Kwanini stand ya mkoa wa Morogoro ni ya hovyo miaka na miaka?

Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
14,634
32,007
Hii stand kwanini haikarabatiwi licha ya kuhudumia mabasi lukuki kila kukicha? Ukipita masika tope, ukipita kiangazi vumbi!

Tatizo ni nini?
 
Kwa Mara ya mwisho kufika Moro ni lini mkuu?? Nafikiri utakuwa una muda mwingi haujafika Moro aisee!!
 
Under construction: Mara ya mwisho ulipopita palikuwa bado lakini kwasasa kuna jambo jema linafanyika mle ndani. Pita ukachungulie tena
 
Kweli kuna jengo la nguvu linapanda pale, lakini vumbi bado lipo.
 
Hii stand kwanini haiakarabatiwi licha ya kuhudumia mabasi lukuki kila kukicha? Ukipita masik tope, ukipita kiangazi vumbi!

Tatizo ni nini?
Uko ulipotoka stendi zipoje mkuu,na uko unapoenda utazikiutaje?hukuona ujenz unaendelea hapo moro?
 
Stendi ya moro iko kwenye upanuzi mkubwa sana na ndio itakuwa stendi bora Tanzania. Inaonekana mtoa mada ulikuwa umelala ukastuka bila kuangalia ujenzi unaoendelea pale Msamvu
 
Stendi ipi Unayosemea? Kwani we huoni km ipo under construction? Nadhani utakua haujapita ck mingi bado mda kdg ikikamilika hata ubungo itakua haioni ndani
 
Mkuu wewe utakuwa unazungumzia makeshift bus stand. Hiyo 'uliyoingizwa' wewe ni stendi ya muda. Hapo pembeni yake kuna jengo kali la stendi linajengwa.
 
Nimepita pale mwezi uliopita palikuwa tope kule ndani hakuna pa kukanyaga, labda kama wameshapakarabati siku hizi za karibuni.


Nilikuwa natokea Iringa!
Labda stendi ya Mikumi. Morogoro kubwa sana ujue. Hata Mikumi ipo ndani ya Morogoro
 
Mkuu wewe utakuwa unazungumzia makeshift bus stand. Hiyo 'uliyoingizwa' wewe ni stendi ya muda. Hapo pembeni yake kuna jengo kali la stendi linajengwa.
Wewe ndio umemueleza vizuri kwa mgeni akipita pale atajua ndio stand ila ukwel ni kwamba stand ipo under construction na itakuwa stand bora sana.
 
mimi mwenyewe nipo hapa msamvu nasubiri kuondoka, kuna ujenzi unaendelea wa nguvu ila huku nje yanakopaki mabus kuna vumbi laana
 
Iyo stendi temporary. inayolekebishwa ndo ilikuwa ikitumika miaka yote na haikuwa na vumbi unaposema miaka nenda rudi ndo tunakuwa hatukuelewi
 
Kwa uelewa wangu stand ya Morogoro pale msanvu ndio bora nikilinganisha na mikoa kadhaa niliyopita. Ila cha ajabu bado wameibomoa wanataka kutoa kitu bora zaidi pale. Pongezi kwao
 
Mtoa mada kakosea kusema miaka nenda rudi wakati kulikuwa stand lami tupu ndani ila kwa sasa wameiweka ya dharula pembeni kwa ajiri ya ukarabati hii ya kwanza kwani huyu bwana hakuona uzio wa mabati yaliandikwa mwiguru nchemba rais
 
Back
Top Bottom