Vawulence
JF-Expert Member
- Jan 4, 2009
- 1,930
- 2,118
Kutokana na matokeo ya kidato cha nne yaliyotoka wiki hii, nilishindwa kuelewa imekuwaje wanafunzi wangu ninaowafundisha wakaishia kupata daraja B na C huku hakuna hata mmoja aliyepata daraja A ilihali nilitumia nguvu na maarifa yangu yote kuhakikisha wanafunzi wangu wanafaulu kwa kiwango cha juu kabisa.
Kwa kuwa pamoja na kukosekana kwa daraja A bado shule yangu iko kwenye nafasi nzuri sana kitaifa....nilishawishika kufuatilia matokeo ya shule zingine nikaona hali ni hiyo tu...
Hata wanafunzi kumi bora na shule kumi bora hakuna A hata moja kwenye somo la CIVICS. Nilishindwa kuelewa tatizo liko wapi kwani sio kawaida. Naelewa kuwa wakati wa kusahihisha kuna kitu tunaita "EXTREME"...ila sidhani kana ni kwa nchi nzima inawezekana ikatokea hivyo...
Au ndio kusema walifanya STANDARDISING kupita kiasi?
Anayeelewa tatizo liko wapi tafadhali atuelimishe kidogo...