Kwanini tunapandisha viwango vya ufaulu kuingia chuo kikuu wakati tuna idadi ndogo ya wasomi?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
SWALI

Ni kwanini tunapandisha viwango vya ufaulu kuingia chuo kikuu huku bado tuna idadi ndogo ya wahitimu wa shahada mbali mbali kulinganisha na nchi zote kubwa Afrika Mashariki? Inamaana Kenya,Uganda na Rwanda tutashindana nao vipi kwenye ushirikiano wetu huu?
 
Hao waliopandisha wenyewe hakutumia hivo viwango na wengi elimu zao a Kununua sana Pia huwa hawafanyi Research za Uhakika
 
Swali.... Hivi wamepandisha au wamerudisha vya zamani..?
 
Hao waliopandisha wenyewe hakutumia hivo viwango na wengi elimu zao a Kununua sana Pia huwa hawafanyi Research za Uhakika
Hats idadi yenyewe ya wahitimu wa angalao shahada ya kwanza imeongezeka kuanzia 2007-2017 baada ya kuongeze kwa vyuo vikuu nchini ambao wengi wao walikua na ufaulu angalau 2Es, Ambazo hizo 2Es za kwetu huku Ukienda nchi yeyote Afrika Mashariki na duniani unasoma chuo kikuu.Tatizo siasa ineshika hatamu.
 
SWALI

Ni kwanini tunapandisha viwango vya ufaulu kuingia chuo kikuu huku bado tuna idadi ndogo ya wahitimu wa shahada mbali mbali kulinganisha na nchi zote kubwa Afrika Mashariki? Inamaana Kenya,Uganda na Rwanda tutashindana nao vipi kwenye ushirikiano wetu huu?
Je, nchi zote kubwa za Afrika Mashariki ziliwezaje kupata wahitimu wengi wa shahada!? ...ni kweli nao walishusha viwango vya ufaulu kupaa wahitimu hawa!?
 
Hats idadi yenyewe ya wahitimu wa angalao shahada ya kwanza imeongezeka kuanzia 2007-2017 baada ya kuongeze kwa vyuo vikuu nchini ambao wengi wao walikua na ufaulu angalau 2Es, Ambazo hizo 2Es za kwetu huku Ukienda nchi yeyote Afrika Mashariki na duniani unasoma chuo kikuu.Tatizo siasa ineshika hatamu.
Badala watatue matatizo ya Ya waalimu na Suala la Technology katika ufundishaji Tanzania weee
 
Alikudanganya nani? Uliza viwango vya elimu vya nchi hizo kwa rank ya kimataifa wametuacha kiasi gani?
Kuachwa isiwe sababu ya sisi kuachia elimu yetu iendeshwe kiholela.
Ubora wa elimu ndio jambo la msingi kuzingatia na sio bora elimu.
Elimu kwa wote ipo kuanzia kidato cha nne kushuka chini, ndio maana elimu hiyo ni bure.
Tusipende konakona ni vyema tukawaasa vijana wetu hasa darasa la 1-Olevel wasome kwa bidii.
Na sisi wazazi wajibu wetu ni kuhakikisha mahitaji ya msingi yanatolewa kwa vijana wetu ili wapate hamasa ya kusoma na kujifunza kila iitwapo leo.
Ni Natumaini yangu/yetu kuwa elimu yetu itapaa iwapo kila mzazi/mlezi atatimiza wajibu wake.
 
Serikali haitaki wasomi wengi kukisha kuwa na wasomi wengi watamdanganya nani sasa wakati wasomi mtapinga wajinga ndio wanatikiwa zaidi.wacha tuisome namba
 
Education at any level is an industry. Inahitaji input, process and output. Hivyo basi kama input ikiwa ni vil**a hata kama process (wakufunz) itakuwa imetoka mbinguni output itakuwa vil..a + makapi. Hivyo basi tukubaliane na watawala wetu kwamba, chuoni tuweke input nzuri na safi ili ikutane na process bora kutoa output ya kushindana si east Africa tu hata globally.
 
Hao waliopandisha wenyewe hakutumia hivo viwango na wengi elimu zao a Kununua sana Pia huwa hawafanyi Research za Uhakika
Achana nao hao wakurupukaji walifuta advanced diploma ili tuendane na wenzetu wa EA sasa wamekuja na hili sijui tunaendana na nchi ipi? Vyuo vya kueleweka huko Duniani hawaingii kwa hizo points walizoweka na bado wako mbali kielimu zaid yetu
 
Hapa ni sawa na wewe kupewa ngazi ya kupanda mahali ukifika juu unatoa ile ngazi unawatupia wenzio kamba wapande
 
Achana nao hao wakurupukaji walifuta advanced diploma ili tuendane na wenzetu wa EA sasa wamekuja na hili sijui tunaendana na nchi ipi? Vyuo vya kueleweka huko Duniani hawaingii kwa hizo points walizoweka na bado wako mbali kielimu zaid yetu
Waboreshe Kwanza huko Primary na Secondary mpaka Leo waalimu kutwa Kulalamika Mazigira ya Kazi na Zana za Kufundishia Kitabu Kimoja wanafunzi 5 Dawati 1 wankaa 4 kama lile Tangazo la HakiElimu
 
Kwa hili naunga mkono serikali
.Tanzania inahitaji zaidi mafundi kuliko kwenye madegree ambayo hayaleti tija. Tuimarishe vyuo Vykati zaidi kuliko vyuo vikuu. Una
 
Tunataka Quality na sio
Quantity... Ni bora tuwe na Quantity ndogo yenye Quality kubwa kuliko kuwa na Quantity kubwa yenye Quality ndogo
 
Back
Top Bottom