Kwanini TanZania haiisaidii Somalia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini TanZania haiisaidii Somalia?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbogela, Dec 4, 2009.

 1. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Sina uhakika kama hii thread niianzishe kwenye jukwaa la habari za kimataifa au hapa.
  Kama tunavyojua kuwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele kwenye suala la ukombozi wa bara la Afrika. Tumesaidia kukomesha ukoloni, kutawaliwa na ubaguzi wa rangi kwa nchi zilizoko kusini mwa bara la afrika. Pia tumewasaidia Polisalio, tumesaidia Uganda, na nchi zote za ukanda wa maziwa makuu kutatua migogoro yao (ingawa hili la kuwauzia siraha tena, mmh! linatia doa). Tumepeleka majeshi yetu kulinda amani kwenye nchi zenye matatizo ya migogoro ya wenyewe kwa wenyewe. Bila kusahau operation ya JWTZ hivi karibuni huko Anjouan.

  Lakini pamoja na yote hayo sasa hivi kuna tishio kubwa tishio jipya, tishio linalohatarisha sio usalama wa majirani zetu lakini ni tishio linaloweza kuua biashara na mahusiano yetu na dunia nyingine. Tatizo linalofanya kuwe na makonteina yanayopita ndani ya aridhi yetu kama yana mizigo kumbe ndani yamebeba watu wanaokimbia nchi yao.Tatizo hili ni tatizo katika ghuba ya Aden, iliyoko kwenye pembe ya Afrika. Naliona ni tatizo kutokana kuongezeka kwa vitendo vya utekaji nyara wa meli zinazotoka au kuja pwani ya afrika mashariki.

  Kitendo cha maharamia wa kisomali kuendelea kupata malipo kutokana ana utekaji nyara wa meli hizo na raia wa kigeni hakitaisha leo wala kesho kama hatua za makusudi hazitachukuliwa. Maharamia wanajua kabisa kuwa hawawezi kukamatwa wala kushindwa kutoka na miundo mbinu yao waliyojiwekea ndani ya Somalia.

  Lakini nadhani, kama Tanzania ikiamua, Kama Tanzania itadhamiria kweli uwezekano wa kumaliza tatizo la Somalia upo na unatekelezeka.

  Kama ningekuwa waziri wa ulinzi wa JMT leo hii ningemshauri amiri jeshi mkuu, JK, kuanza operation maalumu ya kuisaidia Somalia. Kuisaidia Somalia kuwa na serikali yake imara yenye nguvu na jeshi imara lenye adabu na utiikwa serikali yao.

  Ningemshauri Tanzania ianzishe kambi maalumu za mafuzo kwa vijana wa kisomali ambao watakuwa tayari kulitumikia jeshi jipya la nchi yao. Vijana hawa wawe recruited na kupigwa msasa kabambe ndani ya aridhi ya Tanzania, wapewe mafunzo ya kijeshi na kinadharia ya kuipenda nchi yao na kujua umuhimu wa kuwa na serikali yenye nguvu.

  Kama tunaweza kufanikiwa kuzishawishi na nchi zingine kama South Afrika, Msumbiji, Zambia nk kila nchi ikazalisha wanajeshi wa kisomali sema kwa miaka mitatu mfululizo, kama kila mwaka tunatengeneza asikari 50,000 na nchi zingine zikafanya hivyo, ningekuwa na uhakika kuwa ifikapo mwaka 2015 hakuna tatizo la utekeji nyara meli na watu wasio hatia pwani ya Somalia.

  Naamini nchi zilizoendelea zipo tayari kutoa michango na misaada kutaka kusaidia kuhakikisha kuwa Somalia inatawalika, kwani nazo zimechoka kuendelea kutengeneza vichwa vya habari kwenye media kutokana na watu wao kila siku kutishiwa kukatwa vichwa na magaidi wa kisomalia. Obama angefurahi sana mpango huo kwani ungemsaidia kuibomoa ngome mpya ya Al Qaeda inayodaiwa kuanza kujengwa kwenye nchi isiyo na serikali wala jeshi, angetoa support. Na Tanzania ingepata kujenga uhusiano wake na marafiki zake wa nje kwa ukaribu zaidi. Tanzania inaweza, nia na sababu tunazo, tuwasaidie wasomalia jamani!!!!
   
 2. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2009
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,130
  Likes Received: 23,743
  Trophy Points: 280
  Hao wasomali hawasaidiki, waulize Wamarekani watakuambia. Watu wanapewa ukimbizi Marekani lakini baadae wanarudi Somalia kujilipua, ni kuwaacha mpaka watakapotia akili.
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hebu anza kwanza umsaidie Tumaini wa JF. Ukifanikiwa kumbadilisha yule Punda mbeba mizigo ya Mwinyi na Kikwete, basi tutakusaidia kwenda Somalia.

  Ila kama wee ni mla kiti moto, wala usidhubutu kuweka pua lako huko maana watakubeba, wakunolee kisu kwenye nywele zako na mwisho wakuchunje hadi wakate kichwa na kichwa wakupakatishe mikononi mwako.
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Tuimarishe ulinzi wa ndani kwani ujambazi tu unatushinda sasa iweje twende somalia.
   
 5. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Lakini Kundi la wasomali wakimbizi linaua uchumi wetu kwa kiasi kikubwa kuliko hata hao majambazi wa kutumia siraha ndani ya nchi yetu. Suala la Somalia halina uhusiano wowote na dini, somalia ni suala la koo na historia na ubabe nani amtawale nani. Kama mkakati makusudi unafanyika tunamaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe Somalia
   
Loading...