Jum Records
JF-Expert Member
- Jun 30, 2014
- 547
- 551
Habari ndugu,
Nimekuwa nasafiri mara kwa mara kwenda au kutoka mikoani kutokana na kazi ninayoifanya, ila nikiwa njiani nikikatiza kwenye mapori mbalimbali hapa Tanzania nimegundua kuwa tuna ardhi kubwa sana ambayo haijawahi kuguswa kwa maana ya kulimwa.
Sasa nimekuwa nawaza kwamba kila mwaka Chuo kikuu cha kilimo SUA kimekuwa kinatoa wataalam mbalimbali wa sekta ya kilimo, sasa kwanini Serikali hii isiwatumie kulima kilimo cha kisasa katika maeneo mbalimbali nchini kulingana na aina ya udongo, hali ya hewa na mengineyo?
Kuwepo kwa tetesi nchi ina njaa wakati maeneo makubwa na mazuri ya kilimo yapo yamekaa tu ni aibu kwetu sote.