Kwanini TCRA na Jeshi la Polisi wasiweke utaratibu maalum wa namna watu wanavyoweza kuuziana vifaa vya mawasiliano pasipo kuhusishwa na uhalifu?

Huo utaratibu wako wa kuja na shikamoo utakuja kuamkia hata watoto wa shule ya msingi,unakuja humu unasema wakubwa zangu shikamoo kumbe wewe ndio mzee kuliko wote humu JF
Kwa kijana mdogo kama mimi kusema shikamoo kwa wakubwa zangu ndio desturi yetu sisi watanzania. Ndio tabia njema tuliyofundishwa tangu tukiwa wadogo
 
kitu kinachoweza kukuokoa ni risiti sasa wewe huna risiti watu watakuamini vipi.
Mtu ananunua simu kutoka kwa mtoto wa shangazi yake (binamu) sasa receipt huyo binamu atapata wapi? Angekuwa ananunua kutoka katika duka la simu sawa ingekuwa ni rahisi kwa mtu kudai receipt
 
Kuhusu swala la kutunza risiti waafrika wengi huwa hatuzingatii vitu kama hivi tunapuuzia.Mimi hapa mpaka leo nina risiti za simu niliyonunua 2009
Kuna baadhi ya watu ni wazuri sana katika kutunza receipt ila baadae nyumba inaungua na vitu vyote vya ndani pamoja na hiyo receipt.

Kumbuka pia receipt za EFD hupauka haraka sana.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya thanks to God the Almighty.

TCRA na Polisi waweke utaratibu maalum wa namna watu wanaweza kuuziana vifaa vya mawasiliano pasipo kuhusishwa na uhalifu.

Unakuta kwa mfano Athumani ananunua simu kutoka kwa Alexander alafu baada ya mwezi mmoja Athumani anakuwa tracked na wataalam wa TCRA pamoja na Police kisha anakamatwa nyumbani kwake Mbagala kwa kosa la kukutwa na mali ya wizi.

Unaweza kukuta si Athumani wala Alexander ambao ni wezi, ila kwa kuwa umekosekana utaratibu mzuri wa kufanya transactions za secondhand communication devices, unakuta baadhi ya watu wanaingia katika mkenge wa kujihusisha na uhalifu pasipo kujijua.

Unakuta huyo Alexander alinunua simu mwaka 2017 miaka miwili iliyopita jambo ambalo kwa hali ya kawaida ya kibinadamu na maisha yetu ya kiafrika ni ngumu mtu kutunza receipt ya manunuzi, hivyo na yeye pia ilimlazima auze simu ile pasipo kukabidhi original receipt.

Kwanini sisi watanzania tunashindwa kujiwekea utaratibu mziri wa maisha yetu mpaka tusubiri wazungu waanze na sisi ndio tuige?

Mbona TRA wanao utaratibu mzuri sana wa kufanya motor vehicle transfer kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine ilhali wamiliki wa magari na wachache sana ukilinganisha na wamiliki wa simu za kiganjani?

OUR MOTTO: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

View attachment 1215944

OMBI LANGU: NSSF NIPENI PESA ZANGU NINAZOWADAI NYIE WATU. NAONA MNATAKA KUNIUA KWA MSONGO WA MAWAZO HUKU MTAANI
Mkuu unakujaga na mawazo mazuri sana, ila pale tu unaponidai hapo huwa nawaza umetumwa na be beberu au ni akili zako? Maana haiwezekani unidai kitu ambacho sina hata mia mfukoni na ndio maana nafukuzana na wale niliowapiga ndani kwa mizunguko ninayoijua mimi ili nipate japo kidogo, unanikera sana hivi wewe ni mtanzania kweli au nikuhoji kwanza???

Alisikika mlevi kwenye mlima mmoja akiangalia twiga alioletewa toka Longido
 
mada nzuri ila again tunalaumu tulikoangukia sio tulikojikwaa,jibu la mada hii lielekezwe kwa waziri wetu wa mambo ya ndani,lini atatoa IDs kwa watanzania zinazoongea kwenye systems ya nchi nzima?maana nikikuuzia simu ni lazima nikupe na copy ya ID book yangu yenye ID number,na huu ni ushahidi tosha na ukiwa na wasiwasi wa ID mnakwenda police station yeyote mkahakiki ukweli,kinyume cha hapo ni maisha ndani ya shit hole country
 
Yapo mambo hata wao TCRA bado yanawatatiza hasa kuhusu vifaa vya mawasiliano ya kielectronik, hawa jamaa tumesha fanya vikao nao si chini ya vinne kama sikosei, bado kuna suala la IMEI hili bado ni mtihani kwao sababu watu wanazifyatua vibaya mno, mfano mdogo ni huu apa.

Umenunua samsung j4, kwa mtu na receipt anazo lets say kainunulia Dubai, alipofika hapa ikawa inasoma not registered on network, anaipeleka kwa fund inawekwa baseband ingine, hapo anaanza kuitumia lakini tayar IMEI namba zikiwa ni tofauti, anaitumia mpaka anaiuza, anamuuzia mtu mwingine, inaenda huko inamsumbua, anaipeleka kwa fundi simu, na yeye anafanya yake kama kuchange imei ana Kurepair, anaifanyia Patch certificate, inakubali, ktk IMEI zingine, yaani unakuta ktk kujalibu jaribu simu hii moja ishajaribiwa na imei zaid ya tano, mpaka anapata mtandao anarudi hewan, fundi anachojali kaz imeisha hajui ile imei kama ipo moja tuu, ama ipo tracked ama vyovyote vile, mtumiaji anakamatwa na IMEI ya s6 wakati simu ni J4 ukifika kule unakuwa na kesi tatu, ya kwanza wizi wa J4, ya pili S6 ambayo simu yako inasoma imei yakevna ya tatu ni kubadili imei. Hujui unatokaje ktk kes kama hii, na jamaa now days watakuambia mwenye simu hii aliibiwa na vitu vingine ana kunavmtu aliuaawa ktk tukio hilo ama vyovyote vile..ni mtihani. Lakini upo utaratibu wa kuandikishiana unapokuwa unahitaji kununua kifaa cha mawasiliano kutoka kwa mtu mwingine..hili suala bado ni gumu sana..ni unstoppable
 
ukiishaona jambo lolote limehusisha polisi tz,basi jua hapo hakuna kazi ni uhuni mtupu.

taasisi nyingi tz hazina weredi katika utendaji,ila polisi tz ndio mwalimu,wengine wote wana aibu kidogo.

imagine mteja A anaripoti upotevu wa simu,polisi anapokea ripoti na gharama ya ufuatiliaji kisha ufuatiliaji unaanzia tcra,mlalamikiwa B anashikwa na polisi kwa kukutwa na simu iliyopotezwa na A.B anaambiwa A ndio mmliliki halari wa hii simu na anazo docs zote,ili upone weka ushawishi nikamalize kesi.B akieleweka,'A anafuatwa na kuambiwa simu haijapatikana.

simu ya 1mil,inampatia polisi ulaji wa laki 7.na mhanga haipati.dunia ni uwanja wa fujo.
 
ukiishaona jambo lolote limehusisha polisi tz,basi jua hapo hakuna kazi ni uhuni mtupu.

taasisi nyingi tz hazina weredi katika utendaji,ila polisi tz ndio mwalimu,wengine wote wana aibu kidogo.

imagine mteja A anaripoti upotevu wa simu,polisi anapokea ripoti na gharama ya ufuatiliaji kisha ufuatiliaji unaanzia tcra,mlalamikiwa B anashikwa na polisi kwa kukutwa na simu iliyopotezwa na A.B anaambiwa A ndio mmliliki halari wa hii simu na anazo docs zote,ili upone weka ushawishi nikamalize kesi.B akieleweka,'A anafuatwa na kuambiwa simu haijapatikana.

simu ya 1mil,inampatia polisi ulaji wa laki 7.na mhanga haipati.dunia ni uwanja wa fujo.
Kwa kifupi wewe nimekuelewa zaidi
 
Usiwatwishe watu majukumu yasiyo na mashiko mshikwe tu kama unajua kuna maswala hayo ya kuingia matatani why hutumii akili unakurupuka kibwege kununua vitu bila utaratibu,mnalalamika tu sio watu walio jela wana hatia saa nyingine ni uzembe kama huu,kitu kinachoweza kukuokoa ni risiti sasa wewe huna risiti watu watakuamini vipi.Kuhusu swala la kutunza risiti waafrika wengi huwa hatuzingatii vitu kama hivi tunapuuzia.Mimi hapa mpaka leo nina risiti za simu niliyonunua 2009
Mkuu na ww uache mawazo ya miaka ya 90 unasupport paperwork karne ya 21? Mtoa mada anahoja nzito.

Kwanini mtu akinunua simu TCRA isiweke database inayolink na wenye maduka ya simu kila wanapouza wakasajili IMEI against jina la mteja. Hata kma hana receipt ila siku akiuza anaenda na ID yake huko TCRA alafu mna swap details na simu inahamishwa mmiliki pale pale.

Kutunza makaratasi sio sustainable ni urasimu usio na tija hta mavyuoni ukilipa mpaka system ione muamala hta kma receipt huna utaandikiwa ya chuo. Tujifunze kuendelea na teknolojia sio kukariri vitu vya kale.

Heko Infantry Soldier
 
Back
Top Bottom