuwa hivyo mnawatia watu wasiwasi na kuwaona nyinyi waongo, mnaotafuta njia za mkato tu bila ktia bidii zote zinazohitajika katika mafanikio kwenye siasa. Na inakuwa ngumu zaidi kwenu mnapokutana na watu wenye roho mbaya kama waliopo sasa.
 
Mbona watu wasahaurifu namna hii? Kilichofanyika Kakonko na Kinondoni ndo hicho hicho watakachofanya CCM na DED wao. Unless UKAWA wamepata solution, Waitara atarudishwa mjengoni kwa nguvu ya Dola.
 
Back
Top Bottom