Tatizo la Simba liko kwenye Uongozi

ITR

JF-Expert Member
Sep 22, 2022
4,453
11,375
Baada ya kipigo cha kizembe jana nakuja na maoni yafuatayo;

Tangu Babra aondoke Simba Uswahili umerudi kwa kasi sana kwenye uongozi wa Simba, kwa hiyo hata Simba akiletwa Kocha na kusajiliwa wachezaji wengine wazuri hakuna kitakachobadilika iwapo watu wenye tabia za Uswahili wataendelea kuwa ndani ya uongozi wa Simba.

Kiashiria cha kwanza kuwa tatizo la Simba liko ndani ya uongozi ni kitendo cha kumbakisha Boko ndani ya kikosi msimu huu, kwa levo za Simba ya sasa Boko sio mchezaji anayestahili kuwa ndani ya kikosi cha Simba lakini cha kushangaza anapata mpaka namba fast 11.

Boko ambaye kwa sasa hana hata stamina ya kuidhibiti mpira hata wa pasi, moja kwa moja inaonekana kuwepo kwa Boko ndani ya Simba kunawanufaisha baadhi ya Viongozi wa Simba.

Kiashiria cha pili ni u'father unaooneshwa na baadhi ya wachezaji hapo Simba mfano; mzuri ni Ntibazonkiza, watu wanasema Miqson ameshuka kiwango lakini cha kushangaza Miqson ambaye huwa anacheza dakika ishirini katika mechi chache amekuwa na impact na faida kwenye matokea ya Simba kuliko Saido anayecheza dakika 90 na kila mechi.

Ni kwa sababu Miqson sio mtu anayepoteza pasi hovyo na huwa asaidia timu kukaba na ametoa baadhi ya assist za magoli, lakini upande wa Ntibazonkiza amekuwa ni mtu ambaye asilimia kubwa ya pasi zake aidha anyanganywe mpira kirahisi au ampasie adui!

Amekuwa muharibifu mkubwa wa movement za Simba pale anapopewa mpira ili aanzishe shambulizi, mara nyingi huwa ananyanganywa mpira kiurahisi na shambulizi kufa na pia huwa hakabi.

Ila pamoja na mapungufu yote hayo Saido amekuwa ni lazima aanze kila mechi na lazima acheze dakika 90 zote haijalishi amecheza vizuri au vibaya, hali hiyo inaonesha kuwa kuchezeshwa kila mechi kwa Saido ni maekekezo kutoka kwenye uongozi na sio matakwa ya Kocha.

Beki line ya Simba ilianza kuonesha udhaifu mkubwa tangu mwanzo wa ligi kwenye mchezo wa kwanza na bado ikaendelea kuonesha uozo karibia kila mechi lakini cha kushangaza hakuna jitihada yeyote iliyokuwa inaoneshwa na Kocha wala Uongozi kulitatua hilo.

Badala yake wachezaji wale wale wanaofanya makosa kwenye diffense line ndio hao hao wanachezeshwa kila siku licha ya kuwa Simba ina wachezaji wengi hawapewi nafasi kabisa. Nimesha andika zaidi ya nyuzi tatu juu ya mashaka yangu makubwa kwa beki ya Simba lakini watu wakanikejeli.

Halafu jana hakukuwa na ulazima wowote wa kuanzishwa kwa Manura jana, licha ya makosa mengi ya mabeki lakini pia Manura hakuwa kwenye mchezo kabisa.

Cha mwisho, kama Simba watafukuza benchi la ufundi wasisahau pia na makanjanja yaliyojazana hapo Simba yanayojiita 'Viongozi wa Simba', kumbe ndio maana Babra alifanyiwa figisu ili aondoke maana alikuwa amedhibiti makanjanja na madalali.
 
Kweli
Tatizo la Simba linaanza na uongozi wa juu kabisa
 
Kila Neno litasemwa....

Ungetulia Baada ya siku mbili hadi tatu ungetoa ushauri wako.

Ila kwa sasa tutasoma kila kitu hapa jf
Tutasikia kila kitu.
Mkuu hilo ndo tatizo lenu, huko nyuma tumeleta nyuzi nyingi zinazo ongelea mafungufu ya Simba ndani na nje ya uwanja lengo likiwa viongozi na benchi la ufundi uyafanyie kazi lakini mkatukejeli kuwa hatujui mpira , lakini kadili siku zinavyo enda kila kitu kina zidi kujiweka wazi ya kuwa ndani ya Simba kuna kitu hakiko sawa, ya hayo mambo yasipo badilishwa tuta kuja kukumbana na aibu zaidi ya tulio kutana nayo jana.
 
Kwahiyo Bocco anaingiaje kwenye mchezo wajana, kitendo Cha kuanza kumtaja Bocco unaonesha ulivyo kiazi
 
Kwahiyo Bocco anaingiaje kwenye mchezo wajana, kitendo Cha kuanza kumtaja Bocco unaonesha ulivyo kiazi
Sijaongelea mechi ya jana mkuu ebu soma mada vizuri bali nime ongelea matatizo kiujumla yanayo ikumba simba.

Udhaifu wa beki ya simba haujaanza kuonekana jana bali ni wa siku nyingi ni basi tu timu pinzani hawakuwa makini tu.
 
Kila Neno litasemwa....

Ungetulia Baada ya siku mbili hadi tatu ungetoa ushauri wako.

Ila kwa sasa tutasoma kila kitu hapa jf
Tutasikia kila kitu.
20231106_104908.jpg
 
Mo hatoi hela,ni bahili,hapo ndio ahida inapoanzia
Mkuu sasa kama hatoi hela mbona kamati ya usajili wa simba ilikataa kumpa million 70 Mdathiru Yahaya ili asini simba badala yake wakaenda kumsajili sawa dogo kwa milion 200?

Alafu unacho takiwa kujua ni kuwa Mo sio mmiliki wa Simba bali muwekezaji mwenye hisa 49% hivyo anatoa fedha kutokana na hisa anazo miliki ili kuendesha club, asilimia zilizo baki zina milikiwa na wanachama hivyo na wao wanatakiwa kutoa fedha zinazo endana na umiliki wa hisa zao.
 
Unauhakika hizo hela zilitoka,simba ni wasanii sana
 
Mkuu sasa kama hatoi hela mbona kamati ya usajili wa simba ilikataa kumpa million 70 Mdathiru Yahaya ili asini simba badala yake wakaenda kumsajili sawa dogo kwa milion 200?

Alafu unacho takiwa kujua ni kuwa Mo sio mmiliki wa Simba bali muwekezaji mwenye hisa 49% hivyo anatoa fedha kutokana na hisa anazo miliki ili kuendesha club, asilimia zilizo baki zina milikiwa na wanachama hivyo na wao wanatakiwa kutoa fedha zinazo endana na umiliki wa hisa zao.
Kwani mfumo wa hisa imeshaanza kufanya kazi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom