Kwanini Tanzania hatukai na Rais wetu live na kumuhoji mambo mbalimbali katika TV kama Kenya?

mwambadog

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
1,736
1,446
Angalia wenzetu kenya Raisi Kenyatta akifanya mazungumzo mubashara na wananchi wake na wananchi wanamuuliza maswali kuhusu miradi ya kijamii na kufahamu ni kipi serikali inafanya.

Kenya presidential delivery portal launch

Mpaka raha angalau inapunguza maneno maneno
 
Uzoefu unaonyesha mahojiano kati yake na walioketi nao yalikuwa kama ifuatavyo.

Pengine kama unategemea matokeo tofauti, au unauzoefu mwingine, unaweza kuuweka hapa, ili kuhamasisha washauri na wahojaji.
 
hasira tu hakumaansha hivyo

ye anapangiwa na katiba na kusikiliza wananch wanaataka nin
 
Anaweza akakaa hata kesho ila watu wa kumhoji watakuwa washatengenezwa. Tanzania inaenda kama ni mchezo wa kuigiza tu, bado hatujawa serious na kufanya mambo kiuhalisia.
 
hasira tu hakumaansha hivyo

ye anapangiwa na katiba na kusikiliza wananch wanaataka nin

Alimaanisha nini zaidi ya kukataa kwamba hataki kushauriwa na kwamba yeye anajiamani na ndiye alfa na omega? Weka basi kielelezo cha maana uliyoielewa wewe.
 
Angalia wenzetu kenya Raisi Kenyatta akifanya mazungumzo mubashara na wananchi wake na wananchi wanamuuliza maswali kuhusu miradi ya kijamii na kufahamu ni kipi serikali inafanya.

Kenya presidential delivery portal launch
https://www.kenyamoja.com/tv/k24-live/

Mpaka raha angalau inapunguza maneno maneno
Una watu wa kumhoji ama utawaagiza kutoka nje ya nchi? Tanzania tuna waandishi? Hata ma talk show wetu ni bure kabisa. Magufuli anajua kabisa hana wana habari wa maana. Wewe utamweka rais kiti moto na kina Mayalla? Hata wana habari wetu walioajiliwa na vyombo vikubwa pia bure tu kina Kikeke na wenzake. Mtu unafanya kazi BBC unashindwa kupata muda wa kuja kumhoji rais wako wa nchi. Kenya, Uganda ndiyo wana wanahabari ndiyo maana utawaona hata wapo BBC world service, Voice of America. Wa kwetu wanawaweka katika vipindi vya udaku maana wanajua ndivyo vinalingana na sisi.

Angalia Alan Kasuja wa BBC world service, Shaka SSali wa Voa walinganishe na kina Mayalla ama Kikeke.

Kazi tunayo kubwa kuwafikia wakenya.
 
Alimaanisha nini zaidi ya kukataa kwamba hataki kushauriwa na kwamba yeye anajiamani na ndiye alfa na omega? Weka basi kielelezo cha maana uliyoielewa wewe.

kuna mambo mengi yanaonesha anasikiriza wananchi, mfano tumekuwa tukilala mika mafisadi kasikia kawaundia mahakama

na mengine mengi tu
 
Mimi swali langu la kunipeleka mahabusu litakuwa hili: Ndugu mheshimiwa, una undugu gani na Idd Amin, Charles Taylor, na Hitler?
 
Aliwaita waandishi wa habari wakauliza maswali pumba kabisa!
Huyu wa Kenya yupo ktk kampeni, hafanyagi hivyo!
 
Back
Top Bottom