Kwanini Simba huingiza kikosi kamili kwenye kombe la mapinduzi?

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
15,964
24,584
Mabingwa wa mapinduzi cup hapa east Africa (Simba) mwaka huu nimeona wanaingiza kikosi full mkoko (first eleven) tofauti na miaka iliyopita

Hizi zaweza kuwa ni mojawapo ya sababu
1. Uoga, kocha anaogopa kufanya rotation sababu anaogopa lawama.

2. Pia msimu huu Simba haina uhakika wa kubeba kombe la ligi so wanachofanya ni Bora wabebe ubingwa wa mapinduzi.

3. Mashabiki wake wengi ni mbumbumbu, na wanapenda sana kulalamika hovyo. Kwa hiyo viongozi na benchi la ufundi wanalazimika kuwachezesha wachezaji wale wale kuka mechi, ili tu ushindi upatikane......according to Tate Mkuu

NB: Je unahisi sababu zingine zaweza kuwa ni zipi?
 
Kwani hao wachezaji unaowaita first eleven kazi yao ni ipi? Wana mikataba kwa ajili ya kusakata kabumbu.

Ukijifanya una kikosi kipana utaishia kudhulumiana na Jamus FC ya wajaluo wa sudani kusini.

Kupanga ni kuchagua
 
Umeona wanachokifanya wananchi??
 
3. Mashabiki wake wengi ni mbumbumbu, na wanapenda sana kulalamika hovyo. Kwa hiyo viongozi na benchi la ufundi wanalazimika kuwachezesha wachezaji wale wale kuka mechi, ili tu ushindi upatikane.
 
Mleta mada ni nyoka wa kijani. Kama wachezaji hawako timu ya taifa unataka wakae tu au wakauze bangi?? Mashindano haya huenda kocha anayatumia kwa kukijenga kikosi na utimamu wa mwili kwa wachezaji. First 11 iko kwenye akili yako tu ila mchezaji yeyote anaweza kuwa ktk first 11 kama ni wa club husika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…