Kwanini tunashindwa kufanya tunayoyataka?

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,529
3,431
Leo natamani sana kuzungumzia uhalisia uliopo kati ya matamanio na utendaji halisi wa kila siku.Nieleweke wazi ninapotoa maelezo haya na Mimi ni binadamu ninaendelea kujifunza na silengi kumkosoa mtu yeyote yule zaidi ya kuonesha hali inayotuzunguka.

Leo sayansi na teknolojia inatuwezesha kujua mambo mengi sana lakini tunajisahau kwa kiasi kikubwa sana kufuatilia juu ya maisha yetu wenyewe kama binadamu.

Mwili wa binadamu umejawa na kumbukumbu nyingi mno ambazo kwa kiasi kikubwa zinaathiri utendaji wetu kwa kujua au kutokujua.Karibu lila kitu kinachofanyika katika maisha ya watu huhifadhiwa kama kumbukumbu.
Akili,mwili,hisia na nguvu za uhai wa binadamu yeyote yule huhifadhi kumbukumbu nyingi mno jambo ambalo ndilo hufanya mtu kuwa na tafsiri yake juu ya chochote anachokiona katika ulimwengu.Baadhi ya wanafalsafa huita ulimwengu wa mtu.Sihitaji sana kuzungumzia falsafa ila ninataka kujenga hoja yangu kwenye uhalisia wa maisha.

Nieleweke kuwa ninachokielezea hapa hakifungamani na imani yoyote ile ila kinatoa picha ya maisha kama tunayoyaona katika utendaji wetu wa kila siku.

Gereza kubwa la binadamu ni kumbukumbu zilizohifadhiwa ndani ya miili yetu.Mathalani leo kuna vyakula,mahusiano,utendaji na masuala mengine mengi ambayo tunayafanya kwa sababu ya kumbukumbu zilizohifadhiwa ndani ya miili yetu.

Kwa mfano macho yetu yametawaliwa na kumbukumbu jambo ambalo hata kile tunachokiona kinapata tafsiri yake kutokana na kumbukumbu tulizo nazo.Ukitaka kujiridhisha juu ya hili embu angalia mfano huu "Unapokiwa kwenye halaiki kubwa ya watu halafu inatokea umeona mtu mmoja ambaye ulishawahi kuonekana naye siku nyingi unaweza ukahisi anaonekana vizuri kwenye kundi kubwa la watu unaowaona kuliko watu wengine na unaweza ukajikuta unavutiwa kuangalia alipo mara kadhaa,hii inatokana na kumbukumbu ulizo nazo.

Hatuoni vitu kama vilivyo katika uhalisia wake kwa sababu miili yetu imetunza kumbukumbu ambazo inataka izione zikijirudia mara kwa mara na inapotokea tunaona tofauti na kumbukumbu zetu tunaweza tukaona tunachokiona siyo kizuri kwa sababu tupo ndani ya mipaka ya kumbukumbu.

Suala la kumbukumbu siyo kwa binadamu tu ila ni kwa kila kitu mfano mbegu ya embe na mbegu ya papai ukizipanda kwenye ardhi ileile kwenye kuota mbegu ya embe haiwezi hupoteza kumbukumbu za embe na kuota kama papai halikadhalika papai haiwezi kugeuka na kuwa embe.Hii inaonesha kumbukumbu zipo katika namna ambayo siyo rahisi kupoteza zinachokikumbuka.

Unaweza ukawa umesahau kabisa Babu wa Babu wa Babu yako alikuwa namna gani lakini pua yako ikawa inafanana kabisa na pua yake.

Tunatawaliwa sana na kumbukumbu zetu kiasi ambacho kumbukumbu hizi zimegeuka na kuwa kama uhalisia wetu leo hii jambo ambalo siyo sahihi.
Leo tunaona vitu vinavyoakosi mwanga lakini hatuoni vinavyopitisha mwanga na cha ajabu zaidi hata mwanga wenyewe ni kama hatuuoni kutokana na gereza la kumbukumbu.

Ili tuweze kuona vitu katika uhalisia wake kuna haja ya kuamsha mawanda mengine ya kuona yasiyotawaliwa na kumbukumbu,hisia, akili na kani za uhai "we need to evolve other dimension of viewing reality". Nje ya hapo ni kukubaiana na kuanudu ule msemo "HISTORIA INAHUKUMU".
 
Kwamba unaweaza utatoaje simu iliyopasuka screen na kutumia kwenye daladala utaonekanaje,wakati kiuhalisia watu wako busy sana vichwani wanatazama lakini hawaoni na kutafakari wanavyoviangalia.
 
Bila kumbukumbu huwezi kufanya kitu. We act from memories whether from active learning or instinctive learning.
 
Back
Top Bottom