Kwanini serikali ya sasa haiaminiki?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Watumishi wa umma waliambiwa wasubiri suala uhakiki ni la muda mfupi ili maslahi yao yatazamwe sambamba na ajira kwa watumishi wapya lakini hadi sasa matamko ni mengi, katibu mkuu utumishi anasema yake,waziri nae anasema yake.

Serikali ilisema tuwachangie ndugu zetu wa Kagera kwa kila anayekugwa kwa wahanga hao kubomolewa nyumba na tetemeko hilo, Lakini serikali ikasema kila moja abebe msalaba wake.

Serikali ilisema itapanga ada elekezi kwa shule zote binafsi na serikali lakini juzi tukaambiwa kuwa ada kwa shule binafsi ni makubaliano kati ya mmiliki wa shule na mzazi.

Serikali kupitia taasisi yake ya EWURA ikasema inapandisha gharama za Umeme, lakini akajibu waziri kwa kusema hakuna umeme kupanda.

Serikali ilisema kuwa itahakikisha itafanya kila jitihada kunusuru bei ya sukari kupanda ikiwa ni pamoja na kuagiza sukari ya kutosha kutoka nje, lakini mpaka sasa sukari ni zaidi ya Tshs 2400.
 
  • Thanks
Reactions: bne
kama nilivyosema miaka hii mitano itakuwa ya kusikia na kuona mambo mengi ya ajabu hasa kutoka kwa watu tuliokuwa tunawategemea kutuletea maendeleo
 
kama nilivyosema miaka hii mitano itakuwa ya kusikia na kuona mambo mengi ya ajabu hasa kutoka kwa watu tuliokuwa tunawategemea kutuletea maendeleo
Matamko yamekuwa mengi na yataendelea kuwa mengi kwa sababu moja kubwa. Kuongea bila kukaana kupanga nn kifanyike na nn kianze. Watawala wetu wamekiwa na hulka ya matamkp mengi ambayp hayajafanyiwa utafiti, ambayo huishia kutofanikiwa. Ushauri. Kabla mkulu hajatamka lolote. Aombe msaada kufanyiwa utafiri mdogo wa mile anachotaka kuongea au kikifanyoa maamuzi. Akibaini mawazo yake yako sahihi atamke na kitekeleza. Akiona kuna utata. auchune. Hapo atakuwa salama na hatasumbuliwa na pepo LA kukirupika
 
Mtu mwongeaji sana mara nyingi ana hasara kuliko faida, hii serikali ni ya waongeaji tu. Ongea na vitisho vingi uonekane. Mh. Naye kavikwa kilemba cha ukoka
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom