Kwanini shuleni wanalazimisha wimbo wa Taifa?

Kwanini shuleni wanalazimisha wimbo wa Taifa?

Nilufer

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
9,762
Reaction score
14,005
Mi tangu primary nalazimishwa kuimba wimbo wa taifa japo huwa sipendi.

Mi siamini uwepo wa Mungu na katika wimbo ule kuna maneno kama "Mungu ibariki Tanzania"
Jamani mi naona wawe wanawaacha ambao hawataki kuimba wimbo huo siyo wote ambao tunamkiri Mungu huyo mnayemjua aliyeletwa na wazungu halafu mkakariri.

Mkiona mtu kakaa kimya wakati wimbo wa taifa unaimbwa ujue ana maana yake tusilazimishane.
 
Naona unaundugu na jamaa humu jf ambaye na yeye haamini uwepo wa Mungu.
 
Sio lazima umaanishe kinachotoka mdomoni.

Mungu atawabariki wote mpaka wewe usiyeamini, sababu ya wachache wanaomaanisha wanachoimba.

Kwani sala ya asubuhi bungeni, wale jamaa huwa wanamaanisha kweli???
 
Wewe lazima Utakuwa illegal migrant na sio mwana kwetu.
Kwani huoni jina lake. Huo ni mji mmoja huko Asia. Lazima wimbo wa taifa umpe kizunguzungu. Ukiwa mtanzania lazima ukusisimue tu ukiuimba
 
Mung'unya tuu mdomo,badala ya MUNGU we sema shetani.nothing bad mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom