Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Jamii yetu inaona ni jambo jepesi sana kuishi kwa kutegemea uongo. Unampigia simu rafiki yako na kumuuliza umefika wapi anakwambia nimekaribia kituo cha Bamaga, kumbe ndio kwanza yupo Tegeta. Unabaki kusubiri ukidhani kuwa ndani ya dakika kumi atakuwa ameshafika Kijitonyama. Unasubiri kwa zaidi ya dakika hamsini bado hajatokea, kibaya zaidi yule anayezidi kuchelewa ndio mwenye umuhimu wa safari kuliko wewe ambaye umeshafika pale Kijitonyama.
Huo ni mfano tu wa maisha ya kubabaisha tuliyozea kuyaishi kwa takribani kipindi cha awamu ya kuanzia ile ya tatu mpaka sasa. Chanzo cha ubabaishaji naweza kusema kina uhusiano na elimu ndogo tulizonazo, hivyo mtu anaishi kwa kutegemea uwezo wake wa kusema uongo, uwezo wa kuongeza chumvi ili heshima yake iongezeke mbele ya watu anaokutana nao maishani.
Kumekuwepo na "ukanjanja" wa kila aina, kuanzia sekta zile nyeti mpaka zinazoonekana ni za kawaida tu. Sio ajabu Tanzania inaweza ikawa ni mojawapo ya nchi za Afrika ambazo raia wake wanaongoza kwa kupewa habari nusu au zilizopotoshwa (misinformed).
Tumekuwa ni taifa lenye watu laghai sana, watu ambao hupaswi kuwaamini hata kama macho yao wakati wakiongea yanaonyesha ile hali ya ukweli.
Sio dhambi hata kidogo ikiwa awamu hii ya tano, tutarudi kwenye misingi sahihi ya elimu za darasani. Tutarudi kwenye maisha ya kweli, sio haya ambayo mtu mwenye elimu ya "mashaka" lakini ana uwezo wa kuanzisha NGO fulani na uwezo wa kuongea mbele ya waandishi wa habari, anatajirika upesi zaidi kuliko mtu mwenye taaluma yake ambaye hana uwezo wa kuwa "mwongo".
Ni safari ndefu itakayokumbana na maadui wengi waliozoea maisha haya ya kubabaisha, lakini ikiwa kweli tunataka kuiona Tanzania ya viwanda ikishindana na mataifa mengine yaliyotilia mkazo elimu, basi hatuna budi kuianza.