Kwanini ufanye Biashara ya Mtandao na FLP ?

mushijcob

Senior Member
May 20, 2015
104
69
KWANINI BIASHARA YA MTANDAO? KWANINI UFANYE NA FOREVER LIVING PRODUCTS?

BIASHARA YA MTANDAO NA UMUHIMU WAKE.

Biashara ya mtandao ni mfumo wa kipekee kabisa wa biashara kuwahi kutokea. Kwani unampa mtu fursa ya kuanza biashara kwa mtaji kidogo na huhitaji kuwa na frem, tin namba, leseni na mengine mengi.
Zifuatazo ni faida za biashara hii

1. Mafunzo bora kabisa ya biashara.

Kampuni nyingi zina mfumo mzuri wa mafunzo ambayo yatakusaidia kwenye biashara na hata maisha kwa ujumla. Na kwa kampuni nitakayokuonyesha na kukushauri kuingia kuhusu mafunzo usitie shaka.

2. Kila mtu anataka ufanikiwe.

Tofauti na kwenye biashara za kawaida ambapo wafanyabiashara wenzako wanataka wewe ushindwe ndio wao wafanikiwe, kwenye biashara ya mtandao kila mtu anataka wewe ufanikiwe. Aliyeko juu yako anataka sana wewe ufanikiwe maana na yeye atafanikiwa. Hivyo atakusaidia na kukupa moyo mpaka ufanikiwe. Hakuna biashara yenye uhusiano mzuri hivi duniani.

3. Unaweza kuanza kwa muda wa ziada.

Tofauti na biashara za kawaida, biashara hii unaweza kuianza kwa muda wa ziada, huku ukiendelea na mambo yako mengine, hasa kama umeajiriwa au unasoma. Ni daraja zuri sana la kutoka kwenye ajira na kuingia kwenye biashara.

BIASHARA HII INAMFAA KILA MTU ANAETAKA KUFANIKIWA. NA YUPO TAYARI KUCHUKUA HATUA.

Changamoto za biashara hii.

1. Mtizamo hasi wa jamii.
Hasa hapa kwetu, watu wapo hasi sana na hivyo mtu akisikia unafanya biashara hii wanaanza maneno, mara umachinga, mara freemason na mengine mengi. Yote haya yanatokana na watu kukosa maarifa kuhusu biashara hii. Usikate tamaa ni kawaida mafanikio ya kweli hua yanapingwa na wengi.

2. Kukataliwa.

Unapoingia kwenye biashara hii na kutaka kuikuza, utakutana na watu wengi watakaokuambia HAPANA, unahitaji kujiandaa vyema. Na uwe mtu mwenye subira na kutokata tamaa mapema. Ukweli ni kwamba hakuna kitu chenye mafanikio utaanza watu wote wakubaliane na wewe hvyo ukifahamu hili halitakuumiza wala kukuridisha nyuma.

3. Kukosa maarifa sahihi.

Watu wengi hawana maarifa sahihi juu ya mfumo huu wa biashara hivyo watakukatisha tamaa. Unatakiwa uwe mtu mwenye maamuzi binafsi sio wa kutegemea maoni ya wengine ndio ufanye maamuzi.

FOREVER LIVING PRODUCTS

Forever Living Products ni kampuni ya kimarekani inajihusisha na biashara ya mtandao imeanzishwa mwaka 1978 na kwa sasa imeshaenea zaidi ya nchi 150. Inalima mmea wa aloe vera na kutengeza bidhaa mbalimbali kutokana na mmea huo, bidhaa za nyuki wadogo, virutubisho vitokanayo na mimea na matunda mbalimbali. Ni kampuni kubwa sana inayojitegemea kimapato hivyo kukuhakikishia wewe unaetaka kujiunga nayo kua haiwezi kufa leo au kesho. Kufanikiwa kwenye kampuni hii ni uhakika kama upo tayari kufanya kazi kwa bidi bila kukata tamaa kwa hapa Tanzania ina ofisi zake mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Arusha,Mbeya na Dodoma.

KWA NINI UFANYE HII BIASHARA YA MTANDAO NA FLP?

Mafunzo bora.

Katika kampuni zote za Mtandao hapa Tanzania kampuni ya FLP ndio inayoongoza kwa kutoa mafunzo bora sana kuliko kampuni yeyote. Mafunzo haya yatakuwezesha wewe uweze kua mtu makini na uweze kufanikiwa sehemu mbalimbali za maisha. Inakuwezesha wewe uweze kuzungumza na mtu yeyote haijalishi ni rika gani, haijalishi ana pesa au ni maskini unaweza kuzungumza na yeyote kama tu utaamua kufanya na kmpuni yetu ya FLP. Utaweza kuweka malengo na kuweza kuyatimiza. Kampuni hii ni nzuri sana maana hata kama kuna mambo ulikua hujui kufanya utaweza kuyafanya kuweka malengo kuandika ndoto zako na vitu vingine vingi. Fanya maamuzi sasa.

Bidhaa.

Kampuni ya FLP inatengeneza bidhaa bora kabisa za mmea wa aloe vera na bidhaa za nyuki wadogo. Bidhaa hizi ni bora sana kwa afya yako na familia yako tuna makundi mbalimbali ya bidhaa ambazo zinamgusa kila mtu kama; vinywaji vya afya, virutubisho mbalimbali, Bidhaa za usafi wa mwili, Ngozi, Uzito, Mazoezi, Urembo. Kila mmoja ameguswa na bidhaa za FLP. Kuanzia mtoto, kijana, familia, na wazee. Anza leo ufaidike na bidhaa hizi. Unaweza kuanza biashara hii kama mtumiaji wa bidhaa tu na ukapata faida ya kununua kwa bei ya jumla kwa matumizi yako binafsi na familia yako.

Mpango wa Masoko.

Mpango wa masoko wa kampuni ya FLP ni Mojawapo wa mipango bora ya masoko ya makampuni makubwa sana duniani.
Tunaposema mpango wa masoko tunazungumzia jinsi unavyoweza kulipwa namna unavyotengeneza kipato wewe mwanachama. Tuna aina mbalimbali za vipato kupitia kampuni hii ya FLP kama ifuatavyo:

Kipato cha rejareja

Kipato cha rejareja ni pale unapouza bidhaa zetu. Unaponunua bidhaa kwenye kampuni ya FLP kama mwanachama mpya ukauza kwa bei uliyopewa uuzie unapata faida ya 21.5% kwenye kila bidhaa uliyoiuza. Ukimaliza bidhaa zako na ukanunua tena mara ya pili utaweza kwenda kuziuza kwa faida ya 43% kwa kila bidhaa unayouiuza na kwa makadirio tu kwa wanauza bidhaa wanaweza kuendesha maisha yao vizuri kabisa kwa kutegemea faida ya kuuza bidhaa. Unashauriwa angalau uwe na wateja 20 wanaonunua bidhaa kwako kila mwezi wateja 20 kwa Tanzania nzima ni watu wachache sana ambao hushindwi kuwapata.

Bonasi ya Timu

Kama tunavyosema Mtandao tunazungumzia kujenga timu na hapa kwenye bonus ya timu ndipo kwenye pesa nyingi kwanza unapoleta msambazaji mpya kwenye kampuni ya FLP kwa sasa unaweza kulipwa Tsh 200,000/=. Haiishi hapo kampuni itakua inakupatia wewe uliejenga timu ya watu chini yako bonus ya mauzo yao kila mwezi kwa hiyo kama unataka kupata kipato cha uhakika wekeza muda wako mwingi hapa kwenye kujenga timu baada ya muda utaona matunda yake. Wako wanaotengeza hadi million 6 kwa mwezi kwenye bonus ya timu. Ni wewe kuamua kufanya biashara leo na kampuni hii ya FLP ambayo inajali afya yako na kipato chako pia.

Bonasi ya Gari

Kadiri unavyokuza biashara yako kwa kujenga timu kubwa na kuwasaidia wengine kukua kwa kujenga timu zao mwenye kampuni hakuachi bure anakupatia bonus ya gari na hapa unakua unapokea kipato kwa muda wa miezi 36 mfululizo kwa ajili ya kuweza kununua aina ya gari uitakayo. Ni kwanini usianze leo?

Safari za kimataifa.

Kadiri unavyokuza biashara yako mwenye kampuni anatoa nafasi yaw ewe kusafiri na yule umpendae kwa mwaka mara mbili kwenda sehemu za kipekee sana duniani na unalipiwa kil kitu ikiwepo ticketi ya ndege, malazi, chakula, na pesa ya matumizi. Ni wewe kufanya kazi kwa bidi uweze kunufaika na bonus hizi. Kiukweli hata kama una biashara yako sio rahisi uchukue faida ukatembee nje ya nchi hivi hivi labda biashara yako iwe imekua kubwa sana na hiyo itakuchukua zaidi ya miaka 20. Je upo tayari kusubiri miaka 20 ndio uanze kuasafiri? Chukua hatua leo.

Bonus ya mwenyekiti

Kampuni hii ni ya kipekee sana inakuwezesha wewe kupata kile unachokitaka duniani. Mwenye kampuni vilevile anaangalia umefanya nini mwaka mzima katika faida ya kampuni iliyopatikana 60% anairudisha kwako na anakupatia wewe msambazaji wake kama zawadi wako wanaopokea pesa za kitanzania zaidi ya 100 milioni kila mwaka. Ni wewe kuanza sasa usiache fursa hii ya kipekee.

Zipo faida nyingi sana unazipata katika kampuni yetu ya FLP ni wewe kuanza leo kufanyia kazi ndoto zako kupitia kampuni hii ya forever anza leo upate kutimiza ndoto zako leo.
Kianzio ni kidogo sana unahitajika uwe na Mtaji wa Tsh. 1,020,000/= au nusu yake Tsh. 510,000/= tu, kama una mtaji kuanzia Tsh 300,000 na unataka kujikwamua tutakusaidia ili uweze kufikia malengo yako.
Tafadhali usisite kututafuta kupitia no zifuatazo (Whatsapp 0654726668) na 0755192418 tupo kwa ajili ya kukuwezesha kutimiza ndoto zako.
b3ae31f20e59f1be9f025d9be3342ed0.jpg
 
Biashara za aina hii (network marketing) zimeongelewa sana humu jamvini, na sijui kwa nini mod hakuinganisha hii.

Kifupi kwa nchi masikini, biashara hii huwanufaisha wenye nacho na kuwafanya wasionacho kuwa maskini zaidi, kwa sababu zifuatazo:

1) Lazima kuwepo na bidhaa inayouzika.
2) Wawepo wateja wenye uwezo wa kuinunua.
3) Huyo mfanya biashara mlengwa awe na uwezo wa kununua hiyo bidhaa.
4) Huyo mfanya biashara awe na wateja wa kutosha wa kuwauzia. Kitendawili ni pale ambapo mteja anakuwa pia muuzaji (network).

Kutokana na hayo hapo juu, ni mtu mwenye alichonacho anaweza biashara hii, la mlengwa anabaki kudoda na bidhaa aliyoinunua kwa fedha zake (kama kiingilio). Akifanikiwa kuuza ni kwa wateja wa hali kana yake.

Nawajua vijana wengi wakiomaliza vyuo vikuu wakihangaika kushawishi kuuza hizo bidhaa za Forever Living (ambazo ni ghali) bila mafanikio.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
fact nmeshindwa kuielewa kabisa hii biashara mteja anakuwa muuzaji sasa utamuuzia nani?
 
Biashara yenu ya forever haiwezi kufanikiwa Tanzania. Bidhaa zenu no ghali kuliko being ya solo. Na hakuna manufaa yoyote ya kiafya MTU anayapata kwa kuogea sabuni ya 14000 na kuacha ya 2000. Kupiga mswaki na dawa ya 13000 kuacha ya 2000. Uwezekano wa kukua kwa bashara ni ngumu maana hamna wateja. Soko la uhakika lla bidhaa zenu hakuna. Muwe mnawaambia wanqchama wenu kabla ya kujiungaa.
 
Kama umechagua kua maskini kaa kmya. Mbona hamjudge magari ya ghali yanayoletwa Tz nani atayanunua?
 
Biashara yenu ya forever haiwezi kufanikiwa Tanzania. Bidhaa zenu no ghali kuliko being ya solo. Na hakuna manufaa yoyote ya kiafya MTU anayapata kwa kuogea sabuni ya 14000 na kuacha ya 2000. Kupiga mswaki na dawa ya 13000 kuacha ya 2000. Uwezekano wa kukua kwa bashara ni ngumu maana hamna wateja. Soko la uhakika lla bidhaa zenu hakuna. Muwe mnawaambia wanqchama wenu kabla ya kujiungaa.
Wako wanaoweza kununua panua akili yako utawaona. Kila kitu ni mtazamo tu. Badili mtazamo wako kila kitu kinawezekana.
 
Wako wa Tanzania wanaotumia laki kwa siku kwenye kula tu!! Kama umechagua kua maskini na kushindwa kununua kitu usitake na wengine waungane na ww. Kiti kua ghali suluhisho sio kuacha kununua suluhisho ni kuongeza mkondo wako wa kipato ili uweze kumudu gharama.
 
Hao wanaoweza kununua wako wachache. Walio wengi hawana uwezo huo. Kwa sababu bidhaa zenu hazina thamani ya Pesa MTU anayonunulia. Bidhaa ya alovera haina tofauti na bidhaa nyingine zilizo katika soko. Ugumu ndo unakuja hapo
 
Unaelewa vizuri ubora wa bidhaa zetu?? Unaelewaje wakati hujazitumia. Umejuaje wapo wachache wanaoweza kununua ?
 
fact nmeshindwa kuielewa kabisa hii biashara mteja anakuwa muuzaji sasa utamuuzia nani?

Mfano anaanza mwanajamvi mmoja kuwa muuzaji. Ananiuzia mimi na wewe "Disposal". Mimi na wewe tunapata wanajamvi wawili kila moja, hapo network ya yule aliyetuingiza inakua. Tuliowaingiza pia hivyo hivyo. Mwishowe hakuna mteja katika wanajamvi. Aliyeanza ananufaika na juhudi za wanamtandao wake. Wale wa mwisho inabidi watoke nje ya wanajamvi, kama hao nao hawajafikiwa.

HATA VILE LA MSINGI BIDHAA HIZO ZIPENDWE NA ZINUNULIWE.

Bidhaa za Forever Living ni za kudumisha afya na zina ubora wake kasoro tu ni wachache wana uwezo wa kumudu bei zake. .Mathalani bei ya dawa ya meno 'Aloe Vera Tooth Gel" ni maradufu ya dawa za meno zenye ubora sawa. Mleta mada awaambie bei ya hizo FLP.

Bahati mbaya walengwa wa kufanya biashara hii ni wasiokuwa na mtaji, wakishawishiwa kwamba watatajirika haraka mara tu wakijiunga na mtandao huo!!!

Anayeshawishi ni nani, ni yule aliyeshawishika, akakopa hela, akanunua hizo bidhaa, akushawishi mgawane huo umaskini. Hahahaaaa.
 
Biashara yenu ya forever haiwezi kufanikiwa Tanzania. Bidhaa zenu no ghali kuliko being ya solo. Na hakuna manufaa yoyote ya kiafya MTU anayapata kwa kuogea sabuni ya 14000 na kuacha ya 2000. Kupiga mswaki na dawa ya 13000 kuacha ya 2000. Uwezekano wa kukua kwa bashara ni ngumu maana hamna wateja. Soko la uhakika lla bidhaa zenu hakuna. Muwe mnawaambia wanqchama wenu kabla ya kujiungaa.
Ni kweli mkuu! Binafsi nilinunuaga dawa za meno....mara tatu sikuona jipya! Tangu hapo nikaacha nikarudi zangu kwenye Sensodyne
 
Biashara za aina hii (network marketing) zimeongelewa sana humu jamvini, na sijui kwa nini mod hakuinganisha hii.

Kifupi kwa nchi masikini, biashara hii huwanufaisha wenye nacho na kuwafanya wasionacho kuwa maskini zaidi, kwa sababu zifuatazo:

1) Lazima kuwepo na bidhaa inayouzika.
2) Wawepo wateja wenye uwezo wa kuinunua.
3) Huyo mfanya biashara mlengwa awe na uwezo wa kununua hiyo bidhaa.
4) Huyo mfanya biashara awe na wateja wa kutosha wa kuwauzia. Kitendawili ni pale ambapo mteja anakuwa pia muuzaji (network).

Kutokana na hayo hapo juu, ni mtu mwenye alichonacho anaweza biashara hii, la mlengwa anabaki kudoda na bidhaa aliyoinunua kwa fedha zake (kama kiingilio). Akifanikiwa kuuza ni kwa wateja wa hali kana yake.

Nawajua vijana wengi wakiomaliza vyuo vikuu wakihangaika kushawishi kuuza hizo bidhaa za Forever Living (ambazo ni ghali) bila mafanikio.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Hii ni kweli tupu.

Kifupi ukiwa na FLP unakuwa ni machinga na bora hata machinga anauwezo wa kupanda na kushusha. Wenyewe bidhaa zao ziko fixed, ghali na soko ni shida!

Mbaya zaidi unatakiwa kuwatafuta member wapya...wat a business kha!

Kuna watu waliingia kichwa kichwa baada ya kusikia shuhuda mbili tatu za walioacha kazi na kununua magari...wakaishia kutumia bidhaaa wenyewe na kupata hasara baada ya kukosa wateja.

#ZaMBAYUWAYUchanganyanaZAKO#
 
hii biashara ilikuwa inamaliza boom la wanafunzi vyuoni, maana walikuwa wanaoongopewa wanaingia kichwakichwa!! alafu hao wanaouza hizo bidhaa huwa hawa-edit maneno ,yaan wote utasikia nilikuwa meneja wa benki nikaacha, Mara nilikuwa menejea tra nikaacha kazi. yaan waongowaongo tuu, alafu ukikataa bidhaa zao ni wakalii hao!!
 
Back
Top Bottom