Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Hivi karibuni Rais Magufuli alizuru TBC, akatoa maagizo chombo hicho kitoe fursa sawa kwa vyama vya siasa vyote. Nimesikiliza taarifa ya habari ya TBC, saa 2 usiku wa leo Juni 5. Hakuna lolote kuhusu kifo cha Mzee Ndesamburo lililotangazwa. Kwanini tusiamini TBC wamempuuza Rais. Ubaguzi unaaanza kulitafuna Taifa letu. Tuupinge kwa nguvu zote
=====================
Maoni ya Mdau Mwingine
=====================
=====================
Maoni ya Mdau Mwingine
=====================
Heshima kwenu wakuu,
Hawa TBC, rais Magufuli amejaribu kuwabeba lakini hawabebeki. Wamejaa dharau na Kiburi. Rais ni Taasisi, hata Kama Magufuli kama Magufuli hamumuheshimu, basi heshimuni cheo chake na taasisi ya rais.
Tunajua Mkitumbuliwa kunakuwa na madhara kwa jamii hasa familia na watoto, lakini katika kusimamia maadili lazima tuwatumbue bila hivyo nchi haiendi. Watanzania tulikuwa tumefika pabaya ambacho kila mtu alikuwa anafanya anachotaka.
Watu wanalalamika. Hivi karibuni Rais Magufuli alizuru TBC, akatoa maagizo chombo hicho kitoe fursa sawa kwa vyama vya siasa vyote. Nimesikiliza taarifa ya habari ya TBC, saa 2 usiku wa leo Juni 5. Hakuna lolote kuhusu kifo cha Mzee Ndesamburo lililotangazwa.
Kwanini tusiamini TBC wamempuuza Rais. Ubaguzi unaaanza kulitafuna Taifa letu.
Tuupinge kwa nguvu zote hasa hawa wanaomchanganisha rais na Wananchi