Kwanini Tanzania inakwamisha EAC?

Nyie mnaojua mambo hamieni Kenya mkaungane, sisi mtuache hapahapa kwa bibi. Ya nini kupata taabu ya kutuelewesha wakati Kenya ni free WaTz kwenda? Nyie nendeni mkaungane tutawakuta.

EAC si Kenya pekee!
 
Hii jumuiya mfu Faida zake ni kiduchu sana ukilinganisha na hasara lukuki.
Misingi ya kujiunga na jumuiya hii ni ya kizezeta na haijaweka kukuza MAENDELEO ya mwananchi wa kawaida wa nchi wanachama.
Huu na mipango mingi ya VIONGOZI wa kiafrika ndio kiini cha mabalaa na majanga katika baraka letu, UFISADI, uchu wa madaraka, ubinafsi na RUSHWA ndio Misingi ya kuanzishwa kwa jumuiya ya Afrika mashariki na watanzania wamelipotezea hilo litaasisi la kikabila kabla halijakomaa.
KUSHIRIKIANA SIO MPAKA MUUNGANE , KUJUANA MWISHO MIPAKANI, KILA MMOJA A BAKI KWAO
 

La, mie naona Wahenga walikuwa sawa: "Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu"
 
La, mie naona Wahenga walikuwa sawa: "Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu"
NI kweli tupu neno la wahenga, tushirikiane pale inapibidi lakini kuungana HAPANA,tulijaribu awali tukaishia njiani hakuna sababu ya Kurudisha tena NO.
 
NI kweli tupu neno la wahenga, tushirikiane pale inapibidi lakini kuungana HAPANA,tulijaribu awali tukaishia njiani hakuna sababu ya Kurudisha tena NO.

Sentebe, umeoa wewe? Kama ume, utajua "mavi ya kale hayanuki" na...."yaliyopita si ndwele (ugonjwa) tugange yajayo."
Halafu, mara nyingi watu wenye mawazo kama yako huwa hawaja interact na Mkenya kama mtu binfsi au hata pengine kumwona. Ni mawazo ya kujumuisha (generalization) yanayochochewa na wivu na chuki za kisiasa na...to be frank, a sense of inferiority tuliyonayo Watanzania!
Zaidi, hii siyo thread juu ya Ukenya na Utanzania. Soma kichwa cha habari.
 
Heri nusu shari kuliko shari kamili, wahenga walinena , ukishaumwa na NYOKA basi hata unyasi utaogopa, hivyo watanzania tulishagongwa na NYOKA kwenye jumuiya iliyokufa sasa msitulaumu kwa kuwa na tahadhari, NI RAHISI SANA KWA MLAKUNDE(KENYA NA UGANDA) KUSAHAU ILA SISI WATUPA MAGANDA (TANZANIA) HATUWEZI SAHAU TULIVYOSALITIWA.
TUSHIRIKIANE lakini muungano HAPANA
 
Maandishi mengi umejaza pumba tupu. Eti kuongea kiingereza unaijua EAC wewe au unabwabwaja tu. Nenda kaulizie EAC human capital ya jumuiya inategemea watu wa kutoka wapi! !!.Mnaongea vitu msivyofanyia utafiti. Pale EAC think tankers zinatoka Tanzania. Kwa kuhakikisha NENDA EAC kafanye utafiti siyo kubwabwaja tuuu . EAC ni Tanzania bila Tanzania hakuna EAC. Wanatuhitaji kuliko wao tunavyowahitaji tulia wanyooshwe
 
unaandika ujinga..unasifia uchumi unaopendelea wasomi wachache na watu wenye mtaji kwenye jamii ambayo sehemu kubwa hawakwenda shule!?
 
HA

Hata mtoto hawezi ku reason namna hii. Watanzania watu wa ajabu sana. Wale wanaoesabika "wanajua" wamejaa majivuno na mikogo. Si ingekuwa vyema kuelezea tu unachoona kimekosewa?
Sentensi yako ya mwisho yaonesha ujinga na kiburi.
 
unaandika ujinga..unasifia uchumi unaopendelea wasomi wachache na watu wenye mtaji kwenye jamii ambayo sehemu kubwa hawakwenda shule!?

Statistics or you are writing rubbish.
 
Bado tunatofauti kubwa kimfumo, mfano umiliki wa ardhi ampapo Tz ni mali ya Rais na kwa wenzetu kila mtu na chake.

Ili kufikia muungano, tungeachia madaraka ya baadhi ya rasilimali ziwe chini ya states (sijapata kiswahili chake).

Ninamaanisha kwamba.
  • Tuwe na Federation of East Africa.
  • Kila nchi iwe state na iwe chini ya govenor.
  • Kila state iwe na bunge lake na mamlaka yake ya mambo ya ndani.
  • Kila state iwe na sera yake ya ardhi, elimu na makusanyo na matumizi.
East Africa
  • iwe ni serikali itakayo simamia mambo ya nje zaidi.
  • Ihusike na kusimamia elimu kwa level ya juu zaidi.
  • Bunge la East Africa liwe kwenye ratio ya wingi wa watu na ukubwa wa state. Kwa mimi naprefer zaidi ukubwa.
  • Pia tuondoe ile tabia ya Ukenya, Utanzania, Unyarwanda n.k.
  • Tuondoe tabia ya kupenda madaraka, tuheshimu katiba haswa katika ukomo wa muda wa kutawala.
Kwa mimi nitasupport kama hayo yatafanyika, ila sio kuungano na kisha kuja kuwa kama Tanganyika na Zanzibar.
 

Labda useme kenya, uganda n rwanda nchi gan inaendeshwa na mtu mmoja kutoka bunge ,military had mahakama!! Hizo nazo nchi au n mashamba ya pk n m7?

Ss ndo nchi
 
Wewe ni mTanzania?

Hata kama wewe ni mTanzania, basi una walakini, pengine ndio uraia wa kununua.

Unasikia 'propaganda' halafu na wewe unazirukia bila hata kujiridhisha ukweli ni upi? Umeangalia takwimu zinazoonyesha kiasi cha watu wa Afrika Mashariki walioingia katika kila nchi mwanachama wa jumuia hiyo unayo zungumzia hapa?

Wewe utakuwa ni mtu toka Kenya, kwa sababu huko ndiko kwenye kiwanda cha kuilalamikia Tanzania kila mara kwa kila jambo, huku wenyewe ndio wakiwa vinara wa kutofuata wanayolalamikia.

Lakini hili linajulikana sababu zake.mmekuwa na hofu kubwa sana juu ya Tanzania jinsi inavyoinukia na kuchukua nafasi yake kwenye ukanda huu. Elewa kwamba malalamiko yenu hayatazuia chochote, Tanzania itaendelea kusonga mbele, mtake msitake. Hamuwezi kuzuia chochote.
 
Nilijua wewe ni boya, na wala siyo raia wa hapa.

Korea Kusini nao wako kwenye umoja gani? Japan ilijiunga na umoja gani kabla haijapata maendeleo. Kuendelea kwa ujerumani kulisubiri awe kwenye hiyo EEC?

Bure Kabisa.
 
Sasa si uhamie huko Kenya na Uganda ili ukaungane nao huko badala ya kutuletea ujinga na mawazo ya kitoto hapa. Kama unadhani Kenya wameendelea ebu nenda huko Karamoja kwa wakaramajong ukaone!
Unataka tuungane kesho, una haraka ya kwenda wapi? Hatupendi ujinga sisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…