Kwanini sarafu ya shilingi mia tano haipati kutu?

Carbondioxide

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
733
195
Kichwa cha habari kinavosema kwanini sarafu ya shilingi mia tano yaani Shingi mia tano ya chuma haipati kutu?Tofauti na Shingi,5,10,20,50,100,200 za kitanzania hizi zinapata kutu kwanini?Isipokuwa sarafu ya mia 5 haipati kutu kwanini?Kuna nini ndani yake?
 
Bado mpya iyo wewe, subiri subiri ikae muda utaona kutu.

Hii si imetoka mwaka jana tu! Unalinganisha na hela za zamani kama sh 5, 10, 20 nk?

Acha hayo mambo bana, au unatuona hatukumbuki kama hiyo hela ni mpya siyo!
 
Mkuu hii sarafu kwa mujibu wa benki kuu wanasema, imetengenezwa kwa chuma kilichonakshiwa(coated) na nikeli,kabla ya kukujibu naomba nielezee kwanza kutu ni nini.KUTU ni dutu yenye rangi ya brown inayotengenezwa kwenye uso wa chuma(iron) wakati chuma kinapopambana(to react) kikemikakili na hewa ya oxygen(O2) na umande au mvuke(H2O).hivyo basi ili metali ipate kutu oxygen na majimaji(ni vitu muhimu kuwepo.chuma ni rahisi kushika kutu kwa sababu ni more electropositive ukilinganisha na metali nyingine kama aluminiamu copper dhahabu silver nikeli au zinc.Tukirudi kwenye sarafu ya mia tano ni kweli imetengenezwa kwa chuma lakini si asilimia mia kuna kiasi cha nikeli kimepakwa kwa juu(coated) na nikeli ni less electropositive hivyo inashika kwa kiasi kidogo sana na hii inatokana na utengenezwaji wa leya nyembamba ya oksaidi ya nikeli(impermeable oxide layer) inayozuia nikeli kushambuliwa zaidi na oxygen na majimaji hivyo kutokushika kutu.
 
Back
Top Bottom