Kwanini Tanzania Haikutuma Kiongozi Mwandamizi Kwenye Mazishi Ya Fidel Castro

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
Taifa la Cuba chini ya uongozi wa Hayati Fidel Castro Ilikuwa ina uhusiano mzuri sana na serikali ya Tanzania. Wakati dunia ikitutenga wakati wa serikali ya awamu ya kwanza serikali ya Cuba ilitupa misaada mingi ya kirafiki kama kuna vijana wetu wengi walipelekwa Cuba kusomea udaktari na madaktari wengi walikuja hapa nchini kufanya kazi.
Kwa Kumbukumbu yangu Rais Castro akiwa rafiki wa Mwalimu Nyerere alijenga bwawa kubwa la umwagiliaji maji mashambani pale Butiama (Kyarano Project). Fidel Castro alijitoa mhanga kupambana na mataifa ya kibeberu katika kugombea uhuru wa nchi nyingi za kusini za Africa.
Kulikuwa kuna hata umuhimu wa kumtuma Dk Salim Ahamed Salim ambaye alikuwa mwakilishi wetu (Balozi) nchini Cuba kwa muda mrefu. Majuzi makamu wa Rais wa Cuba alifanya ziara hapa nchini na kutoa ahadi ya kuendeleza ushirikiano wa kindugu kati yetu na Cuba. Viongozi wa Africa waliohuduria mazishi ya Comrade Castro ni Rais Mugabe wa Zimbabwe, Rais Obian Nguema wa Equatorial Guinea, Rais Jacob Zuma na Rais Uhuru Kenyatta.
Ni jambo la kusikitisha kwa serikali ya awamu ya tano kusahau historia ya mahusiano ya Tanzania na Cuba. Kulikuwa kuna umuhimu mkubwa kwa Rais Magufuli kuhudhuria mazishi haya kwani kwenye mazishi ya mtu aliyekuwa rafiki mkubwa wa baba wa taifa Mwalimu Nyerere na Watanzania wote kwa ujumla hakuna kisingizio cha kusema tunabana matumizi.
 
Watu wa pwani ndio wenye hulka ya kufarijiana kiukweli nankijaliana hasa kipindi cha misiba. Nimeishi bara na pwani, bara mtu kafiwa na manawe anakodisha mziki anagonga diamond, kiba na bia za kumwaga, pwani watu wanaomboleza kwa huzuni sio kuruka ndombolo.
 
Back
Top Bottom