Kwanini tunauziwa mitungi ya gesi full?

Kwanini tunauziwa mitungi ya gesi full?

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,104
Reaction score
1,924
Wajuzi wa masuala ya gesi,kwanini gesi haiuzwi kwa ujazo tofauti kama mafuta ya petrol? Kwani ni lazima ununue mtungi full? nini madhara ya kuuza gesi kwa ujazo tofautitofauti?
 
wajuzi wa maswala ya gesi,kwanini gesi haiuzwi kwa lita kama mafuta ya petrol? Kwani ni lazima ununue mtungi full? nini madhara ya kuuza gesi kwa lita?

Hakuna madhara, kilichopo tuna upungufu wa maeneo ya kujaza gesi.

Umeelewa Chief?
 
Naomba tu husije kusema kwa nn hatununui mchele kwa lita?,nataninia mkuu.soma post namba tatu mkuu
 
Petroli ni kimiminika ndiyo maana hupimwa kwa lita...

Gesi ipo kwenye mfumo wa hewa, ndiyo maana hupimwa kwa ujazo...

Cc: mahondaw
 
wajuzi wa maswala ya gesi,kwanini gesi haiuzwi kwa lita kama mafuta ya petrol? Kwani ni lazima ununue mtungi full? nini madhara ya kuuza gesi kwa lita?
New member!
Sijui ni nani aliekuonyesha JF na kukufundisha kuitumia.
 
mnaweza kunilekebisha kwa kutumia ''lita''-ila nadhani mmenielewa namaanisha nn!!
 
wajuzi wa maswala ya gesi,kwanini gesi haiuzwi kwa lita kama mafuta ya petrol? Kwani ni lazima ununue mtungi full? nini madhara ya kuuza gesi kwa lita?

Ipo siku utataka uuziwe oxygen kwa Lita ukatumie chumbani kwako
 
  • Thanks
Reactions: isk
Nilitaka kuandika kitu ila nimekosa maneno ya kiswahili, kuchanganya kiingereza na kiswahili haipendezi
 
mnaweza kunilekebisha kwa kutumia ''lita''-ila nadhani mmenielewa namaanisha nn!!
Hilo unalolitaka litawezekana tu kama hiyo mitambo ya kujazia gesi itakuwapo kwenye vituo vyetu vya mafuta a.k.a shell,, kwa sasa hivi vituo vya kujazia gesi viko vichache mno.
 
Jibu linaloweza kuwa sahihi kabisa limetolewa katika post namba 3.

Gesi(kama tulivozoea kuiita, kitaalam inaitwa liquified petrolum gas au LPG) inapokuwa imehifadhiwa kwenye mtungi huwa inakuwa imegandamizwa (compressed ) kwenye pressure kubwa hivo inakuwa katika hali ya kimiminika ila pale inapotoka kwenye mtungi ndio pressure yake inapungua na kuwa vapor hadi pale inapochomwa kwenye jiko kutoa nishati inayotumika kupikia. Hivo kadri inapozidi kutumiwa ndipo inavozidi kupungua kwenye mtungi na pressure inazidi kupungua hadi inapoisha.

Kwa hyo kilichopo ni upungufu wa vituo vya kujaza gesi kwenye mitungi.
 
Petroli ni kimiminika ndiyo maana hupimwa kwa lita...

Gesi ipo kwenye mfumo wa hewa, ndiyo maana hupimwa kwa ujazo...

Cc: mahondaw
[emoji2] [emoji2] [emoji2] inaonekana ulikuwa unafeli sana shule mkuu,

Mbona umejibu tofauti na swali?

Mtoa mada anahitaji kujua kwanini isiwe tunaenda kujaza gesi ujazo tunaotaka sisi na sio fixed kama sasa.
 
Ujazo wa gesi hupimwa kwa kilo na si kwa lita
Kilo ni kipimo cha uziti si ujazo. Neno kilo maana yake ni 1000. Kwa hiyo inaweza kuwa kilogram, kilolita, nk. Ujazo unapimwa katika kyubic za mita au lita, kama nimekosea wataalam mtanirekebisha
 
Wajuzi wa masuala ya gesi,kwanini gesi haiuzwi kwa ujazo tofauti kama mafuta ya petrol? Kwani ni lazima ununue mtungi full? nini madhara ya kuuza gesi kwa ujazo tofautitofauti?
Bora ungeuliza kama mitungi ya 0.5kg, 1kg, 2kg na kuendelea kama ipo.
 
Back
Top Bottom