Kwanini UKAWA itashindwa vibaya?


Mwandishi makini huhakikisha anaepuka kutumia vivumishi vyenye utata kwenye maandiko yake. Kama kuna kushindwa "vibaya" ina maana kuna "kushindwa" na kushindwa "vizuri". Usipotolea maelezo maana ya kushindwa vibaya, andiko lako linakosa maana kwa msomaji. Na ukitaka kusema kushindwa vibaya kuna maana gani, lazima ueleze imekubaliwa na nani kwamba kiwango fulani ni "vibaya" na kipi ni "vizuri"...

Kuhusu hilo la kura kuharibika, nimeshanusa mchezo wa bao la mkono kwa style ya kuharibu kura za wapinzani. Hilo itabidi lipigiwe kelele na kufanyiwa kazi...
 
Binafsi na hili sijaficha lawama nyingi zitaenda kwa CHADEMA. Sijui ni genius gani huko aliyeamua kuingia kwenye hili dubwasha la UKAWA limevuruga sana siasa za upinzani. Kushindwa kwao watalaumu wengine wote isipokuwa wao wenyewe. Na kitu ambacho hatutakikubali ni watu hawa hawa ambao wamechukua hatua zitakazosababisha upinzani ushindwe waje tena na kusema waongoze tena harakati za mabadiliko 2020. Hili tumeshalikataa mapema.
 
Kwa mwenendo wa hali ya kisiasa ulivyo, CCM imeshashinda, ila asilimia ya ushindi ndiyo haina uhakika...

Kwa Maelezo yako Utakuwa na Tatizo kubwa la Ushahabiki...
Mtu ashinde halafu % Ndiyo Haijulikani.Daah!!!! Watu wangu wanaangamia kwa Kukosa Maarifa. Eti ni mtoa Mada..
 
Neno au Jina Dubwana Sio l
a Kistaarabu.a Ki
 
Wewe na ubogo wako wa samaki uwe unapeleka habari za kushindwa kwa ccm sio ukawa njinga
 

katika hili ulionya mapema lakin waliziba masikio sasa ni wakati wa kusubiri muda ufike tu
 
kWA WENYE KUFIKIRI WAMESHAELEWA NIA YA UKAWA SIO KULIKOMBOA TAIFA HILI, BALI NI KUINGIA IKULU TU! WAKAFANYE NINI? WANAJUA WENYEWE WAKITAKACHO. CHAGUA CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA :high5:
 
Tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa kitaasisi wa chama cha mapinduzi, ulioruhusu kustawi kwa siasa za kimtandao ambazo ni matokeo ya kuwa na jamii dhaifu ya kitanzania na waliotufikisha hapa ndio sasa tunawataka.
Chalenge kwa magufuli ni namna atakavyowadhibiti wanamtandao waliobaki ndani ya chama cha mapinduzi kama atashinda ingawa sioni akifanikiwa.
Lakini chalenge kwa chadema ni namna watakavyowadhibiti friends ambao kimsingi ni very powerful
kama atashinda. Sioni namna watavyoweza
nani atashinda? Mnajua ninyi ambao bado mna matumaini na wanasiasa wa kitanzania as to me i dont trust them all and am not a voter.
 
Humu kuna watu walikuwa wanaota U-mnikulu ukawatoroka, hivyo sidhani kama wanaweza wakausemea vizuri UKAWA! Tukutane October 25
 

Kupo kushindwa kubaya na kushindwa kuzuri. Kushindwa vibaya ni pale unapokuwa na nyenzo ya kushindia ukaziacha na kuzidharau ukachukua nyenzo nyingine kwa mbwembwe nyingi halafu nyenzo hizo zikakuletea matatizo badala ya mafanikio. Ukawa ilikuwa inaanza kuunda structure fulani ya utawala ndani yake. Structure ile imebomoka yote baada ya wao kukubali kuendeshwa na matukio. Huko ni kushindwa vibaya...
 

Sawa... next time watakuconsult...
 
ccm wanajuwa kabisa kuwa wanakwenda kushindwa uchaguzi wa mwaka huu!
 
Sawa... next time watakuconsult...

ACT wanaonekana kuwa wasikivu zaidi. Wakiendelea hivihivi watakuwa chama kikuu cha upinzani. Chadema wataponzwa na siasa za matukio...
 
ACT wanaonekana kuwa wasikivu zaidi. Wakiendelea hivihivi watakuwa chama kikuu cha upinzani. Chadema wataponzwa na siasa za matukio...

Amka wewe,ACT ipo funded na ccm sio wapinzani,amekuja kugawa kura za wapinzani,mbona mmelala mpaka akili zenu?
 
Amka wewe,ACT ipo funded na ccm sio wapinzani,amekuja kugawa kura za wapinzani,mbona mmelala mpaka akili zenu?

Hebu acha kuongea propaganda za mwenyekiti wenu Mbowe. Hujui kuwa Mbowe na cohorts wake ndiyo wako bize kuchafua yeyote aliyepingana naye! Mtu asipokubaliana nae basi ni msaliti!
 
Amka wewe,ACT ipo funded na ccm sio wapinzani,amekuja kugawa kura za wapinzani,mbona mmelala mpaka akili zenu?

Yaani hapo ulichosema ni kwamba wapinzani wasiaminiwe kwa vile wanatumiwa na CCM. Kauli za namna hii ndio huwa zinawafanya wananchi wasichague vyama vya upinzani. Unadhani unaichafua ACT kumbe unachafua upinzani wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…