Kwanini Tz haimo kwenye nchi ambazo paypal inazitumia

Smile ltd

Member
Joined
Dec 7, 2013
Posts
20
Reaction score
2
Nina biashara yangu nimeanzisha ebay lakini nimesikitika sana baada ya wateja wangu walioko ulimwengun kote kulalamika kuwa hawawezi kunitumia pesa kupitia paypal na ebay wakaweza kunipatia pesa hizo.

Nilipoangalia kwenye orodha ya nchi ambazo paypal inafanya kazi ya kutuma na kupokea pesa Tz haimo ila wenzetu Kenya wamo na wanafanya biashara miaka mingi kupitia mitandao. Tangu walikua wanapeleka vifurushi sasa wanapeleka cargo

Washauri tusaidieni mimi mpaka sasa nimebaki na deni kubwa ebay ambalo kila mwezi ninatakiwa nilipe.
 
Paypal kwa tanzania unaweza kutuma tu na si kupokea hela, simply coz bank haijaruhusu hilo.. Once again wabongo wako nyuma hata online marketing mizinguo, balaa hili... afu kuwapondea majirani zetu daily...
 
kwanza hatustahili kuwaponda majirani zetu ambao wameiacha Tz nyuma sana.

Na kwanini mabenki yasichukue hatua na serikal ikaingilia kati?

Serikali inakosa pesa nyingi sana ambazo kodi tunastahili kulipia tukituma mizigo.
 
kwa sababu Tanzania ni ka nchi ka ajabu sana hapa duniani.
 
Nina biashara yangu nimeanzisha ebay lakini nimesikitika sana baada ya wateja wangu walioko ulimwengun kote kulalamika kuwa hawawezi kunitumia pesa kupitia paypal na ebay wakaweza kunipatia pesa hizo.

Nilipoangalia kwenye orodha ya nchi ambazo paypal inafanya kazi ya kutuma na kupokea pesa Tz haimo ila wenzetu Kenya wamo na wanafanya biashara miaka mingi kupitia mitandao. Tangu walikua wanapeleka vifurushi sasa wanapeleka cargo

Washauri tusaidieni mimi mpaka sasa nimebaki na deni kubwa ebay ambalo kila mwezi ninatakiwa nilipe.

Tatizo ni sera zetu za kifedha haziendani na standards za kimataifa. Black money ndio tatizo. Wanaoruhusu na kuzuia ni paypal wenyewe.
 
Kwaiyo nisaidie nifanyeje? Na nimesajili duka ebay naweza kupata wapi malipo ili niendelee.
 
Fungua akaunti miongoni mwa nchi zilizo katika orodha kama Kenya. Kama una access na nchi za Magharibi, basi tumia nchi hizo.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kwani huwezi pokea pesa kwa western union?.

Yaani westunion kwa wazungu ni usumbufu sana wao wamezoeya saiv wanunue bidhaa wako kitandani na inatoka Tz anapelekewa kwake

Mara nying westunion wanaitumia wachina
 
Back
Top Bottom