SoC03 Kwanini Tanzania ni masikini?

Stories of Change - 2023 Competition

Librarian 105

JF-Expert Member
May 6, 2023
239
325
KWANINI TANZANIA NI MASIKINI?
Umasikini ulikuwa mjadala wa kitaifa kabla ya mfumo wa vyama vingi kuingia nchini. Ukipigwa vita chini ya sera na mikakati ya Azimio la Arusha lililofuata falsafa ya uchumi wa kilimo na ujenzi wa viwanda utokanao na mapinduzi ya kijani.Huku viongozi kwa ushirikiano wa bega kwa bega na wananchi wakitekeleza mipango ya maendeleo. Baada ya hapo,tumebaki na kumbukizi ya baba wa taifa,aliyetuachia Tanzania hali ya kuwa haamini azimio lake limezimwa kama mshumaa. Nini kilifuatia?
Shinikizo la kuruhusu vyama vingi nchini likapelekea kutukia mambo yafuatayo:

Kisiasa.
Kwa mujibu wa kifungu cha katiba 3(1) na cha 9: ni vigumu kuushinda umasikini kutokana na nchi kufuata siasa za ujamaa wa kujitegemea wakati huo huo na mfumo wa kidemokrasia na vyama vingi. Hii ni mifumo miwili isiyoivaa katika chungu kimoja abadani. Hii haikuwa ajali ya kisiasa. Bali yalikuwa maamuzi yaliyolenga kulinda maslahi ya chama tawala dhidi ya vyama vya upinzani. Matokeo yake:-
  • uchama ukahodhi usimamizi na uendeshaji wa mihimili ya dola.
  • Ukada ukatumika kama kipaumbele katika ajira na utumishi wa umma.
  • Chama kikaendeleza uchumi wa kisiasa kwa malengo ya kudhibiti nguvu ya umma na siasa za vyama vingi.
Haya yalifanyika ili kukijengea chama taswira ya upekee kuwa ndicho chenye uwezo wa kuwaongoza watanzania pamoja na kuwaletea maendeleo.

Kiuchumi.
Kwenye kujenga uchumi wa nchi chama kilifanya yafuatayo:
  • Ilani ya chama kutawala mpango wa maendeleo wa taifa.Wananchi wakaachwa nyuma kushiriki shughuli za ujenzi wa nchi.Madhara yake tunayaona kwa kutazama jinsi rasimali za taifa zinavyonufaisha watu wachache.Haitoshi nao uchumi wa nchi ukaminya fursa ya kutengeneza mamilionea wapya kupitia njia zao za uzalishaji mali zisizofungamana na uswahiba wa kisiasa au ushirika wa kibiashara na kada ya viongozi serikalini.
  • Maslahi ya nchi kiuchumi kuwa utashi wa chama kwanza. Mara nyingi tunaona jinsi ripoti za CAG zinavyozimwa kufunika madudu ya miradi ya maendeleo,bajeti za nchi, na usiri wa mikataba ya uwekezaji inapotakiwa kuhojiwa bungeni. Nguvu kubwa hutumiwa na chama kulinda maslahi yake dhidi ya matendo ya ufisadi unaofisidi maslahi ya nchi.
Hakika inahuzunisha kuona bunge la bajeti linakaliwa halafu kwenye utekelezaji wake kwa wananchi zinahubiriwa ilani za chama. Kwa muktadha huu mwananchi anageuzwa kuwa mtaji wa kisiasa kusubiria kuvushwa hadi nchi ya ahadi ilhali ndiye mdau husika wa maendeleo.

Kijamii.
Leo hii tunalia kuporomoka kwa maadili ndani ya jamii. Lakini hatuhusishi kilio hicho na kuanguka kwa misingi ya utawala bora nchini. Demokrasia ya vyama vingi imekuwa yenye kutawaliwa na upebari wa chama tawala. Tunashindaje vita ya umasikini?
Ukirejea kifuchu cha katiba 145(1-2): serikali za mitaa zilianzishwa ili kupeleka madaraka ya umma kwa wananchi ili kuharakisha maendeleo. Kifupi kumegeuzwa kuwa maabara za kupandikizia watumishi wa umma kwa kutumia vinasaba vya ukada. Na bajeti za nchi ndiko zinakoteketezewa huko. Ambapo hakujadiliwi vita dhidi ya umasikini kulingana na mpango wa maendeleo wa taifa. Ilhali kuna rasilimali watu waliopita katika vyuo vya maendeleo na ustawi wa jamii!

Mbali na kukosa uthubutu pamoja na ubunifu, hali ya kimazingira imewaelemea kusimamia maslahi ya nchi. Imebaki, "kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake" kwa wengi wao kuzigeuza ofisi za umma kuwa maduka ya kifamilia. Hayo yakijiri. Huduma za kijamii kwa raia wa kawaida zinapitia mtihani mkubwa. Ili kuhudumiwa kwa haraka analazimika kufanya moja kati ya mambo yafuatayo a) kuwa mtumishi wa umma au chama b) kuwa ndugu wa mwajiriwa wa serikali ama chama au c) kutoa hongo ya rushwa ambayo kundi kubwa la wananchi ndiko linakoangukia. Na ukisema utazame jamii yenyewe giza ndilo linazidi kutamalaki. Kila mwenye shauku ya utumishi wa umma amefisidika kifikra na kimtazamo. Anayestaafu na kurudi mtaani akijivunia mafao yake, anaonekana mjinga machoni pa wengi.

Nini cha Kufanya?
Tunahitaji umoja wa kitaifa kuponya matatizo yetu ya kisiasa na kiuchumi. Lakini tukiendeleza propaganda za kisiasa zenye utashi wa kununua subira na uvumilivu wa watanzania kuwahimiza kulinda kisiwa chao cha amani. Tutambue hatujengi ila ni sawa na wachache kutoboa jahazi na sote tumo safarini.
Kwani hapa tulipo hatujafika kwa bahati mbaya au kwa ridhaa ya nchi yetu. Ni baada ya viongozi wa chama tawala kutoafika dira mpya ya taifa kusimamia mabadiliko ya kweli ya kidemokrasia na vyama vingi. Wakaamua kujivika cheo cha baba mlezi wa dola na nchi kwa ujumla. Sasa tunasuhubiana na nchi kupitia ukoloni mamboleo wa sisi wenyewe kwa wenyewe.

Ili tuondokane na hali hii. Yatakikana chama kwanza kijivue gamba la ubepari wa kichama ambo ndio chanzo cha matatizo na umasikini unaotukabili watanzania. Bila hivyo. Tunaweza kupata katiba mpya isiyotufaa kitu. Mfano wake itakuwa sawa na mvinyo wa zamani ndani ya chupa mpya.

Hamkani wao hutafuta umoja ndani ya chama kulinda maslahi ya chama kwa maridhiano na kuvumiliana? Je, kwa ajili ya maslahi ya nchi?! Hawana budi sasa kupokea ukweli tunaoumia ni sisi wanyonge wa Tanzania kwa kukataa kwao kujiweka katika hadhi sawa na vyama vingine vya upinzani. Ili wakae meza moja ya maridhiano ya kufanikisha inapatikana katiba mpya,yenye kufata misingi sahihi ya kidemokrasia na utawala wa kisheria, na mpango wa maendeleo wa taifa ukawa ndio ajenda ya kupokezana vijiti katika kuwatumikia watanzania.
Nimalizie kwa kusema: " Siasa sio mchezo mchafu kama uongozi utakuwa mikononi mwa wazalendo waadilifu na wawajibikaji".
 
Shukran kiongozi@Numbisa. Naamini mchakato wa mabadiliko ya kweli yanaishi mioyoni mwa watanzania, ni suala la muda tu.
 
Chanzo kimojawapo ni kuwa hata wewe ni maskini. Huwezi kuwa na watu maskini halafu nchi ikawa tajiri
 
Sawa. Umejibu swali kwa kusoma kichwa cha habari tu. Soma habari yote kwa umakini kisha changanya na akili zako utafakari, kwanini tanzania ni masikini? Wakati imejaliwa kuwa na rasilimali na maliasili mbalimbali.
Asante.
 
Back
Top Bottom