KERO Kwanini Serikali inaonekana kuubana mkoa wa Kagera kielimu? Mpaka leo hakuna chuo chochote cha degree. Chuo cha kanisa kilifungiwa

KERO Kwanini Serikali inaonekana kuubana mkoa wa Kagera kielimu? Mpaka leo hakuna chuo chochote cha degree. Chuo cha kanisa kilifungiwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,451
Ni hali ya kusikitisha kwamba, licha ya historia yake yenye mafanikio katika elimu, mapenzi makubwa katika elimu, jitihada, uwezo wa kipekee, na mchango mkubwa katika kuzalisha wasomi, Kagera bado haina chuo chochote kinachotoa elimu ya juu ya kiwango cha degree.

Vyuo vinavyopatikana ni vile vya ngazi za chini ufundi, unesi, ualimu, n.k. vyenye kutoa certificate na diploma pekee, jambo linaloacha pengo kubwa kwa wanaotamani elimu ya juu ndani ya mkoa.

Kulikuwa na tawi la chuo cha SAUT Bukoba lakini lilifungiwa, na hivyo kuondoa chaguo pekee lililokuwa likikaribisha wanaotafuta elimu ya juu.

Katika nchi yetu kuna mikoa yenye historia, juhudi, uwezo na mapenzi makubwa ya elimu, na ambayo imezalisha wasomi wengi. Miongoni mwa mikoa hiyo ni Moshi, Mbeya, Kagera na Mwanza. Kwa kuwa mikoa yote hiyo imejengewa vyuo, kwa nini isiwe Kagera pia ?

Inaumiza kuona kuna mikoa inaendelea kujengwa vyuo vya ziada, kupanuliwa vyuo vilivyopo wakati Kagera hakuna chochote, It really pains a lot.

Tulisikia kulikuwa na mpango wa kujenga tawi la Chuo Kikuu cha UDSM, lakini baada ya taarifa za nchi za Ulaya kusitisha misaada, matumaini yanaendelea kufifia.
 
Huwezi kupoteza mahela kujenga chuo mahali palipojaa vilaza, na pengine Museveni akiamua kuvamia tena kama babu yake Amin wakachoma majengo, itakuwa ni hasara kubwa kwa uchumi wa Taifa.
 
Mnataka chuo ili mkakijaze maji ya katerero?.wahaya mnashida sana
 
Kwa nini serikali inaonekana kuubana mkoa wa Kagera kielimu ? mpaka leo hakuna chuo chochote cha degree.
Mara, Manyara, Singida, Shinyanga, Kigoma, Njombe, Lindi, Mtwara, Tanga, Simiyu, Rukwa, Katavi, nk.. kuna vyuo vinatoa degree huko?
 
Nyie wahaya mna tambo ila Kagera ni sehemu ya hovyo sana, ni tifauti na umaarufu wake
Mitazamo wako uliojaa kejeli za kikabila si hoja. Umaarufu wa Kagera umejengwa kwenye historia, rasilimali watu na mchango wake katika elimu,

Kama sehemu ya nchi Kagera nayo inahitaji kuendelezwa katika kile wanachokiweza zaidi, ELIMU
 
Licha ya kuwa mkoa mojawapo unaotambulika kwa kutoa wasomi wakubwa kitaifa na kuendelea kuwa na nafasi kubwa katika elimu, bado hakuna chuo hata kimoja Kagera kinachotoa degree, masters, au PhD.

Vyuo vinavyopatikana ni vile vya ngazi za chini ufundi, unesi, ualimu, n.k. vyenye kutoa certificate na diploma pekee, jambo linaloacha pengo kubwa kwa wanaotamani elimu ya juu ndani ya mkoa.

Kulikuwa na tawi la chuo cha SAUT Bukoba lakini lilifungiwa, na hivyo kuondoa chaguo pekee lililokuwa likikaribisha wanaotafuta elimu ya juu.

Ni hali ya kusikitisha kuona kuwa, pamoja na rekodi yake nzuri na mchango wake mkubwa katika kuzalisha wasomi, Kagera haina hata chuo kimoja kinachotoa elimu ya juu ya kiwango cha degree.
Nilisikia UDSM wanajenga tawi huko kama sijakosea.
Bado hawajaanza?
 
Mara, Manyara, Singida, Shinyanga, Kigoma, Njombe, Lindi, Tanga, Simiyu, Katavi, nk.. kuna vyuo vinatoa degree huko?
Upo Tanzania ipi ? Tanga, SIngida, Kigoma kuna TIA inatoa Degree, Shinyanga kuna chuo cha Ushirika, Simiyu kuna IFM inatoa degre, hadi Sumbawanga kuna MUST wanatoa degree ya engineering

Na ni kweli baadhi ya maeneo yana changamoto za kielimu, lakini maendeleo ya elimu hutegemea zaidi historia, uwezo, juhudi za jamii kwenye elimu. Kagera ina msingi thabiti wa kuendelezwa zaidi, kagera ni mkoa unaothamini sana Elimu na watu wake wana uwezo wa kipekee kwenye elimu.
 
Huwezi kupoteza mahela kujenga chuo mahali palipojaa vilaza, na pengine Museveni akiamua kuvamia tena kama babu yake Amin wakachoma majengo, itakuwa ni hasara kubwa kwa uchumi wa Taifa.
Mjadala wa kielimu unahitaji misingi ya ukweli na data, si maneno ya kejeli au ubaguzi.
 
Licha ya kuwa mkoa mojawapo unaotambulika kwa kutoa wasomi wakubwa kitaifa na kuendelea kuwa na nafasi kubwa katika elimu, bado hakuna chuo hata kimoja Kagera kinachotoa degree, masters, au PhD.

Vyuo vinavyopatikana ni vile vya ngazi za chini ufundi, unesi, ualimu, n.k. vyenye kutoa certificate na diploma pekee, jambo linaloacha pengo kubwa kwa wanaotamani elimu ya juu ndani ya mkoa.

Kulikuwa na tawi la chuo cha SAUT Bukoba lakini lilifungiwa, na hivyo kuondoa chaguo pekee lililokuwa likikaribisha wanaotafuta elimu ya juu.

Inaumiza kuona kuna mikoa inaendelea kujengwa vyuo vya ziada, kupanuliwa vyuo vilivyopo wakati Kagera hakuna chochote, It really pains a lot.

Ni hali ya kusikitisha kwamba, licha ya historia yake yenye mafanikio katika elimu, mapenzi makubwa kwa elimu, uwezo wa kipekee, na mchango mkubwa katika kuzalisha wasomi, Kagera bado haina chuo chochote kinachotoa elimu ya juu ya kiwango cha degree.
Kwani wakazi wa Kagera wanazuiliwa kusoma kwenye vyuo vilivyopo nchini?
Kumbuka mhaya wa Kagera ana haki sawa wa mzaramo wa Dar na mluguru wa Morogoro likija suala la kujiunga na vyuo vya maeneo tajwa.
 
TiA ni University?
Kwetu hapa Tanzania Institute, college na University hazina utofauti katika kupata degree. watu watatu tofauti wanaochukua degree inayofanana kwenye college, institute na university wana sifa ile ile.

Institute inaweza kuwa chini ya taasisi au wizara au University kwajili ya kufundisha vitu vichache mfano TIA ipo chini ya wizara ya fedha kwajili ya kozi za biashara

University ni chuo kikuu huwa na lengo la kutoa fani nyingi zaidi na elimu ya juu zaidi hadi Phd
 
Chuo kikikuu cha Dar (UDAM) kinajenga tawi lake Mkoa wa Kagera wilaya ya Bukoba na jiwe la msingi la chuo hicho litawekwa tarehe siku mbili zijazo... Atakaeweka ni JK au Nchimbi.
 
Chuo kikikuu cha Dar (UDAM) kinajenga tawi lake Mkoa wa Kagera wilaya ya Bukoba na jiwe la msingi la chuo hicho litawekwa tarehe siku mbili zijazo... Atakaeweka ni JK au Nchimbi.
soma paragraph ya mwisho
 
Si mjenge wenyewe tu, sio mpaka mjengewe na serikali
You give and get, Kama mkoa unachangia kodi ni haki yake kuletewa miradi inayoweza kuwafaidisha zaidi, kwa mkoa wa Kagera watu wanapenda sana elimu
 
Kwani wakazi wa Kagera wanazuiliwa kusoma kwenye vyuo vilivyopo nchini?
Kumbuka mhaya wa Kagera ana haki sawa wa mzaramo wa Dar na mluguru wa Morogoro likija suala la kujiunga na vyuo vya maeneo tajwa.
Maendeleo ya elimu hutegemea zaidi historia, uwezo, mwamko, juhudi ya jamii kwenye elimu.

Kagera ina msingi thabiti wa kuendelezwa zaidi, kagera ni mkoa unaothamini sana Elina na watu wake wana uwezo wa kipekee kwenye elimu.

Wazaramo na waluguru wana vyuo lakini humo vyuoni waliojaa ni wengine, kila jamii huwa na interests yofauti, wazaramo wanapenda zaidi sanaa, michezo na burudani, huko wana uwezo wao wa kipekee na tunajionea walivyo fanikiwa kwenye hizo sekta.
 
Back
Top Bottom