Kwanini sitta na wenzake hawaondoki CCM ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini sitta na wenzake hawaondoki CCM ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kasyabone tall, Sep 18, 2009.

 1. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2009
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  Kwanini sitta na wenzake hawaondoki CCM?
  Watu wengi wakiwema hata wasomi wakubwa katika nchi hii wanajiuliza kwa nini sitta na watu wenye msimamo kama wake hawaondoki CCM na kuunda chama chao au kujiunga na upinzani.
  Historia ya nchi hii inaonyesha hakuna mtu au watu wameasi CCM wakafanikiwa. Watu wenye malengo ya kisiasa wakimuona mwenyekiti wa TLP mrema alivyofifia kisiasa wanapatwa na hofu kukiacha chama.
  Ukweli ni kwamba vijijini bado wapo watu wanamkumbuka mwalimu kwa uadilifu na uzalendo wake. Wanakihusisha chama na mwalimu kwa kuwajali watu wote. Kwa maana hiyo si rahisi kwa mwana ccm mwenye malengo ya madaraka makubwa kuhama chama.
  Lakini kuna watu wanaofikiri kuwa ni kundi la spika na wenye msimamo kama wakae wanaotakiwa kuondoka chamani au kujiunga na upinzani.
  Huenda wakina sitta nao wanamsimamo wao wakiamini kuwa wao ndio wanaokiwakilisha ccm asili ambayo imekuwa ikikubalika kwa wananchi. Hivyo wanawashangaa kuwa inakuwaje watu wanataka wao ndio wakiame chama.
  Kumekuwapo na usemi kuwa ccm inawenyewe. Mwanzoni kauli hile ilchukuliwa tu kama zingine. Wengine waliamini kuwa ilimaanisha kuwa ccm ni ya wakulima na wafanyakazi. Wengine wakaamini kuwa ccm ilikuwa ni ya wasisi wa taifa na walioleta uhuru. Wengine walielewa kuwa ccm ni ya wanachama walioamini katika imani na ahadi za CCM.
  Na hivi karibuni ccm imeendelea kuwachanganya watu zaidi kwani wanaoweza kudai uhalali wa kuimiliki wameongezeka sana. Na huenda kilichotokea DODOMA kilitoa jibu ni nani mmiliki halali wa ccm.
  Baada ya kundi la walio katika mapambano ya ufisadi (WAMADU) kudhalilishwa na kutishiwa wameamua kutumia nguvu ya umma kudai mafisadi wawaachie ccm yao “ CCM asilia”.
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mbona watu wanataka kuwasafisha kina Sitta na wakati alikuwa na yeye anatuhuma kibao za ufisadi? Nadhani kwa ujumla hakuna msafi CCM. Wote wamekaa na kula pamoja. Ni kama sisi tuibe wote, alafu wewe uchomoke na kuanza kusema mimi ndo mwizi. Hali halisi ni kwamba, wote ni fisadi. Na kwa namna moja au nyingine wamehusika katika utumizi mbovu wa pesa za umma. Siku izi fisadi wamepewa title ya WAPIGANAJI. Hizi ni spins tu. Kama wewe ni fisadi, utabaki fisadi.
   
 3. K

  Kinyikani Member

  #3
  Sep 19, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Usibabaishwe na wote ni wezi, waongo just tisha toto tuu wote ni njaa tu ndio inaowasumbuwa
   
Loading...