Kwanini tusifanye Hitma ya waliopotea ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,643
218,099
Naomba wacha Mungu mnisaidie kama nitakuwa nimekosea , maana mimi si mjuzi sana wa MISA ZA WAFU .

Ni muda mrefu sasa familia za wahanga wanaopotea ama kupotezwa nchini Tanzania zinateseka sana kutokana na utata wa waliko ndugu zao , japo maelfu ya viroba vyenye miili ya binadamu ikiripotiwa kuokotwa hapa au pale kwenye bahari ya hindi , haijawahi kutajwa wanakotokea .

Wasiwasi wangu ni kwamba wanaokotwa ndio waliopotea , " ukimkosa kuku wako bandani lakini ukaona manyoya karibu na banda basi ujue kuku wako kaliwa "

Mimi napendekeza kwamba NI BORA IFANYIKE HITIMA AMA IBADA YA MAZISHI YA WOTE WALIOPOTEA ILI KUWATUA MZIGO NDUGU ZAO WANAOLIA KILA SIKU BILA hata dalili ya kupata ndugu zao , ambao jeshi la polisi limekiri kutokufahamu waliko , ikiwa kama baada ya hitma pakatokea wa kujitokeza basi bila shaka Tutaitana tena ili kumfutia ibada ya mazishi yule atakayeonekana .

Naomba kuwasilisha .

Nakala kwa Mshana Jr .
 
Kwa mila za kabila letu mtu akipotea kwa siku 40 ni lazima kuweke msiba na kisha kuanua matanga siku ya tatu.....

Sasa hawa ndugu zetu wamepotea zaidi ya miaka 2 je junawatu kweli huko?
 
Back
Top Bottom