Kwanini tunasherehekea siku ya kuzaliwa?

vidmate

JF-Expert Member
May 7, 2018
687
1,205
Habarini za saa wandugu?? Natumai wote huko mliko ni wazima mkiparangana na changamoto za maisha ktk nyanja tofauti... Ila mara moja moja msisahau kujipongeza kwa juhudi zenu hata kama hujafanikiwa ila kuna kitu utakuwa umejifunza.

Bila kuwachosha miaka kadhaa iliyopita tarehe kama ya leo 8/5 nilizaliwa chini ya utawala wa mzee wetu ruksa ila kwa kweli hadi sasa sijaona thamani ya kutumia gharama ama muda kusherekea siku ya kuzaliwa, toka asbh nipo na mishe zangu ni siku ambayo sitaki hata watu waijue kuepusha ushawishi wao hata Fb inabidi niji deactivate kwa muda, maana sielewi kwa kweli

Ila kwa wengi ni tofauti naweza kushiriki za wengine ila kimoyo moyo nabaki kushangaa na maswali mengi. Utakuta mtu mfano girlfriend anakutaarifu miezi kadhaa nyuma na anataka umchangie sherehe, mwaka jana girlfriend alinimaind kisa sikujihusisha na birthday yake japo tulikuwa mbali mikoa tofauti

Hivyo wakuu hii birthday nini hasa furaha yake na mimi wakati mwingine niipate?? Ama ni kigezo ili tu watu mjumuike na kuenjoy, Kwann watu mnasherekea ilihali hujui kwann unaishi ama hata kama unajua haujatimiza?

Lengo langu si kumshambulia mtu yeyote ama kuwakosoa ila nawaza kwa sauti
 
Kumbe tpo wengi? Cjawahi sherehekea hii ktu hata cku moja na mara huwa nakuja shtuka tarehe ishapita ktambo!
 
Hatuna Utamaduni Wa kusheherekea birthday kwa watz Ila Sasa ndio tunaigaiga kwa mbaaaali! Na ndio maana unajisahau Ila Wenyewe wenye Utamaduni wao wanafutilia kwei kwei
Nalog off
 
Habari za muda huu wana jf???

Je kuna haja Kusherekea siku yako ya kuzaliwa???

Kwa upande ''WANGU'' sioni 'umuhimu' kabisa wa kusherekea siku yangu ya kuzaliwa tokana na sababu zifuatazo

1:EVERY DAY IT'S MY BIRTHDAY
Kila siku ni siku yangu ya kuzaliwa sababu kila siku nazidi kuongezeka umri na kukisogelea kifo(sijui kama naeleweka)

2:MFANANO
Sidhani kama itaweza kufanana siku ambayo itawiana na siku nilizaliwa.mfano nilizaliwa tare 29/2 siku ya ijumaa.Hapo miaka mingine nakosa.
Itakua tare 29/2 ila siku haiwezi kuwa ijuma.

3:TAFRIJA
Unaandaliwa sherehe ambayo sion mantiki yake.
Watakuandalia keki na soda ambazo kiafya sioni faida yake (zaidi ya kuongeza sumu

''Muda+gharama
 
Mimi huwa ikifika tarehe na mwezi kama zile nilizozaliwa huwa naingia mahala kufanya maombi ya kumshukuru Mungu kwa kunipa mwaka mwingine.

Wengi wanaofanya party ni kutokana na kuiga tu tamaduni za watu na kuzoea hivyo.

Mfano, kununua na kukata keki, kumwagiwa maji n.k

Hatahivyo, sio vibaya na uzuri zaidi ni kuwa hakuna anayelazimishwa kusherehekea hivyo.
 
Ni kumbu kumbu ya siku yako ya kuzaliwa ukiamua kusherehehea ni sawa na usipo fanya hivyo sio dhambi pia....

Ata kwenye dini huwa kuna kumbu kumbu za matukio fulani kama vile kuzaliwa kwa Manabii n.k. na watu huwa wanasherehekea....

Mataifa huwa yana siku zake za kumbu kumbu kama Uhuru day, Muungano n.k na huwa sherehe zinafanyika.....
 
Hollywood Mentalities.

Ni dhana ambayo imewateka wasomi, wachumi, wanasiasa, wasanii & wakesha hoi barani Afrika na kuwaganda vichwani kama yule mzee aliyempanda mgongoni Sindbad katika ngano za kale na kukataa kushuka.

Humu pia huo ugonjwa umo. Tarehe ya kuzaliwa ya kazi gani?. Logic au mfumo sahihi wa kufikiri ni kufahamu umri--siyo tarehe ya kuzaliwa ya kiumbe chochote hai. Hilo la Tarehe ni suala binafsi, kutafuta ujiko (wishing's) ziso--na mantiki no orodha inaendelea...

Birthday parties Ni tabia inayotokana na utamaduni wa kuiga mifumo ya kitamaduni, sheria, utawala, na demokrasia ya nchi nyingine huku tukidharau uwezo wetu wa kuunda mifumo yetu binafsi ya Maisha.

Ni kuhasiwa kisaikolojia. Zaidi sana ingefana kama sherehe/hafla hizo angefanyiwa Mzazi Mama & Baba kama shukrani kutokana na Malezi bora, upendo na Elimu iso--tokana na u-ingi wa vyeti feki na siyo kumfanyia mtoto mchanga asiye--na upeo ang'avu wowote ule.

I stand to be corrected..
 
Unachanganya mambo hapa!!.. kuna vitu viwili hapo kutumia gharama na muda mwingi katika kusherehekea birthday na kuikumbuka siku muhimu ya kuzaliwa kwako!!.. kuikumbuka siku muhimu ya wewe kuja duniani kuna kosa gani? Kumshukuru mungu na wazazi wako na kukumbuka tu ujio na kwanini umeletwa hapa duniani kuna kosa gani!!.. kwa mfano siku ya birthday yako ukakaa tu nyumbani na family yako na ukafurahi au kufanya ibada kuna ubaya gani? Au ukaamua kuwatembelea wazazi wako na kufurahi nao kuna ubaya gani?.. ndugu hii ni siku muhimu sana na katika maisha yako ikumbuke na kama unao uwezo na nafasi fanya kitu kwa mungu wako na wazazi wako kwa kuwa wao ndio sababu ya uwepo wako... suala.la gharama na mbwembwe za watu wapuuzi katika kusherehekea birthdays isiwe sababu ya kuidharau siku ambayo wewe ulikuja hapa duniani...kumbukumbu ya kuzaliwa na kufariki ni muhimu ktk kumshukuru muumba na kumuomba awasamehe makosa waliotangulia.. ndio maana tuna hizi Xmas, maulid na sijui pasaka etc etc
 
Duh kk unachanganya mafaili hadi hbr za kuomba wafu, ila kuna umuhimu gani mbona hao uliowataja hawajawahi kusherekea siku ya kuzaliwa mfano Yesu
 
Duh kk unachanganya mafaili hadi hbr za kuomba wafu, ila kuna umuhimu gani mbona hao uliowataja hawajawahi kusherekea siku ya kuzaliwa mfano Yesu

Nilidhani umenielewa!!.. just wasted my time!!... simple minded!
 
Duh kk unachanganya mafaili hadi hbr za kuomba wafu, ila kuna umuhimu gani mbona hao uliowataja hawajawahi kusherekea siku ya kuzaliwa mfano Yesu
Kila mtu na mtazamo wake.Uyo Yesu inawezekana haukua mtazamo wake kwasababu kila mtu anaishi atakavyo.
 
Mambo yakukumbuka siku yakuzaliwa ni mambo ya kawaida katika jamii zetu na kila mtu anaikumbuka kulingana na mtazamo wake kwasababu sio lazima wala muhimu ila inapendeza ukiikumbuka kwa namna moja au nyingine.Mim ilikua inanifanya nimpende nakua karibu sana na marehem mama yangu.Kwaiyo ni mojawapo ya siku mtu kukaa na ndugu jamaa na marafiki nakushare upendo.Kwaiyo kama mama zetu wanakumbuka siku walizotuleta duniani inapendeza pia nasisi tulioletwa tukakumbuka japo sio lazima sana.
 
Huwa sijushughulishi na tarehe niliozaliwa. Huwa siikumbuki na uzuri hata yf nae huwa hakumbuki!

Mi huwa naona wazazi ndio walipaswa kusherehekea siku mtoto alipozaliwa!
 
Haina maana. Naona kama unafurahia kuisha kwa umri wako. Maana uliona wapi MTU akipoteza fedha akafanya sherehe? Ila anapoteza umri anafurahia hiyo akili matope!!!
 
Back
Top Bottom