Kwanini tumpuuze Dr. Slaa na Mwakyembe?

Kwanini tumpuuze Dr. Slaa na Mwakyembe?

cilla

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2011
Posts
372
Reaction score
299
KWA NINI HOTUBA YA DR SLAA NA INAWAFANYA WATU KUWA NA HASIRA NA KUENDELEA KUMUUNGA MKONO EDWARD LOWASA?
Mwenye akili anapaswa kutafakari hili,Na mwenye ufahamu hawezi kupinga ,Lakini niseme wazi kuwa slaa alikuwa na haki yake kisheria kuzungumza alichozungumza,
I. Tafakari yangu ni kwamba Dr slaa anadai kuwa anaushahidi ambao ni akiba hakuwahi kuutoa wote anasubiri Lowasa ajibu ndipo auweke wazi.Hili si jambo la kwanza kuna wakati aliwahi kutamka kuwa kunaushahidi zaidi na mengine mengi ambayo tume ya mwakyembe iliona si vyema kuyaweka wazi kuogopa nchi inge gawanyika.Kwa miaka nane sasa bado hajaweza kuuweka wazi je hili lina tufundisha nini?

II. Dr Mwakyembe naye ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge kuchunguza Richmond anadai kuwa anaushahidi wa Lowasa kuhusika na ufisadi wa Richmond ambao haukuwekwa wazi katika taarifa yao kwa bunge juu ya wahusika wa Richmond.Lakini huyo huyo Mwakyembe katika kuhitimisha taarifa juu ya Richmond bungeni alitamka waziwazi kuwa waziri mkuu Edward lowasa haonekani kuhusika na Richmond moja kwa moja ila ajipime mwenyewe kama waziri mkuu kama anafaa kuendelea au awjibike kwa hicho kilichotokea.

III. Watanzania wanaona kama wanayumbishwa kwakuwa na hamu yakutaka kujua ukweli lakini ukweli huo unadaiwa kuwekwa kiporo kiasi cha kuchoka kusikia mtu akishutumiwa juu ya Richmond na wanaojiita wa kweli wa mambo hayo wakiendelea kulalia ushahidi huu wanaodai wameuweka kiporo
.
IV. Spika wa zamani Bwana Sita naye anadai anaushahidi anahitaji mdahalo na Lowasa ili aweke wazi kila kitu,Je huu si unafiki?

Kwanini ushahidi huo haukuwekwa wazi bungeni na katika taarifa yao kwa bunge?Wote hao walikuwepo Bungeni kwanini walificha baadhi ya sehemu yenye ushahidi huo je wao nao hawajahusika kwakuficha ukweli huo?

Hii inaonyesha sasa kuwa DR slaa,Sita na Mwakyembe wanacheza naakili za watanzania.Ninachokiona mbele hizo mahakama za Ufisadi zitaanza kwanza na hawa jamaa kwasababu walidanganya Bunge na kuficha ukweli kwa Watanzania.
Wauweke huo ukweli wazi waache kutuchanganya watanzania kwa kusema ushahidi wanao lakini hawauweki wazi.

Tuache unafiki watanzania tunahitaji kujua ukweli wote kwasababu ninachokiona mimi ni kwamba kama kweli kuna ushahidi wasinge uficha kipindi hiki ambacho ccm inatafuta kuvipoteza kabisa vyama hivi vya Ukawa kwa nyukilya na si kwa risasi.
Kwa ufahamu nilionao najiuliza hivi Kweli lowasa angekuwa amehusika na ufisadi huo angethubutu kutoka CCM?kwasababu anaakili na alijua akitoka atatafutiwa ubaya wowote kumdhohofisha ili tu CCM kubaki salama.

Kisaikolojia mtu mwizi hujihami na kujifence haraka anapojua anashutumiwa katika suala ambalo amehusika,lakini sioni hilo kwa Lowasa.

Wapo wanaochukulia kujiuzuru kwake kama sababu yakumuhusisha na wizi huo,Lakini Rais Mwinyi kabla ya kuwa Rais amewahi kujiuzulu kwa kosa la askari kuua raia kwakosa ambalo halikuwa lake ila aliwajibika kama kiongozi.Kwanini Lowasa?
Watanzania bado hawajawaelewa hawa jamaa vizuri watuambie vizuri na kujibu maswali yetu.Vinginevyo tutawapuuza na wanajiondolea heshima na kuaminiwa kwao katika jamii ya kitanzania
.

BADO SIONI HATIA KWA LOWASA.
 
Mkuu watu wanaficha ushahidi wa kumtia hatiani huyu wanayemwita fisadi Lowasa ili kuogopa serikali isianguke au nchi kuigawanyika wakati huo huo wakipinga Lowasa asipewe nchi.
Yaani ni unafiki,unafiki,unafiki
 
leo wacha na mimi niseme.
CCM wa leo wanampongeza Dr. Slaa kwa Misimamo isiyoyumbishwa. Karibu bwana Lizaboni unisaidie katika hili maana ndo imekuwa kauli mbiu ya chama tawala kwa sasa.

Hivi ni sahihi kusema kuwa misimamo ya Dr. kwa tangu akiwa CDM mpaka sasa ambako amestaafu bado haiyumbi yaani imesimama haswa? maana inanijia akilini msimamo mmoja wa Dr kuwa kuna mtoto wa raisi flani amekamatwa china, anayebisha ampeleke mahakamani. hivi huu msimamo pia bado hauyumbi ndani ya kauli mbio ya wazee wa chama? maana hali ya sasa imekuwa imekuwa ni ya undumilakuwili mno nchini
 
Last edited by a moderator:

Watu wanamsikiliza Dr.Slaa na uongo wake, keshadanganya mara ngapi humu jamvini na kwenye jamii?

1: alishawahi kusema kuna contena la karatasi za kura pale Tunduma na watu waliishia mpaka kuvunja contena na kulikuwa hakuna kitu

2: Alishawahi kusema Kikwete na Masha na timu yao wako laCairo hotel wanapanga mikakati, wakati JK wala hakuwa Tanzania kipindi hicho,

wakina Ritz, VUTA-NKUVUTE na timu yao ya CCM walimponda Slaa kuwa ni muongo, cha ajabu leo wote wana muona anaongea kweli
 
Last edited by a moderator:
Hawana maana kabisa hao miaka yote hii nane walikuwa wapi na huo ushahidi wao,hao niwa kuwapuuza
 
Yaani sasa single yoyote itakayoandaliwa kuwachafua ukawa itabuma hata hajatoka studio
 
1.kwa sababu MWAKYEMBE alisema bungeni nchi itaanguka ikiwa ataeleza yote ya richmond
2 SLAA alitufundisha kwa miaka kadhaa tuuchukie ufisadi
3.lowassa kasema richmond si yake bali ni aliye juu
4.aliye juu hakumchukulia lowassa hatua kumfikisha mahakaman kwa ufisadi sasa tunaamin lowassa ni kafara
NOTE:HIZI HOJA NNE ZINATAFSIRIKA KWA PAMOJA
 
Watanzania tuamke tuikomboe Tanzania yetu kutoka mkoloni CCM
 
hakuna wa kumzuia Lowassa 2015. so far ratio kwenye watu 10 utapata 7 kwa 3.
 
Mkuu watu wanaficha ushahidi wa kumtia hatiani huyu wanayemwita fisadi Lowasa ili kuogopa serikali isianguke au nchi kuigawanyika wakati huo huo wakipinga Lowasa asipewe nchi.
Yaani ni unafiki,unafiki,unafiki
Kwa kauli ya huyo huyo Mwakyembe alipokuwa akihitimisha hotuba yake kwa Bunge akiwa ni Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kushughulikia sakata la Richmond alinukuliwa akisema kuwa kama kamati yake ingeamua kuanika wazi kila ilichokiona wakati wa uchunguzi wao kungekuwa na uwezekano serikali hiyo ya CCM ingeweza kuanguka wakati huo.

Ni vyema sasa Mwakyembe atujulishe ni kitu gani ambacho alikificha kukiongea ili serikali ya CCM isianguke?

Hata hivyo jibu la swali hilo tunaweza kulipata kutokana na kauli ya Lowassa ambayo alieleza kuwa mamlaka ya juu ndiyo mhusika mkuu wa mkataba huo wa Richmond, na tokea Lowassa atamke kauli hiyo nzito hatujawahi kusikia kauli yoyote kutoka mamlaka ya juu kukanusha madai hayo na wakati huo huo vyombo vya dola hatujaviona vikimchukulia hatua Lowassa kwa 'kusingizia' mamlaka ya juu kutokana na sakata hilo la Richmond.

Hivi katika mazingira hayo inawezekanaje kwa Umma wa watanzania hususani la kundi la maccm kuendelea kumbebesha Lowassa msalaba wa Richmond ?!
 
Watu wanamsikiliza Dr.Slaa na uongo wake, keshadanganya mara ngapi humu jamvini na kwenye jamii?

1: alishawahi kusema kuna contena la karatasi za kura pale Tunduma na watu waliishia mpaka kuvunja contena na kulikuwa hakuna kitu

2: Alishawahi kusema Kikwete na Masha na timu yao wako laCairo hotel wanapanga mikakati, wakati JK wala hakuwa Tanzania kipindi hicho,

wakina Ritz, VUTA-NKUVUTE na timu yao ya CCM walimponda Slaa kuwa ni muongo, cha ajabu leo wote wana muona anaongea kweli

Ukiona adui yako au mpinzani wako anakusifia,jiangalie,kuna mahali umekosea.
 
Last edited by a moderator:
leo wacha na mimi niseme.
CCM wa leo wanampongeza Dr. Slaa kwa Misimamo isiyoyumbishwa. Karibu bwana Lizaboni unisaidie katika hili maana ndo imekuwa kauli mbiu ya chama tawala kwa sasa.

Hivi ni sahihi kusema kuwa misimamo ya Dr. kwa tangu akiwa CDM mpaka sasa ambako amestaafu bado haiyumbi yaani imesimama haswa? maana inanijia akilini msimamo mmoja wa Dr kuwa kuna mtoto wa raisi flani amekamatwa china, anayebisha ampeleke mahakamani. hivi huu msimamo pia bado hauyumbi ndani ya kauli mbio ya wazee wa chama? maana hali ya sasa imekuwa imekuwa ni ya undumilakuwili mno nchini

Yes, aite press conference afafanue juu ya kashifa zingine alizowahi kuzikomalia ili jamii imuamini vinginevyo atuache tuamini kuwa kuna kinachomsukuma kubwabwaja juu ya jambo ambalo hata bunge lilishatolea adhabu. Unacheza na njaa ya pesa wewe? mzee wa watu anatumika mpaka inatia huruma
 
Watu wanamsikiliza Dr.Slaa na uongo wake, keshadanganya mara ngapi humu jamvini na kwenye jamii?

1: alishawahi kusema kuna contena la karatasi za kura pale Tunduma na watu waliishia mpaka kuvunja contena na kulikuwa hakuna kitu

2: Alishawahi kusema Kikwete na Masha na timu yao wako laCairo hotel wanapanga mikakati, wakati JK wala hakuwa Tanzania kipindi hicho,

wakina Ritz, VUTA-NKUVUTE na timu yao ya CCM walimponda Slaa kuwa ni muongo, cha ajabu leo wote wana muona anaongea kweli

Kama ambavyo machadema yalimtaja na kumtangaza lowasa kuwa ni fisadi na ni no tisa ktk list of shame. Leo ni habuba wenu
 
Last edited by a moderator:
Watu wanamsikiliza Dr.Slaa na uongo wake, keshadanganya mara ngapi humu jamvini na kwenye jamii?

1: alishawahi kusema kuna contena la karatasi za kura pale Tunduma na watu waliishia mpaka kuvunja contena na kulikuwa hakuna kitu

2: Alishawahi kusema Kikwete na Masha na timu yao wako laCairo hotel wanapanga mikakati, wakati JK wala hakuwa Tanzania kipindi hicho,

wakina Ritz, VUTA-NKUVUTE na timu yao ya CCM walimponda Slaa kuwa ni muongo, cha ajabu leo wote wana muona anaongea kweli
Mbona nyie mmempokea mtu alie kuwa anaongoza ccm kwa kuwapiga vita. Hivi mpaka leo hujaelewa mabomu ya arusha nani muhusika mkuu?
 
Last edited by a moderator:
Slaa amepoteza mvuto, heshima aliyojijengea kwa miaka zaidi ya 15 imeyeyuka kama mshumaa....

Watanzania wamemdharau sanaa kwa kumshambulia mtu mmoja wakati list ya ufisadi alizokuwa anazikomalia zipo nyingi...mie kwakweli alivyomaliza kuongea nikajisema nae huyu kapewa kitu mweee!
 
Mwakyembe na slaa wapuuzwe tuh!

1:lowasa kama waziri hana kinga ya kushitakiwa kikatiba mpaka sasa haja shitakiwa kuna nini hapo? 2:mbona muda mrefu umepita hivi richmond ni ya leo ,au sheria haina meno juu ya lowasa 3:wamesema wanaushahidi kwanini dr.slaa asiwe mlaramikaji mwakyembe akawa shahidi wake waka mpeleka lowasa kisutu?
4:kwanini wamseme lowasa tu! Hao wengine vipi ? Au wao watakatifu?
5:hivi hao watu na elimu zao watueleze watanzania mahakama ni vyombo vya habari? 6:mbona escrow ya juzi hawasemi ? Na kati ya hao wawali nani mtakatifu hadi waaminiwe kiasi hicho?
#% watanzania tujitume tusiwe wavivu hata wa kufikiri %# tubadiri shina halina matunda maana walopata uhuru ni viongozi na si raia .lowaaaaasaaaaaaaaaaa
 
Watu wanamsikiliza Dr.Slaa na uongo wake, keshadanganya mara ngapi humu jamvini na kwenye jamii?

1: alishawahi kusema kuna contena la karatasi za kura pale Tunduma na watu waliishia mpaka kuvunja contena na kulikuwa hakuna kitu

2: Alishawahi kusema Kikwete na Masha na timu yao wako laCairo hotel wanapanga mikakati, wakati JK wala hakuwa Tanzania kipindi hicho,

wakina Ritz, VUTA-NKUVUTE na timu yao ya CCM walimponda Slaa kuwa ni muongo, cha ajabu leo wote wana muona anaongea kweli

Lini nimemponda Dr. Slaa Mkuu?

Mzee Tupatupa
 
leo wacha na mimi niseme.
CCM wa leo wanampongeza Dr. Slaa kwa Misimamo isiyoyumbishwa. Karibu bwana Lizaboni unisaidie katika hili maana ndo imekuwa kauli mbiu ya chama tawala kwa sasa.

Hivi ni sahihi kusema kuwa misimamo ya Dr. kwa tangu akiwa CDM mpaka sasa ambako amestaafu bado haiyumbi yaani imesimama haswa? maana inanijia akilini msimamo mmoja wa Dr kuwa kuna mtoto wa raisi flani amekamatwa china, anayebisha ampeleke mahakamani. hivi huu msimamo pia bado hauyumbi ndani ya kauli mbio ya wazee wa chama? maana hali ya sasa imekuwa imekuwa ni ya undumilakuwili mno nchini

mkuu lizaboni akikujibu hapa kama unavyotana. NAJIHUZURU JF
 
Last edited by a moderator:
Inanisuta kwa lipi? Dr. Mihogo katikisa nini kama mlivyodhani? Poleni sana, kila mbinu yenu inakataliwa na wananchi.

usitishiwe na lumumba hawana jipya lazima sindano iwaingie
 
Back
Top Bottom