Habari zenu Watanzania wenzangu na poleni na majukumu ya ujenzi wa Taifa letu hili changa.
Baada ya salamu kwenu nimeona si vibaya nikapata ujuzi na uelewa zaidi juu ya masuala mbalimbali ya Taifa hili ili niondoke katika utata katika masuala kadhaa yanayoniumiza kichwa.
Kwanza ningependa kujua au ninavyofahamu mie ni kwamba Visiwa vya Zanzibar/Pemba viliungana na Tanganyika kuunda nchi moja inayoitwa Tanzania, lakini katika kipindi cha karibuni tumeweza kuona mabadiliko mengi na hasa kila anayeunga au kupinga hoja hizi za muungano kutetea maslahi ya Taifa lake hapa namaanisha Wazanzibar, Wapemba na kiasi kidogo kwa Watanganyika.
Tumeweza kuyaona hayo bungeni na katika baraza la wawakilishi na kwa kiasi kikubwa hoja ya Mafuta kuwa ni suala la Muungano au la Visiwani Pekee.
Katika kipindi hiki tumeona mabadiliko mbalimbali kwa upande wa Visiwani mfano, Bendera ya Zanzibar, Vitambulisho vya Mzanzibar mkazi, kura zilizopigwa hivi karibuni (SERIKALI MSETO) na Mengineyo mengi yanayoamsha maswali na fikra za hali ya juu.
Nimeona nijadili nanyi haya ili nijue nanyi mnadhani kipi kifuate? Nasi twahitaji vitambulisho vya Mtanzania mkazi au siyo? Serikali zetu zi ngapi? Na bendera yetu ya Bara ni ipi na Ya Tanzania, nafikiri haya ni muhimu kuyajua na kuyafanyia kazi kwa maslahi ya ustawi wa Taifa letu.
Ufike wakati sie wote tujue kama tuko na serikali tatu, nne au tano na Muungano.
MOLA ATUBARIKIE
UCHAGUZI WA FANAKA