Kwanini tunalihukumu darasa la saba

kaswalala

Member
Mar 13, 2013
42
8
Habari ndugu yangu unaepitia post hii, mimi ni kijana mtanzania mwenye elimu ya chuo (stashahada) pia natarajia kumaliza shahada mwakani mungu akipenda.

Leo naomba tutafakali kwa pamoja kuhusu umuhimu wa darasa la saba katika soko la ajira. ndugu zangu sote tunatambua kuwa daima mtu baada ya kupata elimu fulani huwa anaenda kutafuta ajira au kujiajiri kupitia ile elimu yake ili ajipatie kipato, kwa bahati mbaya mfumo wa elimu wa nchi yetu haumuandai kijana kwenda kujiajili baada ya kumaliza masomo yake na ndio maana vijana wengi hivi leo huwa wanawaza kuajiriwa baada ya kumaliza masomo. sasa suala la kuajiliwa kuanzaia form four na kuendelea inawezekana kama utakuwa na sifa nyingine kama udereva, mafunzo ya ulinzi n.k. Swali langu la msingi linaanzia hapa, vipi kuhusu hawa watanzania wanaoishia darasa la saba ambao hawana hata ujuzi wa kuweza kujiajili na kama wanao lipo tatizo la rasilimali, kukweli kundi la wahitimu wa darasa la saba ambao wameshindwa kuendelea na masomo ya secondary wakaamua kwenda VETA kujipatia ujuzi wa kiufundi au hata kushindwa kwenda huko kutokana na ukosefu wa kipato kwa sasa limetupwa, halithaminiki tena.

Nasema hivyo kwa sababu waajiri binafsi na serikali kwa ujumla hawana tena sera ya kulikomboa kundi hili, wameshabaguliwa kwenye ajira sasa hivi kila ajira inayotangazwa utasikia uwe na cheti cha kidato cha nne, hata zile za ulinzi wa taifa hawawataki.

Kitakwimu kundi hili ni kubwa sana kuliko makundi mengine ya ngazi za elimu. inasikitisha hata ajira za udereva, ulinzi, eti wanataka kuanzia kidato cha nne huu ni uonevu na ukatili mkubwa, kama darasa la saba hawalitaki basi elimu ya lazima iwe kidato ch anne.

kwa uchungu mkubwa namalizia kwa kusema kuwa watawala mmejisahau na hamataki tena kufikili juu ya watanzania, mmeingia kwenye jumuiya ya Afrika mashariki huku mmewagandamiza watanzania hawa, sasa kama ninyi hamuwatambui kwenye soko la ajira, je hao wenzetu watawatambua?

"WATANZANIA TUAMKE VINGINEVYO TUTALIA UMASIKINI KILA SIKU"
 
Mkuu, inasikitisha sana kuona ubaguzi huu wa kielimu ukiwa umeshika kasi huku hakuna juhudi zozote za makusudi zinazochukuliwa na watawala wetu ili kuondokana na hali hii.
 
baadhi yao wamo humu,watakujibu tu,subili wamalize kikao cha mchana.
 
kama kuna mwakilishi yeyote wa wananchi kule bungeni ninaomba achukue tafakali hii na kuijengea hoja binafsi awafikishie waheshimiwa wamejisahau, vinginevyo masikini tutaendelea kuwa vibaraka wa matajiri milele kwa kuwa wao ndio wanaosmeshana saint marry, cambrige international,green acres na nyinginezo za maada kibao wakimaliza degree ulaya wakirudi wameshaandaliwa ukuu wa wilaya, mara wakurugenzi mara wabunge mara mawaziri sisi tuko palepale da! inasikitisha sana wadau.

" UKITAKA KUWATALAWA WATU KWA URAHISI WAPE UMASIKINI"
 
Back
Top Bottom