sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,685
- 1,111
Ni hatari sana majanga,misiba na kila aina ya ajali inapotokea inakuwa neema kwa upande fulani. Sitaki kuamini kufa kufaana lakini sasa nimeanza kuamini kutokana na uhalisia uliopo. Lilipotokea tetemeko la ardhi,maafa makubwa yaliwakumba ndugu zetu wa Kagera,wengine kuondokewa na wapendwa wao ikiwa pamoja na kupoteza rasilimali mali. Serikali iliweka utaratibu wa kukusanya pesa kwa ajili ya maafa hayo,kama rambirambi ya kuwafidia waliokumbwa na adha hiyo.
Lengo la serikali halikuwa baya,ila matendo yaliyofanywa na serikali kupitia mfuko wa maafa yalikuwa kinyume kabisa na makusudi yaliyotegemewa na wachangaji. Fedha zile hazikuwafikia wahanga ila zilingia serikalini na mpaka leo hatujui nini hatima ya michango ile ya wasamaria wema kwa ndugu zao.
Kilichotokea Kagera kwangu niliamini serikali ilijikwaa nakujikuta ikitumia fedha za wananchi waliowasaidia ndugu zao kujikwamua kwenye lindi la matatizo yaliyowakumba. Pamoja na kejeli za watawala kwa waathirika hao,serikali ilijiwekea kinga kuzuia michango ile isiwafikie walengo kwa kauli mbiu yao kuwa,serikali haikuleta tetemeko la ardhi kwenye ardhi ya viumbe wale. Kwa mantiki hiyo basi viumbe wale waliishia kulalamika dhuluma waliofanyiwa na serikali yao.
Kule Kagera tunaweza kusema kuwa serikali haikujuwa kuwa kula pesa za wahanga ni kosa ukizingatia ugeni wa serikali ya Magu ndiyo kwanza ilikuwa ina mwaka mmoja toka kusimikwa kwake, japokuwa angeweza kuomba msaada toka kwa serikali ya CCM ambayo ilikwisha tolewa madarakani kuhusu uzoefu wa matumizi ya pesa za majanga humlenga nani hasa kati ya serikali na wahanga.
Hili janga la Arusha limeniibua kifikra na kuamini kuwa jasiri kumbe huwa haachi asili yake, japo kuna tofauti kidogo angalau safari hii wahanga wa tukio la ajali lililosabaisha kupoteza makumi ya watoto wetu waliambulia kidogo kifuta machozi,lakini serikali iliendeleza kupanga matumizi ya shughuli ,angalau safari hii tulijuwa hesabu ya matumizi iliyotolewa na mtawala jasiri wa Arusha bwana Gambo.
Kilichotushtua wengi pamoja na serikali kuhodhi shughuli nzima ya mazishi,kitendo cha fedha za rambirambi kupelekwa kwenye mfuko wa maendeleo kwa ajili ya ukarabati wa hospitali ya Mount Meru,kuimeibua sintofahamu ya kutaka kujua nini adhima ya serikali kwa wananchi wake ikiwa majanga nayo ni chanzo cha mapato.
Sintofahamu iliyotuacha midomo wazi huenda ndiyo chachu ya kuwakamata meya wa jiji la Arusha na jopo lake walipokwenda kuhani msiba kwa wana familia wa st Lucky na kutoa ubani wao,kumbe siku hizi kutoa rambirambi kwa wafiwa bila kupata kibari cha mkuu wa mkoa ni kuhujumu mapato ya serikali?
Ikiwa majanga yatahesabika Kama sehemu ya chanzo cha mapato tutegemee nini kama taifa, yaani kwanza tufe michango ikipatikana ndiyo tufanyie utekelezaji wa bajeti za maendeleo!!!
Kwa staili ya maafa kuwa chanzo cha mapato ya serikali,Watanzania twafaa usalama wetu upo mashakani!!!!