Nimesikiliza album zote mbili za Antivirus ukiachana na matusi kuna ujumbe mkubwa kutoka kwa Sugu na inaonekana ana ushahidi wa kutosha wa aliyofanyiwa na Ruge.Sugu pia alijiandaa kwanza kwa kutafuta support kutoka kwa watu wengine ikiwemo Anti-clouds,ikiwemo wasanii wa Hiphop kama wakina Mapacha,Danny Msimamo etc ambayo wasanii wa hiphop sio waoga inapokuja suala la bif.
Kwa upande wa Jide pia mi naona ngoma bado nzito,Jide ana support kubwa pia ndani na nje ya nchi,wanomjua Ruge ni watu wa dar tu na hao 'wakubwa' wa serikali,huku vijijini kwenye redio one na tbc watu wanamjua na kumpenda Jide hivyo kitakachomuokoa hapa ni 'nguvu ya umma', nani alijua album ya matusi tena kwenda kwa clouds fm imevuma na tena haikuzuia chochote kwa Sugu kuwa Mbunge? Ukweli utaushinda uongo daima,hata Ruge akishinda hili alilofungulia kesi bado kuna mengine mengi yatakuja.