Kwanini Rais Kikwete hakuongea na wananchi leo?

Kwanini Rais Kikwete hakuongea na wananchi leo?

MKONGA

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2015
Posts
667
Reaction score
458
Wataalam wa siasa na wanasiasa njooni hapa mtoe majibu kwa hili swali langu rahisi

1.Hivi ni kwanini Rais Kikwete hakuongea na wananchi leo siku ya Muungano na ni maadhimisho yake ya mwisho akiwa kama rais?
 
Ikulu pabaya panafuka moshi mambo si mambo pale jumba kubwa, yanayominywa kwasasa yakitoka nje nchi itatikisika
 
Anaogopa sana, kama Leo angetoa hotuba kura za ccm zingepungua zaidi , najua angekwaza tu wapiga kura
 
Wataalam wa siasa na wanasiasa njooni hapa mtoe majibu kwa hili swali langu rahisi

1.Hivi ni kwanini Rais Kikwete hakuongea na wananchi leo siku ya Muungano na ni maadhimisho yake ya mwisho akiwa kama rais?
Hizi Sherehe ni za kuuzia sura tu sio za kuongea ongea
 
hajawahi kufanya hivyo katika sikukuu ya muungano wala haogopi sasa amwogope nani mbowe?au ........
 
hajawahi kufanya hivyo katika sikukuu ya muungano wala haogopi sasa amwogope nani mbowe?au ........
Umempa jibu sahihi, sikukuu za Muungano huwa hazina hotuba.

Katika kumbukumbu zangu tokea enzi za uongozi wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, sikumbuki Rais yeyote aliyewahi kuhutubia sherehe za Muungano pale uwanja wa Uhuru.
 
Mimi niliona Mkuu wa kaya akitafuta tambuu ( BIG G) kama hajala wiki hivi hahahaaaaa nae ana njaa kali, #TUO8OKTOBA .
 
Huwa hakuna hotuba siku ya muungano wala siku ya uhuru.
 
hajawahi kufanya hivyo katika sikukuu ya muungano wala haogopi sasa amwogope nani mbowe?au ........

Ya jana ilikuwa na umuhimu maalum...!

Angeongea tu kuwaasa Watanzania kuhusu kuendeleza muungano..!
 
hajawahi kufanya hivyo katika sikukuu ya muungano wala haogopi sasa amwogope nani mbowe?au ........

Ya jana ilikuwa na umuhimu maalum, kwani ni ya mwisho kwake akiwa rais wa Jamhuri ya Muungano...!

Angeongea tu angalao kuwaasa Watanzania kuhusu kuendeleza muungano..!
 
tz50-14.jpg

Rais Kikwete akitoa hotuba katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano
 
Naye anazisoma nyakati, hawezii kuongelea kitu ambacho kipo kwa faida za wakubwa wakati wavuja jasho hawakitaki. Tanganyika oyeeeeeee.
 
Hana la kuongea kaharibu kila idara mpaka anajionea haya mwenyewe.
 
Back
Top Bottom